bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 28
Matthew 28
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 27
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
1
*Siku ya mapumziko ilipokwisha, siku ya kwanza ya juma kulipokucha, wakaenda Maria Magdalena na yule Maria mwingine kulitazama kaburi.
2
Mara kukawa na tetemeko kubwa la nchi. Kwani malaika wa Bwana alishuka toka mbinguni, akaja akalifingirisha lile jiwe, likatoka mlangoni, akalikalia.
3
Sura yake ilikuwa kama umeme, nguo zake zikang'aa kama chokaa juani.
4
Walinzi wakaingiwa na woga, wakatetemeka, wakawa kama wafu.
5
Malaika akawaambia wale wanawake akisema: Msiogope! Kwani ninajua, ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyewambwa msalabani.
6
Hayumo humu, kwani amefufuliwa, kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali, Bwana alipokuwa amewekwa!
7
Nanyi nendeni upesi, mwaambie wanafunzi wake kwamba: Amefufuliwa katika wafu! Tazameni, anawatangulia ninyi kwenda Galilea. Huko ndiko, mtakakomwona. Tazameni, nimekwisha kuwaambia.
8
Wakatoka upesi kaburini wakishikwa na woga, tena wakifurahi sana, wakaenda mbio kuwasimulia wanafunzi wake.
9
Mara Yesu akakutana nao, akasema: Salamu kwenu! Nao wakamjia, wakamshika miguu yake, wakamwangukia.
10
Ndipo, Yesu alipowaambia: Msiogope, nendeni, mwasimulie ndugu zangu, waende Galilea! Ndiko, watakakoniona.*
11
Walipokwenda zao, mara nao walinzi wakafika mjini mmoja mmoja, wakasimulia watambikaji wakuu yote yaliyokuwapo.
12
Wakakusanyika pamoja na wazee, wakala njama, wakatoa fedha nyingi za kuwapa wale askari,
13
wakawaambia: Semeni: Wanafunzi wake wamekuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala!
14
Neno hili likijulikana kwa mtawala nchi, sisi tutasema naye kwa werevu, ninyi msipate mahangaiko.
15
Kwa hiyo wakazichukua zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Nalo neno hili linasimuliwa kwa Wayuda mpaka leo.
16
*Wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilea, wakafika mlimani pale, Yesu alipowaagizia.
17
Walipomwona wakamwangukia, lakini wengine waliingiwa na mashaka.
18
Naye Yesu akawajia, akawaambia: Nimepewa nguvu zote mbinguni na nchini.
19
Nendeni, mkawafundishe wao wa mataifa yote, wawe wanafunzi wangu, mkiwabatizia Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu
20
na kuwafundisha, wayashike yote, niliyowaagiza! Tazameni, niko pamoja nanyi siku zote, mpaka dunia itakapokoma.*
← Chapter 27
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28