bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 12
Matthew 12
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 13 →
1
Siku zile Yesu alipita katika mashamba siku ya mapumziko; nao wanafunzi wake walipoona njaa wakaanza kukonyoa masuke, wakala.
2
Lakini Mafariseo walipoviona wakamwambia: Tazama, wanafunzi wako wanafanya yaliyo mwiko kuyafanya siku ya mapumziko.
3
Naye akawaambia: Hamkusoma, Dawidi alivyofanya alipoona njaa yeye na wenziwe?
4
Hapo aliingia Nyumbani mwa Mungu, wakaila mikate aliyowekewa Bwana, nayo kuila ni mwiko kwake na kwa wenziwe, huliwa na watambikaji peke yao.
5
Tena hamkusoma katika Maonyo, ya kuwa siku za mapumziko watambikaji wa pale Patakatifu huivunja miiko ya siku ya mapumziko, nao hawakosi?
6
Lakini nawaambiani: Hapa yupo aliye mkuu kuliko Patakatifu.
7
Lakini kama mngalitambua maana ya neno la kwamba: Huruma ndizo, nizitakazo, lakini vipaji vya tambiko sivyo, basi, hamngaliwawazia mabaya wasio na kosa.
8
Kwani Mwana wa mtu ni bwana wa siku ya mapumziko.*
9
Alipoondoka huko akaenda kuingia katika nyumba yao ya kuombea.
10
Akaona mtu mwenye mkono uliokaukiana. Wakamwuliza wakisema: Iko ruhusa kuponya siku ya mapumziko? maana walitafuta la kumsuta.
11
Nay akawaambia: Mwenye kondoo mmoja tu akitumbukiwa naye shimoni siku ya mapumziko, kwenu yuko asiyemkamata na kumwopoa?
12
Je? Mtu hapiti kondoo kabisa? Kwa hiyo iko ruhusa kufanya mema siku ya mapumziko.
13
Ndipo, alipomwambia yule mtu: Unyoshe mkono wako! Nao, alipounyosha, ukageuka kuwa mzima kama ule mwingine.
14
Lakini Mafariseo wakatoka, wakamlia njama ya kumwangamiza.
15
Yesu alipoyatambua akaondoka kule.
16
Watu wengi wakamfuata, akawaponya wote;
17
lakini akawatisha, wasimtangaze, kusudi litimie, mfumbuaji Yesaya alilolisema:
18
Tazameni, huyu ndiye mtoto wangu, niliyemchagua; ni mpendwa wangu, ambaye Roho yangu inapendezwa naye. Nitamtia Roho yangu, awatangazie wamizimu, ya kwamba hukumu yao iko.
19
Hatateta, wala hatapiga kelele, wala mtu hatamsikia kinywa chake majiani.
20
Utete uliopondeka hatauvunja kabisa, wala utambi unaotoka moshi bado hatauzima, mpaka aitokeze ile hukumu kuwa ya kushinda.
21
Jina lake ndilo, wamizimu watakalolingojea.
22
Hapo akaletewa mwenye pepo aliyekuwa kipofu na bubu. Alipomponya, yule bubu akapata kusema na kuona.
23
Ndipo, makundi ya watu waliposhangaa wote wakisema: Kumbe huyu siye mwana wa Dawidi?
24
Mafariseo walipoyasikia wakasema: Huyu hafukuzi pepo, isipokuwa kwa nguvu ya Belzebuli aliye mkuu wa pepo.
25
Kwa kuyajua hayo mawazo yao, Yesu akawaambia: Kila ufalme unapogombana wao kwa wao huwa mahame tu, nao kila mji au nyumba tu inapogombana wao kwa wao haitasimamika.
26
Naye Satani akimfukuza Satani mwenziwe amejigombanisha mwenyewe. Basi, ufalme wake utasimamikaje?
27
Nami nikiwafukuza pepo kwa nguvu ya Belzebuli, Je? Wana wenu huwafukuza kwa nguvu ya nani? Kwa hiyo hao ndio watakaowaumbua.
28
Lakini mimi nikiwafukuza pepo kwa nguvu ya Roho ya Mungu, ufalme wa Mungu umekwisha kuwafikia ninyi.
29
Au mtu atawezaje kuingia katika nyumba ya mwenye nguvu, aviteke vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Kisha ataweza kuiteka nyumba yake.
30
Asiye wa upande wangu hunikataa; naye asiyekusanya pamoja nami hutapanya.
31
Kwa hiyo nawaambiani: Kila kosa na kila neno la kumbeza Mungu watu wataondolewa, lakini la kumbeza Roho hawataondolewa.
32
Mtu ye yote atakayesema neno la kumkataa Mwana wa mtu ataondolewa; lakini mtu atakayesema neno la kumkataa Roho Mtakatifu hataondolewa, wala katika ulimwengu huu wa sasa, wala katika ule utakaokuja.
33
Mkipanda mti nzuri, basi mtapata hata matunda mazuri. Au mkipanda mti mwovu, basi, mtapata hata matunda maovu. Kwani mti hutambulikana kwa matunda yake.
34
Enyi wana wa nyoka, mnawezaje kusema mema, mlio wabaya? Kwani moyo unayoyajaa, ndiyo, kinywa kinayoyasema.
35
Mtu mwema hutoa mema katika kilimbiko chake chema, lakini mtu mbaya hutoa mabaya katika kilimbiko chake kibaya.
36
Nami nawaambiani: Siku ya hukumu watu wataulizwa kila neno baya walilolisema.
37
Kwani kwa maneno yako utapata wongofu, vile vile utapata hukumu kwa maneno yako.
38
Hapo walikuwapo waandishi na Mafariseo, wakamwuliza wakisema: Mfunzi, twataka, ufanye kielekezo, tukione.
39
Naye akajibu akiwaambia: Wao wa ukoo huu mbaya wenye ugoni wanatafuta kielekezo, lakini hawatapata kielekezo, ila kielekezo cha mfumbuaji Yona.
40
Kwani kama Yona alivyokuwa tumboni mwa nyangumi siku tatu mchana na usiku, vivyo naye Mwana wa mtu atakuwa ndani ya nchi siku tatu mchana na usiku.
41
Siku ya hukumu waume wa Niniwe watauinukia ukoo huu, wauumbue; kwani walijuta kwa tangazo la Yona. Tena tazameni, hapa yupo anayempita Yona!
42
Yule mfalme wa kike aliyetoka kusini atauinukia ukoo huu siku ya hukumu auumbue. Kwani yeye alitoka mapeoni kwa nchi, aje kuusikia werevu wa Salomo uliokuwa wa kweli. Tena tazameni, hapa yupo anayempita Salomo!
43
Pepo mchafu anapomtoka mtu hupita mahali pasipo na maji akitafuta kituo asikione.
44
Halafu husema: Nitarudi nyumbani mwangu, nilimotoka. Anapokuja huiona, ni tupu, tena imefagiwa na kupambwa;
45
ndipo, anapokwenda kuchukua pepo saba wengine walio wabaya kuliko yeye, wawe wenziwe; nao huingia, wakae humo: hivyo ya mwisho ya mtu yule yatakuwa mabaya kuliko ya kwanza. Ndivyo, vitakavyowapata wao wa ukoo huu ulio mbaya.
46
*Alipokuwa akisema bado na makundi ya watu, mara mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje kwa kumtaka, waseme naye. Mtu akamwambia:
47
Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje kwa kutaka, waseme na wewe.
48
Naye akajibu akimwambia yule aliyesema naye: Mama yangu ni nani? Nao ndugu zangu ni akina nani?
49
Akawanyoshea wanafunzi wake mkono, akasema: Watazameni walio mama yangu na ndugu zangu!
50
Kwani mtu ye yote atakayeyafanya, ayatakayo Baba yangu alioko mbinguni, huyo ndiye ndugu yangu na dada yangu na mama yangu.*
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 13 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28