bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 5
Matthew 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 6 →
1
*Alipoyaona hayo makundi ya watu akapanda mlimani, akakaa, nao wanafunzi wake wakamkaribia.
2
Ndipo, alipokifumbua kinywa chake, akawafundisha akisema:
3
Wenye shangwe ndio walio maskini rohoni mwao, maana hao ufalme wa mbingu ni wao.
4
Wenye shangwe ndio wanaosikitika, maana hao watatulizwa.
5
Wenye shangwe ndio wapole, maana hao watairithi nchi.
6
Wenye shangwe ndio wenye njaa na kiu ya kupata wongofu, maana hao watashibishwa.
7
Wenye shangwe ndio wenye huruma, maana hao watahurumiwa.
8
Wenye shangwe ndio waliotakata mioyoni mwao, maana hao watamwona Mungu.
9
Wenye shangwe ndio wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu.
10
Wenye shangwe ndio wanaofukuzwa kwa ajili ya wongofu wao, maana hao ufalme wa mbingu ni wao.
11
Nanyi mtakuwa wenye shangwe, watu watakapowatukana na kuwafukuza na kuwasingizia maneno mabaya yo yote yaliyo ya uwongo kwa ajili yangu mimi.
12
Furahini na kushangilia! Kwani mshahara wenu ni mwingi mbinguni. Kwani ndivyo, walivyowafukuza wafumbuaji waliowatangulia.*
13
*Ninyi m chumvi ya nchi. Lakini chumvi ikiwa imepotewa na ukolezi, itatiwa kitu gani, ipate kukolea tena? Hakuna kitu tena, ilichokifalia, itatupwa tu nje, ikanyagwe na watu.
14
Ninyi m mwanga wa ulimwengu. Mji ukiwa juu ya mlima haufichiki.
15
Nao watu wakiwasha taa hawaiweki chini ya kapu, ila huiweka juu ya mwango; ndivyo inavyowaangazia wote waliomo nyumbani.
16
Vivyo mwanga wenu uangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu alioko mbinguni.*
17
Msiniwazie, ya kuwa nimejia kuyatangua Maonyo au maneno ya Wafumbuaji. Sikujia kutangua, nimejia kutimiza.
18
Kweli nawaambiani: Mpaka hapo, mbingu na nchi zitakapokoma, hata kiandiko kimoja au kichoro kimoja kilichomo katika Maonyo hakitakoma, isipokuwa yametimizwa yote.
19
Mtu akiondoa moja tu katika maagizo hayo, ijapo liwe dogo, na kufundisha watu hivyo, huyo ataitwa mdogo kuliko wote katika ufalme wa mbingu; lakini mtu akiyafanya maagizo hayo na kufundisha watu hivyo, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbingu.
20
Kwani nawaambiani: *Wongofu wenu usipoupita wongofu wao waandishi na Mafariseo, hamtaingia kabisa katika ufalme wa mbingu.
21
Mmesikia, ya kuwa watu wa kale waliambiwa: Usiue! Mtu akiua, itampasa, ahukumiwe.
22
Lakini mimi nawaambiani: Kila anayemwonea ndugu yake chuki, itampasa, ahukumiwe. Naye atakayemwambia ndugu yake: Mshenzi wee! itampasa, ahukumiwe na baraza ya wakuu wote. Lakini atakayemtukana ndugu yake, itampasa, atupwe shimoni mwa moto.
23
Ukipeleka kipaji chako mezani pa Bwana, ukakumbuka hapo, ya kuwa ndugu yako ana mfundo moyoni kwa ajili yako,
24
basi, kwanza kiache kipaji chako mbele ya meza ya Bwana! Uende kwanza, upatane na ndugu yako! Kisha urudi, ukitoe kipaji chako!
25
Umwitikie mshtaki wako upesi ukiwa naye, mngaliko njiani! Maana mshtaki wako asikupeleke kwa mwenye hukumu, naye mwenye hukumu asikutie mkononi mwa askari, ukatiwa kifungoni.
26
Kweli nakuambia: Hutatoka humo kabisa, mpaka utakapomaliza kulipa, isisalie hata senti moja*
27
Mmesikia ya kuwa ilisemwa: Usizini!
28
Lakini mimi nawaambiani: Kila mtu anayetazama mwanamke kwa kumtamani, basi, huyo amekwisha zini naye moyoni mwake.
29
Nawe kama jicho lako la kuume linakukwaza, ling'oe, ulitupe mbali! kwani itakufaa, kiungo kimoja tu kiangamie, kuliko mwili wako mzima ukitupwa shimoni mwa moto.
30
Nawe kama mkono wako wa kuume unakukwaza, uukate, uutupe mbali! Kwani itakufaa, kiungo kimoja tu kiangamie, kuliko mwili wako mzima ukijiendea shimoni mwa moto.
31
Tena ilisemwa: Mtu akimwacha mkewe ampe cheti cha kuachana.
32
Lakini mimi nawaambiani: kila mtu anayemwacha mkewe, isipokuwa kwa ajili ya ugoni, huyo anamzinisha. Naye atakayeoa mke aliyeachwa anazini.
33
Tena mmesikia, ya kuwa watu wa kale waliambiwa: Usiape kiapo cha uwongo, lakini umtimizie Mungu, uliyomwapia!
34
Lakini mimi nawaambiani: Usiape na kutaja yoyote, wala mbingu, kwani ndicho kiti cha kifalme cha Mungu;
35
Wala nchi, kwani ndipo pa kuiwekea miguu yake; wala Yerusalemu, kwani ndio mji wa mfalme aliye mkuu;
36
wala kichwa chako, kwani hata unywele mmoja tu huwezi kuugeuza uwe mweupe au mweusi.
37
Mkisema: Ndio, iwe ndio kweli! Au mkisema: Sio, iwe sio kweli! Lakini yanayoyapita hayo hutoka kwa Mbaya.
38
Mmesikia, ya kuwa ilisemwa: Jicho kwa jicho, jino kwa jino!
39
Lakini mimi nawaambiani: Msibishane na mbaya! Lakini mtu akikupiga kofi shavu la kuume, mgeuzie la pili, alipige nalo!
40
Mtu akitaka kushtakiana na wewe, apate kuichukua shuka yako, basi, umwachie na kanzu!
41
Naye atakayekushurutiza kwenda naye nusu saa, basi, nenda naye saa nzima!
42
Anayekuomba umpe, naye anayetaka kukopa kwako usimgeukie mgongo!
43
Mmesikie, ya kuwa ilisemwa: Umpende mwenzio, naye adui yako umchukie!
44
Lakini mimi nawaambiani: Wapendeni adui zenu! Wabarikini wanaowaapiza! Wafanyieni mazuri wanaowachukia! Waombeeni wanaowachokoza na kuwafukuza!
45
Fanyeni hivi, mpate kuwa wana wa Baba yenu alioko mbinguni! Kwani yeye huwacheshea jua lake wabaya na wema, tena huwanyeshea mvua waongofu nao wapotovu.
46
Kwani mkiwapenda wanaowapendani mtapata mshahara gani? Je? Hata watoza kodi hawafanyi hivyo hivyo?
47
Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu mnawapitaje wengine? Je? Hata wamizimu hawafanyi vivyo hivyo?
48
Basi, ninyi mwe watimilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mtimilifu!
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28