bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 7
Matthew 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 8 →
1
Msiumbue mtu, msije mkaumbuliwa!
2
Kwani kama mnavyowaumbua wengine, ndivyo, mtakavyoumbuliwa wenyewe. Kipimo, mnachopimia wengine, ndicho, mtakachopimiwa nanyi.
3
Nawe unakitazamiani kibanzi kilichomo jichoni mwa ndugu yako, lakini gogo lililomo jichoni mwako wewe hulioni?
4
Au utamwambiaje ndugu yako: Ngoja, nikitoe kibanzi katika jicho lako, wewe mwenyewe ukiwa unalo gogo zima jichoni mwako?
5
Mjanja, kwanza litoe gogo katika jicho lako! Kisha utazame vema, ndivyo upate kukitoa kibanzi katika jicho la ndugu yako!
6
Kilichotakata msiwape mbwa, wala msiwatupie nguruwe ushanga wenu wa lulu, wasije wakaukanyaga kwa miguu yao na kuwageukia na kuwararua ninyi.
7
Ombeni! ndipo, mtakapopewa. Tafuteni! ndipo, mtakapoona. Pigeni hodi! ndipo, mtakapofunguliwa mlango.
8
Kwani kila anayeomba hupewa, naye anayetafuta huona, naye anayepiga hodi hufunguliwa mlango.
9
Au kwenu yuko mtu, mwanawe anapomwomba mkate, ampe jiwe?
10
Au anapomwomba samaki, ampe nyoka?
11
Basi, ninyi mlio wabaya mkijua kuwapa watoto wenu vipaji vyema, Baba yenu alioko mbinguni asizidi kuwapa mema wanaomwomba?
12
Yo yote, mnayotaka, watu wawafanyie ninyi, nanyi mwafanyie yaleyale! Kwani hayo ndiyo Maonyo na Wafumbuaji.
13
*Uingieni mlango ulio mfinyu! Kwani liko lango lililo pana, nayo njia yake ni kubwa; ndiyo inayokwenda penye kuangamizwa, nao wanaoingia mle ni wengi.
14
Tena uko mlango ulio mfinyu, nayo njia yake inasonga; ndiyo inayokwenda penye uzima, lakini wanaoiona ni wachache.
15
Jilindeni kwa ajili ya wafumbuaji wa uwongo! Wanawajia wamevaa kama kondoo, lakini mioyoni ni mbwa wa mwitu wenye ukali.
16
Kwa matunda yao mtawatambua. Je? Huchuma zabibu miibani? Au huchuma kuyu mikongeni?
17
Hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; lakini mti mwovu huzaa matunda mabaya.
18
Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu hauwezi kuzaa matunda mazuri
19
Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa, utupwe motoni.
20
Kwa hiyo mtawatambua kwa matunda yao.
21
Miongoni mwao wanaoniita: Bwana! Bwana! sio wote wakaoingia katika ufalme wa mbingu, ni wao tu wanaoyafanyiza, Baba yangu alioko mbinguni ayatakayo.
22
Siku ile wengi wataniuliza: Bwana, sisi hatukufumbua kwa Jina lako? Hatukufukuza pepo kwa Jina lako? Hatukufanya mengi yenye nguvu kwa Jina lako?
23
Ndipo, nitakapowaambia waziwazi: Sijawatambua ninyi kabisa. Ondokeni kwangu, mliofanya maovu!*
24
*Basi, kila mtu anayeyasikia haya maneno yangu na kuyafanyiza atafanana na mtu mwenye akili aliyeijenga nyumba yake mwambani.
25
Mvua kubwa ikanyesha, mito ikajaa, pepo zikavuma, vyote vikaipiga ile nyumba, lakini haikuanguka, kwani misingi yake ilikuwa imejengwa mwambani.
26
Lakini kila mtu anayeyasikia haya maneno yangu asipoyafanyiza atafanana na mtu mpumbavu aliyeijenga nyumba yake mchangani.
27
Mvua kubwa ikanyesha, mito ikajaa, pepo zikavuma vyote vikaipiga ile nyumba, basi, ikaanguka, anguko lake likawa kubwa.
28
Ikawa, Yesu alipokwisha kuyasema maneno haya, makundi ya watu walishangazwa na mafundisho yake.
29
Kwani alikuwa akiwafundisha kama wenye nguvu, si kama waandishi wao.*
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28