bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 14
Matthew 14
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 15 →
1
Siku zile mfalme Herode alipousikia uvumi wa Yesu,
2
akawaambia watoto wake: Huyo ndiye Yohana Mbatizaji, amefufuka katika wafu, kwa sababu hii nguvu hizo humtendesha kazi.
3
Kwani Herode alikuwa amemkamata Yohana, akamfunga, akamtia kifungoni kwa ajili ya Herodia, mke wa nduguye, Filipo.
4
Kwani Yohana alimwambia: Ni mwiko kwako kuwa naye.
5
Naye alitaka kumwua, lakini aliwaogopa watu, kwani walimwona Yohana kuwa mfumbuaji.
6
Ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti Herodia akacheza ngoma mbele yao, akampendeza Herode.
7
Ndipo, alipomwapia kumpa cho chote, atakachomwomba.
8
Naye kwa hivyo, alivyokwisha kuhimizwa na mama yake, akasema: Nipe sasa hivi katika chano kichwa chake Yohana Mbatizaji!
9
Mfalme akasikitika, lakini kwa ajili ya viapo vyake na kwa ajili ya wale waliokaa naye chakulani akaagiza, apewe.
10
Akatuma mtu, akamkata Yohana kichwa kifungoni.
11
Kisha hicho kichwa chake kikaletwa katika chano, msichana akapewa, akampelekea mama yake.
12
Kisha wanafunzi wake wakaja, wakautwaa mwili wake, wakauzika; kisha wakaenda, wakampasha Yesu habari.
13
Yesu alipoyasikia akaingia chomboni, akaondoka huko kwenda peke yake mahali palipokuwa pasipo watu.
14
Nayo makundi ya watu walipovisikia wakamfuata kwa miguu toka mijini. Yesu alipotoka chomboni akaona, watu ni wengi sana, akawaonea uchungu, akawaponya waliokuwa hawawezi.
15
Ilipokuwa jioni, wanafunzi wake wakamjia, wakasema: Hapa tulipo ni nyika, nazo saa za mchana zimepita; basi, waage hawa watu wengi, waende zao vijijini, wajinunulie vyakula!
16
Yesu akawaambia: Waendeje? Wapeni ninyi vyakula!
17
Nao wakamwambia: Hatuna kitu hapa ila mikate mitano na visamaki viwili.
18
Naye akasema: Nileteeni hapa!
19
Akawaagiza hao watu wengi, wakae chini majanini. Akaitwaa ile mikate mitano na vile visamaki viwili, akatazama juu mbinguni akaviombea, akawamegea, akawapa wanafunzi ile mikate; nao wanafunzi wakawapa wale watu wengi.
20
Wakala wote, wakashiba. Kisha wakayaokota makombo ya mikate yaliyosalia, wakajaza vikapu kumi na viwili.
21
Nao waliokula walikuwa waume tu kama 5000 pasipo wanawake na watoto.
22
Kisha Yesu akawashurutisha wanafunzi waingie chomboni, wamtangulie kwenda ng'ambo, mpaka yeye kwanza awaage makundi ya watu.
23
Naye alipokwisha kuwaaga makundi ya watu akapanda mlimani peke yake kuomba. Jua lilipokwisha kuchwa, akawa huko peke yake.
24
Nacho chombo kilikuwa kimeendelea kitambo kirefu kikahangaishwa na mawimbi, kwani upepo uliwatokea mbele.
25
Ilipofika zamu ya nne ya usiku, akawajia akienda juu ya bahari.
26
Wanafunzi walipomwona, anavyokwenda juu ya bahari, wakatetemeka wakisema: ni mzimu! wakalia kwa woga.
27
Papo hapo Yesu akawaambia akisema: Tulieni! Ni miye, msiogope!
28
Petero akamjibu akisema: Bwana, ukiwa ni wewe, agiza nije kwako majini juujuu!
29
Alipomwambia: Njoo! Petero akashuka chomboni, akaenda juu ya maji, amfikie Yesu.
30
Lakini alipotazama, upepo ulivyo na nguvu, akaogopa, akaanza kuzama majini, akapiga kelele akisema: Bwana, niokoa!
31
Mara Yesu akaunyosha mkono, akamshika, akamwambia: Mbona unanitegemea kidogo tu? Mbona umeingiwa na wasiwasi?
32
Walipopanda chomboni, upepo ukakoma.
33
Nao waliokuwamo chomboni wakamwangukia wakisema: Kweli ndiwe Mwana wa Mungu!
34
Walipokwisha vuka wakafika nchini kwa Genesareti.
35
Wenyeji wa huko walipomtambua wakatuma watu kwenda katika nchi zote za pembenipembeni, wakamletea wote waliokuwa hawawezi.
36
Wakambembeleza, wamguse pindo la kanzu yake tu; nao wote walioligusa wakapona kabisa.
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28