bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 8
Matthew 8
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 9 →
1
*Alipotelemka mlimani, makundi mengi ya watu wakamfuata.
2
Mara akaja mwenye ukoma, akamwangukia akisema: Bwana, ukitaka waweza kunitakasa.
3
Ndipo, Yesu aliponyosha mkono, akamgusa akisema: Nataka, utakaswe. Mara ukoma ukatakaswa.
4
Kisha Yesu akamwambia: Tazama, usimwambie mtu! Ila uende, ujionyeshe kwa mtambikaji, ukitoe kipaji, Mose alichokiagiza, kije kinishuhudie kwao.
5
Yesu alipoingia Kapernaumu, mkubwa wa askari akamjia, akambembeleza akisema:
6
Bwana, mtoto wangu amelala nyumbani, anaumia vibaya kwa kulemaa.
7
Yesu akamwambia: Mimi ninakuja kumponya
8
Lakini yule mkubwa wa askari akamjibu akisema: Bwana, hainipasi, uingie kijumbani mwangu, ila sema neno tu! ndipo, mtoto wangu atakapopona!
9
Kwani nami ni mtu wa serikali, ninao askari chini yangu. Nami nikimwambia huyu: Nenda! basi, huenda; na mwingine: Njoo! huja; nikimwagiza mtumishi wangu: Vifanye hivi! huvifanya.
10
Yesu alipoyasikia akastaajabu, akawaambia waliomfuata: Kweli nawaambiani: Kwa Waisiraeli sijaona bado mtu mwenye kunitegemea kama huyu.
11
Lakini nawaambiani: Wengi watatoka maawioni na machweoni kwa jua, watakaa chakulani pamoja na Aburahamu na Isaka na Yakobo katika ufalme wa mbingu,
12
lakini wana wa huo ufalme watatupwa penye giza lililoko nje; ndiko, kitakakokuwa kilio na kukereza meno.
13
Kisha Yesu akamwambia mkubwa wa askari: Nenda kwenu, na uyapate uliyoyategemea! Saa ileile mtoto wake akapona.*
14
Ikawa, Yesu alipoingia nyumbani mwa Petero, akamwona mama ya mkewe Petero, amelala kwa kuwa na homa.
15
Alipomgusa mkono, homa ikamwacha, akainuka, akamtumikia.
16
Ilipokuwa jioni, wakampelekea wengi waliopagawa na pepo; naye akawafukuza pepo kwa neno tu. Nao wote waliokuwa hawawezi akawaponya,
17
kusudi litimizwe lililosemwa na mfumbuaji Yesaya: Yeye ameyachukua manyonge yetu, akajitwisha maumivu yetu.
18
Lakini Yesu alipoona, watu wengi wakimzunguka, akaagiza, wavuke kwenda ng'ambo.
19
Ndipo, mwandishi mmoja alipomjia, akamwambia: Mfunzi, nitakufuata po pote, utakapokwenda.
20
Yesu akamwambia: Mbweha wanayo mapango, nao ndege wa angani wanavyo vituo, lakini Mwana wa mtu hana pa kukilazia kichwa chake.
21
Mwanafunzi wake mwingine akamwambia: Bwana, nipe ruhusa, kwanza niende, nimzike baba yangu!
22
Yesu akamwambia: Nifuata mimi, waache wafu, wazikane wao kwa wao!
23
*Alipoingia chomboni, wanafunzi wake wakafuatana naye.
24
Mara kukawa na msukosuko mkubwa baharini, hata chombo kilifunikizwa na mawimbi, lakini yeye alikuwa amelala usingizi.
25
Ndipo, walipomjia, wakamwamsha wakisema: Bwana, tuokoe, tunaangamia!
26
Yesu akawaambia: Mbona mnaogopa hivyo? Mbona mnanitegemea kidogo tu? Kisha akainuka, akaukaripia upepo na bahari, kukawa kimya kabisa.
27
Lakini watu wakastaajabu wakisema: Ni mtu gani huyu, ya kuwa hata upepo na bahari zinamtii?*
28
Alipofika ng'ambo katika nchi ya Wagadara, watu wawili waliopagawa na pepo wakakutana naye wakitoka penye makaburi, ni wakorofi mno; kwa hiyo mtu hakuweza kuipita njia ile.
29
Mara wakapiga kelele wakisema: Tuko na jambo gani sisi na wewe, mwana wa Mungu? Umejia hapa kutuumiza, siku zetu zikiwa hazijatimia bado?
30
Mbali yao kulikuwako kundi la nguruwe wengi waliokuwako malishoni.
31
Wale pepo wakambembeleza wakisema: Ukitufukuza, tutume, tuliingie lile kundi la nguruwe!
32
Yesu alipowaambia: Haya! Nendeni! ndipo, pepo walipowatoka, wakawaingia nguruwe. Mara kundi lote likatelemka mbio mwambani, wakaingia baharini, wakafa majini;
33
lakini wachungaji wakakimbia, wakaenda zao mjini, wakayatangaza yote, hata mambo ya wenye pepo.
34
Mara watu wa mji wakatoka wote, wakutane na Yesu. Walipomwona wakambembeleza, atoke mipakani kwao.
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28