bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 24
Matthew 24
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 25 →
1
Yesu alipotika Patakatifu akaenda zake. Wakamjia wanafunzi wake, wakamwonyesha majengo ya hapo Patakatifu;
2
ndipo, alipojibu akiwaambia: Je? Mwayatazama haya yote? Kweli nawaambiani: Hapa halitaachwa hata jiwe moja juu ya jiwe lenziwe lisiloporomoshwa chini.
3
Kisha alipokaa mlimani pa michekele, wanafunzi wakamjia; walipokuwa peke yao wakasema: Tuambie, hayo yatakuwapo lini? Tena kielekezo cha kurudi kwako na cha mwisho wa dunia ni nini?
4
Yesu akajibu akiwaambia: Angalieni, mtu asiwapoteze!
5
Kwani wengi watakuja kwa jina langu na kusema: Mimi ni Kristo; nao watapoteza wengi.
6
Tena mtasikia vita na mavumi ya vita; vitazameni tu, msivihangaikie! Kwani hivyo sharti viwepo, lakini huo sio mwisho.
7
Kwani watainukiana taifa na taifa, tena wafalme na wenzao wafalme; mahali penginepengine patakuwa na kipundupindu, pengine na njaa, pengine na matetemeko.
8
Lakini hayo yote ni mwanzo tu wa uchungu.
9
Hapo watatoa ninyi, mpate kuumizwa, hata kuuawa, tena mtachukiwa na makabila yote kwa ajili ya Jina langu.
10
Hapo ndipo, wengi watakapokwazwa, watoane wenyewe kila mtu na mwenziwe kwa kuchukiana wao kwa wao.
11
Hata wafumbuaji wa uwongo wengi watainuka na kupoteza wengi.
12
kwa sababu upotovu utazidi kuwa mwingi, upendo wa wengi utapoa.
13
Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokoka.
14
Nao huu utume mwema wa ufalme wa Mungu utatangawa ulimwenguni mote, uje, unishuhudie kwa wamizimu wote. Kisha ndipo, mwisho utakapokuja.
15
*Hapo ndipo, mtakapochafukwa mioyo mkiona, mwangamizaji atapishaye akisimama mahali Patakatifu, kama mfumbuaji Danieli alivyosema; mwenye kupasoma hapa sharti aangalie, ajue maana!
16
Siku zile watakaokuwako Yudea na wakimbilie milimani!
17
Mtu atakayekuwapo nyumbani juu asishuke kuvichukua vilivyomo nyumbani mwake!
18
Naye atakayekuwako shambani asirudi nyuma kuichukua nguo yake!
19
Lakini watakaoona vibaya zaidi ndio wenye mimba na wenye kunyonyesha siku zile.
20
Lakini ombeni, kukimbia kwenu kusitimie siku za kipupwe wala siku ya mapumziko!
21
Kwani hapo patakuwa na maumivu makuu kuyapita yote yaliyopatikana tangu mwanzo wa ulimwengu mpaka sasa, hata halafu hayatapatikana tena kama hayo.
22
Nazo siku zile kama hazingalipuinguzwa, hangaliokoka mtu hata mmoja. Lakini kwa ajili ya wale waliochaguliwa siku zile zitapunguzwa.
23
Hapo mtu akiwaambia: Tazama, huyu hapa ni Kristo! au akisema: Yule kule! msiitikie!
24
Kwani watainuka makristo wa uwongo na wafumbuaji wa uwongo; nao watatoa vielekezo vikubwa na vioja, wawapoteza hata waliochaguliwa, kama inawezekana.
25
Tazameni, nimetangua kuwaambia ninyi.
26
Basi, watakapowaambia ninyi: Tazameni, yuko jangwani! msitoke kwenda kule! Au: Yule! Yumo nyumbani! msiitikie!
27
Kwani kama umeme unavyotoka maawioni, ukamulika mpaka machweoni, ndivyo, kutakavyokuwa kurudi kwake Mwana wa mtu.
28
Penye nyamafu ndipo, tai watakapokusanyikia.*
29
Maumivu ya siku zile yatakapopita, papo hapo jua litakuwa jeusi lenye giza, nao mwezi hautaumulikisha mwanga wake, nazo nyota zitaanguka toka mbinguni, nazo nguvu za mbingu zitatukutishwa.
30
Hapo ndipo, patakapoonekana mbinguni kielekezo cha Mwana wa mtu. Ndipo, watakapoomboleza wao wa makabila yote ya nchi, watakapomwona Mwana wa mtu, anavyokuja juu ya mawingu toka mbinguni mwenye nguvu na utukufu mwingi.
31
Naye atawatuma malaika zake wenye mabaragumu yanayolia sana, wawakusanye waliochaguliwa naye toka pande zote nne, upepo unapotokea, waanzie mwanzoni kwa mbingu, waufikishe mwisho wake.
32
Jifundisheni mfano kwa mkuyu: matawi yake yanapochipua na kuchanua majani, mnatambua, ya kuwa siku za vuli ziko karibu.
33
Vivyo hivyo nanyi mtakapoyaona hayo yote tambueni, ya kuwa mwisho umewafikia milangoni!
34
Kweli nawaambiani: Kizazi hiki hakitakoma, mpaka yatakapokuwapo hayo yote.
35
Mbingu na nchi zitakoma, lakini maneno yangu hayatakoma.
36
Lakini ile siku na saa yake itakapofikia, mtu hapajui, wala malaika wa mbingu, wala Mwana, ila Baba peke yake tu.
37
Kama vilivyokuwa siku za Noa, ndivyo kutakavyokuwa kurudi kwake Mwana wa mtu.
38
Kwani siku zile zilizoyatangulia yale mafuriko makubwa ya maji walikuwa wakila, hata wakinywa, wakioa, hata wakiozwa mpaka siku, Nao alipoingia katika chombo kikubwa.
39
Hawakuyatambua, mpaka mafuriko makubwa ya maji yakaja, yakawachukua wote pia. Ndivyo, kutakavyokuwa hata kurudi kwake mwana wa mtu.
40
Hapo wawili watakuwa shambani, mmoja atapokewa, mmoja ataachwa.
41
Hapo wawili watakuwa shambani, mmoja atapokewa, mmoja ataachwa.
42
Kwa hiyo kesheni! Kwani hamwijui siku, atakapojia Bwana wenu.
43
Lakini litambueni neno hili: Kama mwenye nyumba angaliijua zamu, mwizi atakayojia, angalikesha, asiache, nyumba yake ibomolewe.
44
Kwa sababu hiyo nanyi mwe tayari! Kwani Mwana wa mtu atajia saa, msiyomwazia.
45
Basi, yuko nani aliye mtumwa mwelekevu na mwerevu, bwana wake akimpa kuwatunza wa nyumbani mwake, awape vyakula, saa yao itakapofika?
46
Mwenye shangwe ni mtumwa yule, bwana wake atakayemkuta, akifanya hivyo, atakapokuja.
47
Kweli nawaambiani: Atampa kuzitunza mali zake zote.
48
Lakini mtumwa aliye mwovu atasema moyoni mwake: Bwana wangu anakawia,
49
akaanza kuwapiga watumwa wenziwe na kula na kunywa pamoja na walevi.
50
Basi, bwana wake mtumwa yule atamjia siku, asiyomngojea, na saa, asiyoitambua,
51
kisha atamchangua kuwa vipande viwili, nalo fungu lake atampa pamoja na wajanja. Ndiko, kitakakokuwa kilio na kukereza meno.
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 25 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28