bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 15
Matthew 15
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 16 →
1
Ndipo, walipomjia Yesu Mafariseo na waandishi waliotoka Yerusalemu, wakasema:
2
Kwa sababu gani wanafunzi wako hawayafuati mazoezo ya wakale? Kwani hawanawi mikono wakila chakula.
3
Ndipo, alipowajibu akisema: Nanyi sababu gani hamlifuati agizo lake Mungu kwa ajili ya mazoezo ya wakale wenu?
4
Kweli Mungu alisema: Mheshimu baba yako na mama yako! na tena: Atakayemwapiza baba au mama sharti afe kwa kuuawa!
5
Lakini ninyi husema: Mtu akimwambia baba au mama: Mali, unazozitaka, nikusaidie nazo, amepewa Mungu, basi, ni vema.
6
Hivyo hatamheshimu baba na mama tena; ndivyo, mlivyolitangua Neno la Mungu kwa ajili ya mazoezo ya wakale wenu.
7
Enyi wajanja, Yesaya aliwafumbua vizuri hayo mambo yenu aliposema:
8
Ukoo huu huniheshimu kwa midomo tu, lakini mioyo yao inanikalia mbali.
9
Hivyo hunicha bure, kwani hufundisha mafundisho yaliyto maagizo ya watu tu.
10
Akaliita kundi la watu, akawaambia: Sikilizeni, mjue maana!
11
Kinachoingia kinywani sicho kinachomtia mtu uchafu, ila kinachotoka kinywani ndicho kinachomtia mtu uchafu.
12
Ndipo, wanafunzi walipomjia, wakamwuliza: Unajua, ya kuwa Mafariseo walikwazwa walipolisikia neno hilo?
13
Naye akajibu akisema: Kila mmea, asioupanda Baba yangu wa mbinguni, utang'olewa.
14
Waacheni hao! Ni mapofu wenye kuongoza vipofu wenzao. Kipofu akimwongoza kipofu mwenziwe, wote wawili watatumbukia shimoni.
15
Petero akajibu, akamwambia: Tuelezee mfano huu!
16
Naye akasema: Kumbe nanyi hajaerevuka hata leo!
17
Hamjui, kila kitu kinachoingia kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni?
18
Lakini yanayotoka kinywani mwa mtu yametoka moyoni mwake, nayo ndiyo yanayomtia mtu uchafu.
19
Kwani moyoni hutoka mawazo mabaya: uuaji, uzinzi, ugoni, wizi, usingiziaji, matusi.
20
Haya ndiyo yanayomtia mtu uchafu; lakini kula na mikono isiyonawiwa hakumtii mtu uchafu.
21
*Yesu alipotika huko akajiepusha kwenda pande za Tiro na Sidoni.
22
Mara mwanamke wa Kikanaani aliyekaa mipakani huko akatokea, akapaza sauti akisema: Nihurumie, Bwana, mwana wa Dawidi! Binti yangu anapagawa vibaya na pepo.
23
Lakini hakumjibu neno. Wanafunzi wake wakamjia, wakamwomba wakisema: Mwache, aende zake! Kwani anatupigia kelele nyuma yetu.
24
Naye akajibu: Sikutumwa pengine, ni kwao tu walio kondoo waliopotea wa mlango wa Isiraeli.
25
Naye mwanamke akaja, akamwangukia, akasema: Bwana, nisaidie!
26
Naye akajibu akisema: Haifai kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia vijibwa.
27
Mwanamke akasema: Ndio Bwana, lakini nao vijibwa hula makombo yanayoanguka mezani pa bwana zao.
28
Ndipo, Yesu alipojibu akimwambia: Mama, umenitegemea kabisa. Na uvipate unavyovitaka! Saa ile ile binti yake akapona.*
29
Kisha Yesu akaondoka huko, akafika kandokando ya bahari ya Galilea, akapanda mlimani, akakaa huko.
30
Wakamjia makundi mengi ya watu walio na viwete na wenye vilema na vipofu na mabubu na wengine wengi pamoja nao. Wakawaweka miguuni pa Yesu, naye akawaponya.
31
Ikawa, makundi ya watu wakastaajabu waliupoona, mabubu wakisema, nao waliolemaa wakiwa wazima, nao viwete wakitembea, nao vipofu wakiona. Wakamtukuza Mungu wa Isiraeli.
32
Yesu akawaita wanafunzi wake, akasema: Kundi hili la watu nalionea uchungu, kwa kuwa wameshinda kwangu siku tatu, wasione chakula. Nami sitaki kuwaaga, waende zao pasipo kula, maana wasije, wakazimia njiani.
33
Wanafunzi wakamwambia: Hapa nyikani tutapata wapi mikate inayotosha kuwashibisha watu walio wengi kama hawa?
34
Yesu akawauliza: Mnayo mikate mingapi? Nao waliposema: Tunayo saba na visamaki vichache,
35
akawaagiza hao watu wengi, wakae chini.
36
Kisha akaitwaa ile mikate saba na samaki, akashukuru, akaimega akawapa wanafunzi, nao wanafunzi wakawapa wao wa makundi ya watu.
37
Wote wakala, wakashiba; kisha wakayaokota makombo ya mikate yaliyosalia, wakajaza makanda saba.
38
Nao waliokula walikuwa waume tu 4000 pasipo wanawake na watoto.
39
Kisha akawaaga makundi, waende zao, akaingia chomboni, akaja mipakani kwa Magadala.
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 16 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28