bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 11
Matthew 11
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 12 →
1
Yesu alipokwisha kuwaagiza haya wanafunzi wake kumi na wawili akaondoka, alikokuwa, akaenda kufundisha watu na kuwapigia ile mbiu katika miji yao.
2
*Lakini Yohana alipozisikia mle kifungoni kazi zake Kristo akatuma wanafunzi wake wawili,
3
akamwuliza: Wewe ndiwe mwenye kuja, au tungoje mwingine?
4
Yesu akajibu akiwaambia: Rudini, mmsimulie Yohana, mliyoyasikia nayo mliyoyaona:
5
vipofu wanaona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanapigiwa mbiu njema.
6
Tena mwenye shangwe ndiye asiyejikwaa kwangu.
7
Wao walipokwenda zao, Yesu akaanza kusema na yale makundi ya watu mambo ya Yohana: Mlipotoka kwenda nyikani mlikwenda kutazama nini? Mlikwenda kutazama utete unaotikiswa na upepo?
8
Au mlitoka kutazama nini? Mlikwenda kutazama mtu aliyevaa mavazi mororo? Tazameni, wanaovaa mavazi mororo wamo nyumbani mwa wafalme.
9
Au mlitoka kutazama nini? Mlitaka kuona mfumbuaji? Kweli, nawaambiani: Ni mkuu kuliko mfumbuaji.
10
Huyo ndiye aliyeandikiwa: Utaniona mimi, nikimtuma mjumbe wangu, akutangulie, aitengeneze njia yako mbele yako.*
11
Kweli nawaambiani: Miongoni mwao wote walizaliwa na wanawake hajaonekana aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji. Lakini aliye mdogo katika ufalme wa mbingu ni mkuu kuliko yeye.
12
Tangu siku za Yohana Mbatizaji mpaka leo ufalme wa mbingu huendewa kwa nguvu, nao wenye nguvu lhuupoka.
13
Kwani Wafuambuaji wote nayo Maonyo waliufumbua, mpaka Yohana akitokea.
14
Tena kama mnataka kuitikia: Yeye ndiye Elia atakayekuja.
15
Mwenye masikio yanayosikia na asikie!
16
*Lakini wao wa kizazi hiki niwafananishe na nini? Wamefanana na watoto wanaokaa sokoni na kuwaita wenzi wao wakisema:
17
Tumewapigia filimbi, nanyi hamkucheza; tena tumewaombelezea, nanyi hamkulia.
18
Kwani Yohana alikuja, hakula, wala hakunywaakala, wakasema: Ana pepo.
19
Mwana wa mtu alikuja, akala, akanywa, wakasema: Tazameni mtu huyu mlaji na mnyuwaji wa mvinyo, mpenda watoza kodi na wakosaji! Lakini werevu hutokezwa na matendo yake kuwa wa kweli.
20
Ndipo Yesu alipoanza kuikaripia miji, yalimofanyika ya nguvu yake mengi, kwa maana haikujuta.
21
Akasema: Yatakupata, wewe Korasini! Yatakupata, wewe Beti-Saida! Kwani ya nguvu yaliyofanyika kwenu, kama yangalifanyika Tiro na Sidoni, wangalijuta kale na kujivika magunia na kujikalisha majivuni.
22
Lakini nawaambiani: Siku ya hukumu miji ya Tiro na Sidoni itapata machungu yaliyo madogo kuliko yenu.
23
Nawe Kapernaumu, hukupazwa mpaka mbinguni? Utatumbukia mpaka kuzimuni, kwani ya nguvu yaliyofanyika kwako, kama yangalifanyika Sodomu, ungalikuwako mpaka leo.
24
Lakini nawaambiani: Siku ile ya hukumu nchi ya Sodomu itapata machungu yaliyo madogo kuliko yako.*
25
*Siku zile Yesu akasema kwamba: Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwani hayo umewaficha werevu na watambuzi, ukawafunulia wachanga.
26
Ndio, Baba, kwani hivyo ndivyo, ulivyopendezwa navyo.
27
Vyote nimepewa na Baba yangu. Hakuna anayemtambua Mwana pasipo Baba; wala hakuna anayemtambua Baba pasipo mwana na kila, Mwana atakayemfunulia.
28
Njoni kwangu nyote, wenye kusumbuka na wenye kulemewa na mizigo! Mimi nitawatuliza.
29
Twaeni kata yangu, mjifunze kwangu! Kwani ndimi mpole na mnyenyekevu moyoni. Kwa hivyo mtaipatia mioyo yenu kituo;
30
kwani kata yangu ni njema, nao mzigo wangu ni mwepesi.*
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28