bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 20
Matthew 20
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 21 →
1
*Ufalme wa mbingu umefanana na mtu mwenye numba aliyetoka mapema kutafuta wakulima, wamlimie mizabibu yake.
2
Alipokwisha patana na wakulima mchana kutwa kwa shilingi akawatuma katika mizabibu yake.
3
Ilipopata saa tatu, akatoka, akaona wengine waliosimama sokoni pasipo kazi.
4
Nao akawaambia: Nendeni nanyi katika mizabibu! Nami kinachowapasa nitawapani.
5
Basi, wakaenda. Ilipopata saa sita na saa kenda, akatoka tena, akafanya vilevile.
6
Hata ilipopata saa kumi na moja, akatoka, akaona wengine waliosimama, akawaambia: Mnasimamaje hapa mchana kutwa pasipo kazi?
7
Wakamwambia: Kwa sababu hakuna mtu aliyetuita kazini. Akawaambia: Nendeni nanyi katika mizabibu!
8
Basi ilipokuwa jioni, mwenye mizabibu akamwambia msimamizi wake: Waite wakulima, uwape mshahara wao, uanzie wa mwisho, uishilizie wa kwanza!
9
Wakaja wa saa kumi na moja, wakapokea kila mtu shilingi.
10
Walipokuja wa kwanza wakadhani, ya kuwa watapokea zaidi. Lakini nao wakapokea kila mtu shilingi.
11
Walipoipokea wakamnung'unikia mwenye nyumba
12
wakisema: Hawa wa mwisho wamefanya kazi saa moja tu, nawe umewalinganisha na sisi tuliosumbuka kwa kazi na kwa jua kali mchana kutwa.
13
Naye akamjibu mmoja wao akisema: Mwenzangu, sikukupunja, hukupatana nami kwa shilingi?
14
Chukua iliyo yako, ujiendee! Huyu wa mwisho nataka kumpa kama wewe.
15
Kumbe sina ruhusa ya kufanya na mali yangu mwenyewe, kama nitakavyo? Au jicho lako linakuwa baya, kwa sababu mimi ni mwema?
16
Hivyo ndivyo, walio wa mwisho watakavyokuwa wa kwanza, nao walio wa kwanza watakuwa wa mwisho. Kwani waalikwao ni wengi, lakini wachaguliwao ni wachache tu.*
17
Yesu alipotaka kupanda kwenda Yerusalemu akawachukua wale kumi na wawili, wawe peke yao. Akawaambia njiani:
18
Tazameni tunapanda kwenda Yerusalemu. Huko Mwana wa mtu atatiwa mikononi mwao watambikaji wakuu na waandishi, nao watamhukumu, auawe;
19
kwa hiyo watamtia mikononi mwa wamizimu, wapate kumfyoza na kumpiga viboko na kumwamba msalabani. Naye siku ya tatu atafufuliwa.
20
Ndipo, alipomjia mama yao wana wa Zebedeo pamoja na wanawe, akamwangukia na kumwomba kitu.
21
Alipomwuliza: Wataka nini? akamwambia: Sema, hawa wanangu wawili wakae katika ufalme wako mmoja kuumeni, mmoja kushotoni kwako!
22
Yesu akajibu akisema: Hamjui mnaloliomba. Mwaweza kukinywa kinyweo, nitakachokinywa mimi? Walipomwambia: Twaweza,
23
akawaambia: Kinyweo changu mtakinywa, lakini kumketisha mtu kuumeni na kushotoni kwangu hii si kazi yangu, ila hupewa walioandaliwa na Baba yangu.
24
Wenzao kumi walipoyasikia wakawakasirikia hao ndugu wawili.
25
Lakini Yesu akawaita, wamjongelee, akasema: Mnajua: wafalme wa mataifa huwatawala, nao wakubwa huwatumikisha kwa nguvu.
26
Kwenu ninyi visiwe hivyo ila mtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu sharti awe mtumishi wenu!
27
Naye anayetaka kuwa wa kwanza kwenu sharti awe mtumwa wenu!
28
Kama Mwana wa mtu asivyokuja, atumikiwe, ila amekuja kutumika na kuitoa roho yake kuwa makombozi ya watu wengi.
29
Walipokuwa wakotoka Yeriko, likamfuata kundi la watu wengi.
30
Ndipo, vipofu wawili waliokaa njani kando waliposikia, ya kuwa ni Yesu anayepita, wakapaza sauti wakisema: Bwana, mwana wa Dawidi, tuhurumie!
31
Lakini watu wakawakaripia, wanyamaze. Lakini wao wakazidi kupaza sauti wakisema: Bwana, mwana wa Dawidi, tuhurumie!
32
Ndipo, Yesu aliposimama, akawaita, akasema: Mwataka, niwafanyie nini?
33
Wakamwambia: Bwana, twataka, macho yetu yafumbuke!
34
Yesu akawaonea uchungu, akawagusa macho yao. Mara wakapata kuona, wakamfuata.
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 21 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28