bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 9
Matthew 9
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 10 →
1
*Akaingia chomboni, akavuka, akafika mjini mwake yeye.
2
Papo hapo wakamletea mgonjwa wa kupooza aliyelala kitandani. Yesu alipoona, walivyomtegemea, akamwambia mwenye kupooza: Tulia, mwanangu! Makosa yako yameondolea.
3
Ndipo, waandishi waliokuwako waliposema mioyoni: Huyu anambeza Mungu.
4
Kwa kuyajua hayo mawazo yao Yesu akasema: Mbona mnawaza mabaya mioyoni mwenu?
5
Kwani kilicho chepesi ni kipi? kusema: Makosa yako yameondolewa! au kusema: Inuka, uende?
6
Lakini kusudi mpate kujua, ya kuwa Mwana wa mtu ana nguvu ya kuondoa makosa nchini, - basi, akamwambia mwenye kupooza: Inuka, jitwishe kitanda chako, uende nyumbani kwako!
7
Ndipo, alipoinuka akaenda nyumbani kwake.
8
Lakini makundi ya watu walipoyaona wakaogopa, wakamtukuza Mungu aliyewapa watu nguvu kama hizo.*
9
*Yesu alipotoka huko, aende zake, akaona mtu anayeitwa Mateo, amekaa forodhani. Akamwambia: Nifuata! Akainuka, akamfuata.
10
Ikawa, alipokaa chakulani nyumbani mwake, ndipo, walipokuja watoza kodi na wakosaji wengi, wakakaa chakulani pamoja na Yesu na wanafunzi wake.
11
Mafariseo walipowaona wakawaambia wanafunzi wake: Kwa nini mfunzi wenu anakula pamoja na watoza kodi na wakosaji?
12
Yesu alipoyasikia akasema: walio wazima hawapaswi na mganga, ila walio wagonjwa.
13
Lakini nendeni zenu, mkajifunze maana ya neno hili: Huruma ndizo, nizitakazo, lakini vipaji vya tambiko sivyo. Kwani sikujia kuwaita wongofu, ila wakosaji.*
14
Ndipo, walipomjia wanafunzi wa Yohana wakisema: Kwa nini sisi na Mafariseo hufunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?
15
Yesu akawaambia: Walioalikwa arusini hawawezi kusikitika hapo, bwana arusi akingali pamoja nao. Lakini siku zitakuja, watakapoondolewa bwana arusi; ndipo, watakapofunga. Hakuna mtu anayetia kiraka cha nguo mpya katika kanzu chakavu,
16
kwani kinaondoa pote paliposhonwa katika kanzu, hivyo tundu lake litakuwa kubwa zaidi.
17
Wala watu hawatii mvinyo mpya katika viriba vichakavu; kwani wakiitia mle, viriba vitapasuka, mvinyo imwagike, navyo viriba vitaangamia. Ila hutia mvinyo mpya katika viriba vipya; hivyo vyote viwili vitakaa.
18
*Alipokuwa akiwaambia haya, mara akaja jumbe, akamwangukia akisema: Binti yangu amekufa sasa hivi; lakini uje umbandikie mkono wako! mdipo atakapokuwa mzima tena.
19
Yesu akaondoka, akafuatana naye pamoja na wanafunzi wake.
20
Mara akaja mwanamke mwenye kutoka damu miaka 12, akamjia nyuma, akaligusa pindo la nguo yake,
21
maana alisema moyoni: Hata nikiigusa nguo yake tu nitapona.
22
Lakini Yesu akageuka, akamwona, akasema: Tulia, mwanangu! Kunitegemea kwako kumekuponya. Yule mwanamke akapona saa ileile.
23
Yesu alipoingia nyumbani mwa jumbe akawaona wapiga filimbi na kundi la watu, wakiomboleza,
24
akasema: Ondokeni! Kwani kijana hakufa, ila amelala usingizi tu; ndipo, walipomcheka sana.
25
Lakini wale watu walipokwisha fukuzwa, akaingia, akamshika mkono wake; ndipo, yule kijana alipoinuka.
26
Habari hizi zikatoka, zikaenea katika nchi ile yote.*
27
Yesu alipotoka huko, aende zake, wakamfuata vipofu wawili, wakapaza sauti za kuita: Tuhurumie, mwana wa Dawidi!
28
Alipoingia nyumbani, wale vipofu wakamjia. Yesu akawauliza: Mwanitegemea kwamba: Naweza kufanya hivyo? Wakamwambia: Ndio, Bwana.
29
Ndipo, alipowagusa macho akisema: Hayo, mliyoyategemea, na myapate vivyo hivyo!
30
Ndipo, macho yao yalipofumbuka. Kisha Yesu akawakemea akisema: Angalieni, mtu hata mmoja asiyasikie haya!
31
Lakini wale walipotoka wakamsimulia po pote katika nchi ile yote.
32
Hao walipotoka, mara wakamletea bubu aliyepagawa na pepo. Naye pepo alipokwisha fukuzwa, yule bubu akaweza kusema.
33
Makundi ya watu wakastaajabu wakisema: Tangu zamani havijaonekana katika Isiraeli vilivyo kama hivi.
34
Lakini Mafariseo wakasema: Nguvu ya mkuu wa pepo ndiyo, huyu anayofukuzia pepo.
35
*Yesu akawa akizunguka mijini mote na vijijini, akawafundisha katika nyumba zao za kuombea, akautangaza Utume mwema wa ufalme, akaponya ugonjwa wote na unyonge wote.
36
Lakini alipowatazama makundi ya watu akawaonea uchungu, kwani walikuwa wamechoka kwa kuteswa na kutawanyishwa kama kondoo wasio na mchungaji.
37
Ndipo, alipowaambia wanafunzi wake: Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache.
38
Mwombeni mwenye mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake!*
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 10 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28