bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 21
Matthew 21
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 22 →
1
Hapo, walipoukaribia Yerusalemu na kufika Beti-Fage mlimani pa michekele, ndipo, Yesu alipotuma wanafunzi wawili,
2
akawaambia: Nendeni katika kijiji kinachowaelekea! Mara mtaona punda, amefungwa, hata mtoto wake yuko pamoja naye; mfungueni, mniletee!
3
Kama mtu atawaambia neno, mwambieni: Bwana wetu anamtakia kazi! mara atawapani.
4
Haya yote yamekuwapo, lipate kutimizwa neno la mfumbuaji la kwamba:
5
Mwambieni binti Sioni: Tazama, mfalme wako anakujia, ni mpoke, amepanda mwana punda aliye na mama yake, mwenye kuchukua mizigo.
6
Wanafunzi wakaenda, wakafanya, kama Yesu alivyowaagiza.
7
Wakamleta punda na mwanawe, wakatandika nguo juu yao, kisha wakampandisha.
8
Nayo makundi ya watu wengi sana wakatandika nguo zao njiani, wengine wakakata matawi ya miti, wakayatandika njiani,
9
nao wale watu wengi waliomtangulia, nao waliomfuata wakapaza sauti wakisema: Hosiana, mwana wa Dawidi! Na atukuzwe ajaye kwa Jina la Bwana! Hosiana juu mbinguni!*
10
Alipoingia Yerusalemu, mji wote ukatukutika, wakisema: Nani huyu?
11
Makundi ya watu wakasema: Huyu ndiye mfumbuaji Yesu wa Nasareti wa Galilea.
12
Yesu akapaingia Patakatifu, akawafukuza wote wenye kuuzia na kununulia hapo Patakatifu, akaziangusha meza za wavunja fedha na viti vya wachuuzi wa njiwa,
13
akawaambia: Imeandikwa: Nyumba yangu itaitwa nyumba ya kuombea, lakini ninyi mnaigeuza kuwa pango la wanyang'anyi.
14
Kisha wakamwendea hapo Patakatifu vipofu na viwete, naye akawaponya.
15
Lakini watambikaji wakuu na waandishi walipoyaona mataajabu, aliyoyafanya, tena waliposikia, watoto wakipaza sauti hapo Patakatifu na kusema: Hosiana, mwana wa Dawidi! ndipo, walipokasirika,
16
wakamwambia: Unasikia, hawa wanavyosema? Yesu akawaambia: Ndio. Hamjalisoma bado neno lile la kwamba: Vinywani mwao watoto wachanga namo mwao wanyonyao ulitengeneza tukuzo?
17
Kisha akawaacha, akatoka mjini, akaenda Betania, akalala huko.
18
Asubuhi alipokuwa akirudi mjini akaona njaa.
19
Alipoona mkuyu kando ya njia akauendea, asione kitu kwake, ila majani matupu, akauambia: Kale na kale lisipatikane tena tunda kwako! Mara mkuyu ukawa umenyauka.
20
Wanafunzi walipoviona wakastaajabu, wakasema: Mkuyu huu umenyaukaje mara?
21
Yesu akajibu akiwaambia: Kweli nawaambiani: Mkimtegemea Mungu pasipo mashaka hamtafanya kama hili tu la huu mkuyu, ila hata mkiuambia mlima huu: Ondoka hapa, ulipo, ujitupe baharini! basi itatendeka.
22
Nayo yo yote, mtakayoyaomba katika maombo, mtayapata mkiwa mnamtegemea Mungu.
23
Alipokwisha ingia Patakatifu, akiwa akifundisha, wakamjia watambikaji wakuu na wazee wa huku kwao, wakamwuliza: Hayo unayafanya kwa nguvu gani?
24
Tena ni nani aliyekupa nguvu hii? Yesu akajibu akiwaambia: Hata mimi nitawauliza neno moja; mtakaponijibu neno hilo, basi, hata mimi nitawaelezea nguvu yangu ya kuyafanya hayo.
25
Ubatizo wake Yohana ulikuwa umetoka wapi? Mbinguni au kwa watu? Nao wakafikiri mioyoni mwao kwamba: Tukisema: Ulitoka mbinguni, atatuuliza: Mbona hamkumtegemea?
26
Lakini tukisema: Ulitoka kwa watu, tunawaogopa watu; kwani wote wanamshika Yohana kuwa mfumbuaji.
27
Kwa hiyo wakamjibu Yesu wakisema: Hatujui. Ndipo, alipowaambia: Basi, hata mimi siwaambii nguvu inayonifanyisha hayo.
28
*Lakini mwaonaje? Kulikuwa na mtu mwenye wana wawili. Akamwendea mkubwa, akasema: Mwanangu, nenda leo kufanya kazi mizabibuni!
29
Akamjibu, akasema: Sitaki; lakini halafu alijuta akaenda.
30
Alipomwendea wa pili na kumwambia yaleyale, yeye akajibu akisema: Ndio, bwana; lakini hakuenda.
31
Katika hao wawili aliyeyafanya, baba aliyoyataka, ni yupi? Wakasema: Ni wa kwanza. Yesu akawaambia: Kweli nawaambiani: Watoza kodi na wenye ugoni watawatangulia ninyi kuingia katika ufalme wa Mungu.
32
Kwani Yohana alikuja kwenu, akafuata njia yenye wongofu, nanyi hamkumtegemea, lakini watoza kodi na wenye ugoni walimtegemea. Lakini ninyi mlipoviona, hata hapo hamkujuta na kumtegemea.*
33
Sikilizeni mfano mwingine! Kulikuwa na mtu mwenye nyumba aliyepanda mizabibu, akaizungusha ugo, akachimbua humo kamulio la kuzikamulia zabibu, akajenga dungu, akaipangisha wakulima, kisha akaenda katika nchi nyingine.
34
Siku za kuiva zabibu zilipotimia, akatuma watumwa wake kwa wale wakulima, wapewe zabibu zake.
35
Nao wakulima wakawakamata watumwa wake, mmoja wakampiga, mmoja wakamwua, mmoja wakamtupia mawe.
36
Akatuma tena watumwa wengine walio wengi kuliko wa kwanza. Wakawatendea vilevile.
37
Mwisho akamtuma mwanawe kwao akisema: Watamcha mwanangu.
38
Lakini wakulima walipomwona mwanawe wakasemezana wao kwa wao: Huyu ndiye kibwana, njoni, tumwue, tuupate urithi wake!
39
Kwa kiyo wakamkamata, wakamsukuma sukuma mpaka nje ya mizabibu, wakamwua.
40
Basi, mwenye mizabibu atakapokuja wakulima wale atawafanyia nini?
41
Wakamwambia: Hao wabaya atawaangamiza vibaya, nayo mizabibu atawapangisha wakulima wengine watakaompa zabibu zake, zitakapoiva.
42
*Yesu akawaambia: Hamjasoma katika Maandiko ya kuwa: Jiwe, walilolikataa waashi, hilihili limekuwa la pembeni? Hivyo vimefanywa na Bwana; nasi tukivitazama, ni vya kustaajabu.
43
Kwa sababu hiyo nawaambiani: Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu taifa jingine litakalozaa matunda yake liupate.
44
Naye atakayeanguka juu ya jiwe hilo atapondeka, naye litakayemwangukia, litambana tikitiki*.
45
Watambiakaji wakuu na Mafariseo walipoisikia mifano yake wakatambua, ya kuwa anawasema wao.
46
Kwa hiyo wakatafuta kumkamata, lakini waliwaogopa makundi ya watu, kwani walimwona kuwa mfumbuaji.
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 22 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28