bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 16
Matthew 16
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 17 →
1
Wakaja Mafariseo na Masadukeo, wakamjaribu wakitaka, awaonyeshe kielekezo kitokacho mbinguni.
2
Naye akajibu akiwaambia: Kukichwa mnasema: Kutakucha na kianga, kwani mbingu ni nyekundu.
3
Tena kukicha mnasema: Leo itakunya mvua, kwani mbingu ni nyekundu, tena kumetanda mawinguwingu. Enyi wajanja! Mnayoyaona ya mbinguni, mnajua kuyatambua, lakini vielekezo vya siku hizi vinawashindani?
4
Wao wa ukoo huu mbaya wenye ugoni wanataka kielekezo, lakini hawatapata kielekezo, ila kielekezo cha mfumbuaji Yona. Kisha akawaacha, akaenda zake.*
5
Wanafunzi walipofika ng'ambo walikuwa wamesahau kuchukua mikate.
6
Yesu akawaambia: Tazameni, jilindeni kwa ajili ya chachu yao Mafariseo na Msadukeo!
7
Ndipo, walipoyafikiri na kusemeza wao kwa wao: Ni kwa sababu hatukuchukua mikate;
8
Lakini Yesu akawatambua, akawaambia: Enyi mnaonitegemea kidogo tu, mbona mnafikiri hivyo mioyoni mwenu ya kuwa hamnayo mikate?
9
Hamjaerevuka bado? Wala hamwikumbuki mikate ile mitano ya wale 5000 na makapu, mliyoyachukua, kama ni mangapi?
10
Wala hamwikumbuki ile mikate saba ya wale 4000 na makanda, mliyoyachukua, kama ni mangapi?
11
Kwa sababu gani hamtambui, ya kuwa sikuwaambia kwa ajili ya mikate niliposema: Jilindeni kwa ajili ya chachu yao Mafariseo na Masadukeo?
12
Ndipo, walipotambua, ya kuwa hakusema, wajilinde kwa ajili ya chachu ya mikate, ila wajilinde kwa ajili ya ufundisho wao Mafariseo na Masadukeo.
13
Yesu akaenda pande za mji wa Kesaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akisema: Watu humsema Mwana wa mtu kuwa ni nani?
14
Nao wakajibu: Wengine husema kuwa u Yohana Mbatizaji, wengine: Elia, wengine: Yeremia au mmoja wao wafumbuaji.
15
Yesu akawauliza: Lakini ninyi mnanisema kuwa ni nani?
16
Simoni Petero akajibu akisema wewe ndiwe Kristo, Mwana wake Mungu Mwenye uzima.
17
Yesu akajibu akimwambia: U mwenye shangwe, Simoni wa Yona, kwani mwenye mwili na damu hakukufunulia hili, ila Baba yangu alioko mbinguni.
18
Nami nakuambia: Wewe ndiwe Petero, juu ya mwamba huu nitalijenga kundi la wateule wangu, nayo malango ya kuzimu hayatawashinda.
19
Nitakupa funguo za ufalme wa mbingu: lo lote, utakalolifunga nchini, litakuwa limefungwa hata mbinguni; nalo lo lote, utakalolifungua nchini, litakuwa limefunguliwa hata mbinguni.
20
Ndipo, alipowatisha wanafunzi, wasimwambie mtu ya kuwa yeye ndiye Kristo.
21
*Tokea hapo Yesu Kristo akaanza kuwaonyesha wanafunzi wake, ya kuwa imempasa kwenda Yerusalemu ateswe mengi nao wazee na watambikaji wakuu na waandishi, mpaka auawe, kisha afufuliwe siku ya tatu.
22
Ndipo, Petero alipomchukua pembeni, akaanza kumtisha akisema: Jionee uchungu, wewe Bwana, haya yasikupate!
23
Naye akageuka, akamwambia Petero: Niondokea hapa nyuma yangu, wewe Satani! Wewe wataka kunikwaza, kwani wewe huyawazi mambo ya Kimungu, ila unayawaza ya kiwatu tu.
24
Ndipo, Yesu alipowaambia wanafunzi wake: Mtu akitaka kunifuata mimi ajikataze mapenzi yake, ajitwishe nao msalaba wake, kisha anifuate!
25
Maana mtu anayetaka kuikoa roho yake ataiangamiza. Lakini mtu atakayeiangamiza roho yake kwa ajili yangu mimi ataiponya.
26
Kwani mtu vitamfaa nini, hata avichume vya ulimwengu wote, roho yake ikiponwa navyo? Au mtu atatoa nini, aikomboe roho yake?*
27
Kwani Mwana wa mtu atakapokuja mwenye utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake, ndipo, atakapomlipa kila mtu, kama matendo yake yalivyo.
28
Kweli nawaambiani: Miongoni mwao wanaosimama hapa wamo wengine, ambao hawatakuonja kufa, mpaka watakapomwona Mwana wa mtu, akija mwenye ufalme wake.
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 17 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28