bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 25
Matthew 25
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 24
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 26 →
1
*Hapo ufalme wa mbingu utafanana na wanawali kumi walioshika taa zao, wakatoka kwenda kumpokea bwana arusi.
2
Watano wao walikuwa wajinga, wenzao watano walikuwa werevu.
3
Kwani wale wajinga walizishika taa zao tu, wasichukue na mafuta.
4
Lakini wale werevu walichukua mafuta katika vichupa pamoja na taa zao.
5
Bwana arusi alipokawia, wakasinzia wote, wakalala usingizi.
6
Kati ya usiku pakawa na kelele: Tazameni, bwana arusi huyo! Tokeni, mmpokee!
7
Ndipo, wanawali wale wote walipoinuka, wakazitengeneza taa zao.
8
Lakini wajinga wakawaambia wenzao werevu: Tugawieni mafuta yenu! kwani taa zetu zinazimika.
9
Lakini wale werevcu wakajibu wakisema: Sivyo, hayatatutosha sisi na ninyi; sharti mwende kwa wachuuzi, mjinunulie wenyewe!
10
Walipokwenda kununua, bwana arusi akafika, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini, kisha mlango ukafungwa.
11
Halafu wakaja nao wanawali wale wengine wakasema: Bwana, Bwana, tufungulie!
12
Lakini akajibu akisema: Kweli nawaambiani: Siwajui ninyi.
13
Kwa hiyo kesheni! Kwani hamwijui siku wala saa, Mwana wa mtu atakapojia.*
14
Kwani vinafanana na mtu aliyefunga safari, akawaita watumwa wake mwenyewe, akawapa mali zake kuzitunza.
15
Akampa kila mtu fungu, aliwezalo mwenyewe kulitunza, mmoja fedha elfu tano, mmoja elfu mbili, mmoja elfu moja, kisha akaenda zake.
16
Yule aliyepokea elfu tano akaenda, akazichuuzia, akachuma nazo nyingine elfu tano.
17
Vile vile na yule aliyepokea elfu mbili, naye akachuma nazo nyingine elfu mbili.
18
Lakini yule aliyepokea elfu moja akaenda, akachimba shimo, akazifukia mle fedha za bwana wake.
19
Siku zilipopita nyingi, akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao.
20
Akaja yule aliyepokea elfu tano, akaleta elfu tano nyingine akasema: Bwana, umenipa elfu tano; tazama, nimechuma elfu tano nyingine.
21
Bwana wake akamwambia: Vema, wewe mtumwa mwema na mwelekevu, ulikuwa mwelekevu wa machache, nitakupa kutunza mengi. Ingia penye furaha ya bwana wako!
22
Akaja na yule aliyepokea elfu mbili, akasema: Bwana, umenipa elfu mbili. Tazama, nimechuma elfu mbili nyingine.
23
Bwana wake akamwambia: Vema, wewe mtumwa mwema na mwelekevu, ulikuwa mwelekevu wa machache, nitakupa kutunza mengi. Ingia penye furaha ya bwana wako!
24
Akaja na yule aliyekuwa amepokea elfu moja, akasema: Bwana, nalitambua, ya kuwa wewe u mkorofi; huvuna, usipopanda, hukusanya, usipotandaza.
25
Nikaogopa, nikaenda, nikazifukia fedha zako shimoni. Tazama, hizi mali zako, uzichukue!
26
Lakini bwana wake akajibu akimwambia: Mtumwa mbaya wewe! U mvivu! Ulinijua, ya kuwa navuna, nisipopanda, nakusanya nisipotandaza?
27
Basi, ilikupasa kuziweka fedha zangu kwao wenye maduka, nami nilipokuja ningalizichukua zilizo zangu pamoja na faida.
28
Kwa hiyo ichukueni elfu yake ya fedha, mmpe mwenye elfu kumi!
29
Kwani kila mwenye mali atapewa, ziwe nyingi zaidi; lakini asiye na kitu atachukuliwa hata kile, alicho nacho.
30
Lakini huyu mtumwa asiyefaa mtupeni penye giza lililoko nje! Ndiko, kitakakokuwa kilio na kukereza meno.
31
*Hapo, atakapokuja Mwana wa mtu mwenye utukufu wake na malaika wote pamoja naye, ndipo, atakapokalia kiti cha utukufu wake,
32
nayo mataifa yote yatakusanywa mbele yake; naye atawabagua, kama mchungaji anavyowabagua kondoo na mbuzi.
33
Atawaweka kondoo kuumeni kwake, nao mbuzi kushotoni.
34
Hapo mfalme atawaambia walioko kuumeni kwake: Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme, mliotengenezewa tangu hapo, ulimwengu ulipoumbwa!
35
Kwani nilipokuwa na njaa, mlinipa chakula; nilipokuwana kiu, mlininywesha; nilipokuwa mgeni, mlinipokea;
36
nilipokuwa uchi, mlinivika; nilipokuwa mgonjwa, mlinikagua; nilipokuwa kifungoni mlinijia.
37
Ndipo wale waongofu watakapomjibu: Bwana, ni lini, tulipokuona na njaa, tukakulisha? Au tulipokuona na kiu, tukakunywesha?
38
Tena ni lini, tulipokuona mgeni, tukakupokea? Au tulipokuona uchi, tukakuvika?
39
Ni lini tena, tulipokuona mgonjwa au kifungoni, tukakujia?
40
Naye mfalme atawajibu akisema: Kweli nawaambiani: Yote, mliyomtendea mwenzao mmoja wa hawa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi.
41
Kisha atawaambia walioko kushotoni: Ondokeni kwangu, mlioapizwa, mwingie kwenye moto usiozimika, uliowashiwa Satani na malaika zake!
42
Kwani nilipokuwa na njaa, hamkunipa chakula; nilipokuwa na kiu, hamkuninywesha;
43
nilipokuwa mgeni, hamkunipokea; nilipokuwa uchi, hamkunivika; nilipokuwa mgonjwa na kifungoni, hamkuja kunikagua.
44
Ndipo, nao wale watakapojibu wakisema: Bwana, ni lini, tulipokuona na njaa au na kiu au mgeni au mwenye uchi au mgonjwa au kifungoni, tusikutumikie?
45
Hapo atawajibu akisema: Kweli nawaambiani: Yote, msiyomtendea mwenzao mmoja tu wa hawa ndugu zangu wadogo, basi hamkunitendea hata mimi.
46
Kisha hawa watakwenda kuingia penye maumivu ya kale na kale. Lakini wale waongofu watakwenda kuingia penye uzima wa kale na kale.*
← Chapter 24
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 26 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28