bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 2
Matthew 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 3 →
1
Yesu alipokwisha kuzaliwa Bet-Lehemu wa Uyuda wakati wa mfalme Herode, ndipo, walipofika Yerusalemu wachunguza nyota waliotoka upande wa maawioni kwa jua.
2
Wakasema: Yuko wapi aliyezaliwa kuwa mfalme wa Wayuda? Kwani tumeiona nyota yake katika nchi ya maawioni kwa jua, basi, tumekuja kumwangukia.
3
Mfalme Herode alipoyasikia haya akahangaika, nao Yerusalemu wote pamoja naye.
4
Akawakusanya wote waliokuwa watambikaji wakuu na waandishi wa kwao akapeleleza kwao mahali, Kristo atakapozaliwa.
5
Nao wakamwambia: Atazaliwa Beti-Lehemu wa Uyuda, kwani ndivyo, alivyoandika mfumbuaji:
6
Nawe Beti-Lehemu wa nchi ya Yuda, hu mdogo kamwe katika majumbe ya Yuda. Kwani mwako ndimo, atakamotoka mtawala atakayewachunga walio ukoo wangu wa Isiraeli.
7
Kisha Herode akawaita wale wachunguza nyota na kufichaficha, akazidi kuwauliza vema siku, ile nyota ilipooneka.
8
Akawatuma Beti-Lehemu akisema: Nendeni, mkapeleleze sana habari za mtoto huyo! Mtakapomwona mnipashe habari, nami nipate kwenda nimwangukie.
9
Nao walipokwisha msikia mfalme wakashika njia. Walipotazama, ile nyota, waliyoiona maawioni kwa jua, ikawatangulia, mpaka ikaja kusimama juu sawa ya mle alimokuwa yule mtoto.
10
Walipoiona hiyo nyota wakafurahi furaha kubwa mno.
11
Wakaingia nyumbani mle, wakamwona mtoto pamoja na mama yake Maria, wakamwangukia na kumnyenyekea. Walipokwisha wakayafungua malimbiko yao, wakamtolea mtoto tunu, dhahabu na uvumba na manemane.
12
Nao walipoonywa kwa ndoto, wasimrudie Herode, wakashika njia nyingine, wakaenda kwao.*
13
Hao walipokwisha kwenda zao, malaika wa Bwana akamtokea Yosefu katika ndoto akisema: Inuka, mchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukakae huko, mpaka nitakapokuambia! Kwani Herode atamtafuta mtoto, amwangamize.
14
Kisha akainuka, akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda Misri.
15
Akakaa huko, mpaka Herode alipokwisha kufa, lipata kutimia neno, Bwana alilolisema kwa mfumbuaji: Misri ndiko, nilikomwitia mwanangu.
16
Herode alipoona, ya kuwa wale wachunguza nyota wamemdanganya akakasirika sana, akatuma watu, wawaue watoto waume wote waliokuwako Beti-Lehemu na vilimani pake pote, waliokuwa wa miaka miwili nao waliopungua, kama alivyoipeleleza siku kwao wachunguza nyota.
17
Ndipo, lilipotimia lililosemwa na mfumbuaji Yeremia kwamba:
18
Sauti imesikiwa Rama, ni kilio na maombolezo mengi. Raheli anawalilia watoto wake, hakutaka kubembelezwa, kwani hawako.
19
Herode alipokwisha kufa, mara malaika wa Bwana akamtokea Yosefu kwa ndoto huko Misri, akamwambia:
20
Inuka, umchukue mtoto na mama yake, uende katika nchi ya Isiraeli! Kwani wamekwisha kufa waliotafuta kumwua mtoto.
21
Ndipo, alipoinuka, akamchukua mtoto na mama yake, akaiingia nchi ya Isiraeli.
22
Lakini aliposikia, ya kuwa Arkelao ametawala Yudea mahali pa Herode, baba yake, akaogopa kwenda huko. Basi akaagizwa kwa ndoto, aende zake pande za Galilea;
23
kwa hiyo akaja, akakaa mji uitwao Nasareti, lipate kutimia lililosemwa na wafumbuaji: Ataitwa Mnasareti.*
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28