bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 22
Matthew 22
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 23 →
1
Yesu akaendelea kusema tena kwa mifano akiwaambia:
2
Ufalme wa mbingu umefanana na mtu mfalme aliyemfanyia mwanawe arusi.
3
Akawatuma watumwa wake, wawaite walioalikwa arusini; nao hawakutaka kuja.
4
Akatuma watumwa wengine akisema: Waambieni walioalikwa: Tazameni, nimekwisha kuiandaa karamu yangu, ng'ombe na vinono vimechinjwa, vyote viko tayari, njoni arusini!
5
Lakini wale wakavibeza, wakaenda zao, mmoja shambani kwake, mmoja kwa uchuuzi wake.
6
Nao waliosalia wakawakamata watumwa wake, wakawapiga, wakawaua.
7
Lakini mfalme akachafuka, akawatuma askari wake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao.
8
Hapo akawaambia watumwa wake: Arusi iko tayari, lakini walioalikwa hawakufaa.
9
Basi, nendeni, mfike kwenye njia panda mwalikie arusini wo wote, mtakaowaona!
10
Wale watumwa wakatoka, wakaenda njiani, wakawakusanya wote, waliowaona, wabaya na wema; arusi ikajaa wageni.
11
Lakini mfalme alipoingia kuwatazama wageni akaona mle mtu asiyevaa nguo inayopasa arusini.
12
Akamwambia: Mwenzangu, uliingiaje humo, nawe hukuvaa nguo inayopasa arusini? Yule akanyamaza kimya.
13
Ndipo, mfalme alipowaambia watumishi: Mfungeni miguu na mikono, mmtupe penye giza lililoko nje! ndiko, kitakakokuwa kilio na kukereza meno.
14
Kwani waalikwao ni wengi, lakini wachaguliwao ni wachache tu!*
15
Mafariseo wakaenda zao, wakala njama ya kumtega kwa maneno yake.
16
Wakatuma kwake wanafunzi wao pamoja na watu wa Herode, wakasema: Mfunzi, tumekujua, ya kuwa wewe ni mtu wa kweli, nayo njia ya Mungu unaifundisha, ilivyo kweli, tena humwuliziulizi mtu ye yote, kwani hutazami nyuso za watu.
17
Tuambie, unaonaje wewe? Iko ruhusa ya kumtolea Kaisari kodi au haiko?
18
Kwa kuutambua ubaya wao Yesu akasema: Enyi wajanja, mwanijaribiaje? Nionyesheni fedha ya kodi! Walipomletea shilingi,
19
akawauliza: Chapa hiki cha nani? Maandiko nayo ya nani?
20
Wakasema: Ni yake Kaisari.
21
Ndipo, alipowaambia: Basi, yaliyo yake Kaisari mtoleeni Kaisari, naye Mungu yaliyo yake Mungu!
22
Walipoyasikia wakastaajabu, wakamwacha, wakaenda zao.*
23
Siku ileile wakamjia Masadukeo wanaosema: Hakuna ufufuko, wakamwuliza
24
wakisema: Mfunzi, Mose alisema: Mtu akifa asipokuwa na wana, nduguye amwingilie mkewe, amzalie mkubwa wake mwana!
25
Kwetu kulikuwa na waume saba walio ndugu. Wa kwanza akaoa, akafa; kwa sababu hakuwa na mwana, alimwachia nduguye mkewe.
26
Vilevile na wa pili na wa tatu na wale saba wote.
27
Mwisho wao wote akafa naye mwanamke.
28
Basi, katika ufufuko atakuwa mke wa yupi wa hao saba? Kwani wote waliokuwa naye.
29
Yesu akajibu, akawaambia: Mwapotelewa, kwani hamyajui Maandiko wala nguvu ya Mungu.
30
Kwani katika ufufuko hawataoa, wala hawataolewa, ila watakuwa, kama malaika walivyo mbinguni.
31
Lakini kwa ajili ya ufufuko wa wafu hamkusoma, mliloambiwa na Mungu aliposema:
32
Mimi ni Mungu wa Aburahamu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo? Basi, Mungu siye wa wafu, ila wao walio hai.
33
Watu walipoyasikia wakastushwa kwa ufundisho wake.
34
*Mafariseo waliposikia, ya kuwa amewashinda Masafukeo na kuwafumba vinywa, wakakusanyika pamoja.
35
Mmoja wao aliyekuwa mjuzi wa Maonyo yake Mungu akamwuliza kwa kumjaribu akisema:
36
Mfunzi, agizo lililo kubwa katika Maonyo yake Mungu ni lipi?
37
Naye akamwambia: Umpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa mawazo yako yote!
38
Hili ndilo agizo lililo kubwa, tena ni la kwanza. Nalo la pili limefanana nalo,
39
ndilo hili: Umpende mwenzio, kama unavyojipenda mwenyewe!
40
Katika haya maagizo mawili yamo Maonyo yote ya Mungu pamoja na Wafumbuaji.
41
Wao Mafariseo walipokusanyika, Yesu akawauliza
42
akisema: Mwamwonaje Kristo kuwa ni mwana wa nani? Wakamwambia: Wa Dawidi.
43
Akawauliza: Tena Dawidi alimwitaje Bwana kwa nguvu ya Roho aliposema: Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti kuumeni kwangu,
44
mpaka niwaweke adui zako chini miguuni pako?
45
Basi Dawidi akimwita Bwana, anakuwaje mwana wake?
46
Hata mmoja hakuweza kumjibu neno, wala toka siku ile hakuwako mtu aliyejipa moyo wa kumwuliza neno tena.*
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 23 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28