bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 26
Matthew 26
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 25
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 27 →
1
Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo yote, akawaambia wanafunzi wake:
2
Mmejua, baada ya siku mbili itakuwa Pasaka; naye Mwana wa mtu atatolewa, awambwe msalabani.
3
Hapo watambikaji wakuu na wazee wa huko kwao wakakusanyika nyumbani mwa mtambikaji mkuu, jina lake Kayafa,
4
wakala njama ya kumkamata Yesu kwa werevu wapate kumwua.
5
Lakini walisema: Kwanza sikukuu ipite, watu wasije, wakafanya fujo!
6
Yesu alipokuwa Betania nyumbani mwa Simoni Mkoma,
7
akamjia mwanamke mwenye kichupa cheupe cha jiwe kilichojaa mafuta ya maua yaliyo yenye bei kubwa. Akammiminia kichwani pake, alipokaa akila.
8
Lakini wanafunzi walipoviona wakachukiwa, wakasema: Upotevu huu ni wa nini?
9
Kwani mafuta haya yangaliwezekana kuuzwa kwa fedha nyingi, wakapewa maskini.
10
Lakini Yesu alipovitambua, akawaambia: Mbona mnamsikitisha mwanamke huyu? Maana amenitendea tendo zuri.
11
Kwani maskini mnao kwenu siku zote, lakini mimi hamwi nami siku zote.
12
Kwani alipoyamimina mafuta haya, aupake mwili wangu, ameutengenezea kuzikwa.
13
Kweli nawaambiani: Po pote katika ulimwengu wote, patakapotangazwa Utume huu mwema, patasemwa nacho hiki, alichokitenda yeye, naye akumbukwe.
14
Hapo wale kumi na wawili mwenzao mmoja aliyeitwa Yuda Iskariota akaenda kwa watambikaji wakuu,
15
akasema: Mwataka kunipa nini, nitakapomtia mikononi mwenu? Wakaagana kumpa fedha 30.
16
Toka hapohapo alitafuta njia iliyofaa amtoe.
17
Siku ya kwanza ya kula mikate isiyotiwa chachu wanafunzi wakamjia Yesu wakisema: Unataka, tukuandalie wapi, uile kondoo ya Pasaka?
18
Naye akasema: Nendeni mjini kwa fulani, mmwambie: Mfunzi anasema: Siku zangu zinatimia! Kwako nitaila kondoo ya Pasaka pamoja na wanafunzi wangu.
19
Wanafunzi wakafanya, kama Yesu alivyowaagiza, wakaiandaa kondoo ya Pasaka.
20
Ilipokuwa jioni, akakaa chakulani pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili.
21
Walipokuwa wakila, akasema: Kweli nawaambiani: Mwenzenu mmoja atanichongea.
22
Wakasikitika sana, wakaanza kumwuliza kila mmoja: Bwana, ni mimi?
23
Naye akajibu akisema: Aliyetowelea pamoja nami bakulini ndiye atakayenichongea.
24
Mwana wa mtu anakwenda njia yake, kama alivyoandikiwa; lakini yule mtu, ambaye Mwana wa mtu atachongewa naye, atapatwa na mambo. Ingalimfalia yule mtu, kama asingalizaliwa.
25
Ndipo, Yuda aliyemchongea alipomwuliza akisema: Mfunzi mkuu, ni mimi? Akamjibu: Ndio umesema.
26
Walipokuwa wakila, Yesu akatwaa mkate, akauombea, akaumega, akawapa wanafunzi akisema: Twaeni, mle! Huu ndio mwili wangu.
27
Kisha akatwaa kinyweo, akashukuru, akawapa akisema: Nyweni nyote humu!
28
Maana hii ndiyo damu yangu ya Agano Jipya inayomwagwa kwa ajili ya wengi, wapate kuondolewa makosa.
29
Lakini nawaambiani: Tangu sasa sitayanywa tena mazao ya mizabibu mpaka siku ile, nitakapoyanywa mapya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.
30
Walipokwisha kuimba wakatoka kwenda mlimani pa michekele.
31
Hapo Yesu akawaambia: Usiku huu wa leo ninyi nyote mtajikwaa kwangu kwani imeandikwa:
32
Nitampiga mchungaji, kondoo wa kundi lake watawanyike; lakini nitakapokwisha kufufuliwa nitawatangulia kwenda Galilea.
33
Ndipo, Petero alipojibu akimwambia: Ijapo wote wajikwae kwako, lakini mimi sitajikwaa kamwe.
34
Yesu akamwambia: Kweli nakuambia: Usiku huu wa leo jogoo atakapokuwa hajawika, utakuwa umenikana mara tatu.
35
Petero akamwambia: Hata ijaponipasa kufa pamoja nawe, sitakukana kabisa. Nao wanafunzi wote wakasema vivyo hivyo.
36
Kisha Yesu akaenda pamoja nao mahali panapoitwa Getisemane. Akawaambia wanafunzi: Kaeni hapa, niende kule, niombe!
37
Akamchukua Petero na wale wana wawili na Zebedeo, akaanza kusikitika na kuhangaika,
38
akawaambia: Roho yangu inaumizwa sana na masikitiko, imesalia kufa tu. Kaeni papa hapa, mkeshe pamoja nami!
39
Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akaomba akisema: Baba, ikiwezekana kinyweo hiki kinipite, nisikinyuwe! Lakini yasifanyike, kama nitakavyo mimi, ila yafanyike kama utakavyo wewe!
40
Alipowajia wanafunzi, akawakuta, wamelala usingizi, akamwambia Petero: Hamkuweza kukesha pamoja nami saa moja tu?
41
Kesheni na kuomba, msije kuingia majaribuni! Roho inataka kuitikia, lakini mwili ni mnyonge.
42
Akaenda tena mara ya pili, akaomba akisema: Baba, isipowezekana, hiki kinipite, nisikinywe, basi, uyatakayo wewe na yafanyike!
43
Alipokuja tena, akawakuta, wamelala usingizi, kwani macho yao yalikuwa mazito.
44
Akawaacha, akaenda tena, akaomba mara ya tatu akisema tena maneno yale yale.
45
Kisha akawajia wanafunzi, akawaambia: Mwafuliza kulala usingizi, uchovu uwatoke? Tazameni, saa iko karibu, Mwana wa mtu atiwe mikononi mwa wakosaji!
46
Inukeni, twende! Tazameni, mwenye kunichongea yuko karibu!
47
Angali akisema, mara akaja Yuda, mmoja wao wale kumi na wawili, pamoja na watu wengi sana wenye panga na rungu waliotoka kwa watambikaji wakuu na kwa wazee wa huko kwao.
48
Lakini mwenye kumchongea alikuwa amewapa kielekezo akisema: Nitakayemnonea ndiye, mkamateni!
49
Mara akamjia Yesu, akasema: Salamu, mfunzi mkuu! Akamnonea.
50
Yesu akamwambia: Mwenangu, umejia nini? Ndipo, walipokuja, wakamkamata Yesu kwa mikono yao, wakamfunga.
51
Papo hapo wale waliokuwako pamoja na Yesu mmoja wao akanyosha mkono, akauchomoa upanga wake, akampiga mtumwa wa mtambikaji mkuu, akamkata sikio.
52
Ndipo, Yesu alipomwambia: Urudishe upanga wako mahali pake! kwani wote wenye kushika panga wataangamizwa kwa upanga.
53
Au unadhani: Siwezi kumbembeleza Baba yangu, naye akaniletea sasa hivi malaika wengi kupita elfu kumi na mbili?
54
Lakini Maandiko yangetimizwaje yale ya kwamba, sharti yawe vivyo hivyo?
55
Saa ile Yesu akawaambia yale makundi ya watu: Mmetoka wenye panga na rungu, mnikamate mimi, kama watu wanavyomwendea mnyang'anyi. Kila siku nilikaa hapa Patakatifu nikifundisha, lakini hamkunikamata.
56
Lakini haya yote yamekuwapo, Maandiko ya Wafumbuaji yatimizwe. Papo hapo wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.
57
Lakini wale waliomkamata Yesu wakampeleka kwa mtambikaji mkuu Kayafa; ndiko, walikokusanyika waandishi na wazee.
58
Lakini Petero akamfuata mbalimbali, mpaka akafika uani kwa mtambikaji mkuu, akaingia ndani akakaa pamoja na watumishi, uone mwisho.
59
Lakini watambikaji wakuu na baraza ya wakuu wote wakamtafutia Yesu ushuhuda wa uwongo, wapate kumwua.
60
Lakini hawakuupata, ingawa walikuja mashahidi wa uwongo wengi, lakini hawakumshinda.
61
Halafu wakaja wawili, wakasema: Huyu amesema: Nina nguvu ya kulivunja Jumba la Mungu na kulijenga tena muda wa siku tatu.
62
Ndipo, mtambikaji mkuu alipoinuka, akamwambia: Hujibu neno, hawa wanayokusimangia?
63
Lakini Yesu akanyamaza kinya. Mtambiakaji mkuu akamwambia: Ninakuapisha na kumtaja Mungu Mwenye uzima, utuambie, kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu!
64
Yesu akamwambia: Wewe ulivyosema, ndivyo. Tena nawaambiani: Tangu sasa mtamwona Mwana wa mtu, anavyokaa kuumeni kwa nguvu, tena atakavyokuja juu ya mawingu ya mbinguni.
65
Ndipo, mtambikaji mkuu alipozirarua nguo zake, akasema: Amekwisha kumbeza Mungu. Mashahidi tunawatakia nini tena? Tazameni, sasa hivi mmesikia, anavyombeza Mungu.
66
Mwaonaje? Nao wakajibu, wakasema: Amepaswa na kufa.
67
Kisha wakamtemea mate usoni, wakampiga makonde; wengine wakampiga makofi
68
wakisema: Tufumbulie, Kristo: ni nani aliyekupiga?
69
Naye Petero alikuwa nje, amekaa uani. Kijakazi mmoja akamjia, akasema: Hata wewe ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilea.
70
Akakana mbele yao wote akisema: Sijui unayoyasema.
71
Alipotoka uani na kufika mlangoni, mwingine akamwona, akawaambia wale waliokuwako: Huyu alikuwa pamoja na Yesu na Nasareti.
72
Akakana tena na kuapa akisema: Simjui mtu huyo.
73
Punde kidogo wakamjia Petero waliosimama pale, wakamwambia: Kweli, na wewe u mwenzao, kwa maana matamko yako yanakutambulisha.
74
Ndipo, alipoanza kujiapiza na kuapa akisema: Simjui mtu huyo! Mara hiyo jogoo akawika.
75
Hapo Petero akalikumbuka lile neno la Yesu, aliposema: Jogoo atakapokuwa hajawika, utakuwa umenikana mara tatu. Akatoka nje, akalia sana kwa uchungu.
← Chapter 25
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 27 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28