bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 6
Matthew 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 7 →
1
Angalieni, msigawie watu vipaji vyenu machoni pa watu, kwamba wawaone! Msipojiangalia hivyo, hamna mshahara kwa Baba yenu alioko mbinguni.
2
Basi, ukimgawia mtu usipigishe baragumu mbele yako kama wanavyofanya wajanja katika nyumba za kuombea na katika njia za mijini, wapate kutukuzwa na watu. Kweli nawaambiani: wamekwisha upata mshahara wao.
3
Lakini wewe ukimgawia mtu, mkono wako wa kushoto usitambue, wa kuume unayoyafanya,
4
huko kugawa kwako kuwe kumejificha! Ndipo, Baba yako anayeyaona hata yanayojificha atakapokulipa waziwazi.
5
Tena mnapomwomba Mungu msiwe kama wajanja! Kwani wanapenda kuomba wakisimama katika nyumba za kuombea na pembeni pa njia za mijini, watu wapate kuwaona. Kweli nawaambiani: wamekwisha upata mshahara wao.
6
Lakini wewe unapoomba uingie mwako chumba cha ndani na kuufunga mlango wako! Kisha umwombe Baba yako alioko fichoni! Ndipo, Baba yako anayeyaona hata yanayojificha atakapokulipa waziwazi.
7
Tena mnapoomba msijisemee maneno tu kama wamizimu! Kwani hudhani, ya kuwa maneno yao mengi yatawapatia kusikilizwa.
8
Msifanane nao! Kwani Baba yenu anayajua yanayowapasa, mnapokuwa hamjamwomba.
9
Ninyi mnapoomba mwombe hivi: Baba yetu ulioko mbinguni, Jina lako litakaswe!
10
Ufalme wako uje! Uyatakayo yatimizwe nchini, kama yanavyotimizwa mbinguni!
11
Tupe leo chakula chetu cha kututunza!
12
Tuondolee makosa yetu, kama nasi tulivyowaondolea waliotukosea!
13
Usituingize majaribuni! Ila tuokoe maovuni! Kwani wako ni ufalme na nguvu na utukufu kale na kale. Amin.
14
Kwani ninyi mnapowaondolea watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawandolea ninyi vilevile.
15
Lakini ninyi msipowaondolea watu makosa yao, hata Baba yenu hatawaondolea ninyi makosa yenu.
16
Tena mnapofunga msikunjamane nyuso kama wajanja! Kwani huzirembua nyuso, kusudi watu wawaone, wanavyofunga. Kweli nawaambiani: Wamekwisha upata mshahara wao.
17
Lakini wewe unapofunga jipake kichwa chako mafuta, unawe nao uso wako,
18
kusudi watu wasikuone, ya kama unafunga, ila akuone Baba yako alioko fichoni. Ndipo, Baba yako anayeyaona yanayojificha atakapokulipa.
19
Msijilimbikie malimbiko nchini, mende na kutu zinapoyaharibu! Nao wezi huyafukua na kwiba.
20
Lakini jilimbikieni malimbiko mbinguni, yasikoharibiwa na mende wala na kutu, wala wezi wasikoyafukua na kwiba!
21
Kwani limbiko lako liliko, ndiko, nao moyo wako utakakokuwa.
22
Taa ya mwili ni jicho. Basi jicho lako liking'aa, mwili wako wote utakuwa na mwanga.
23
Lakini jicho lako likiwa bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Basi, mwanga uliomo ndani yako unapokuwa giza, giza yenyewe itakuwaje?
24
*Hakuna mtu anayeweza kutumikia mabwana wawili. Kwani itakuwa hivi: atamchukia wa kwanza na kumpenda wa pili, au atashikamana naye wa kwanza na kumbeza wa pili. Hamwezi kuwatumikia wote wawili, Mungu na Mali za Nchini (Mamona).
25
Kwa hiyo nawaambiani: Msiyasumbukie maisha yenu mkisema: Tutakula nini? Tutakunywa nini? Wala msiisumbukie miili yenu mkisema: Tutavaa nini? Je? Maisha hayapiti vyakula? Nao mwili haupiti mavazi?
26
Watazameni ndege wa angani! Hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi waweke vichanjani. Naye Baba yenu wa mbinguni anawalisha nao. Je? Nyinyi hamwapiti hao?
27
Tena kwenu yuko nani anayeweza kwa kusumbuka kwake kujiongezea miaka yake kipande kama cha mkono mmoja tu?
28
Tena yale mavazi, mbona mnayasumbukia? Jifundisheni mnapoyatazama maua ya uwago yaliyoko porini kama yanavyokua! Hayafanyi kazi, wala hayafumi nguo.
29
Lakini nawaambiani: Hata Salomo katika utukufu wake wote hakuvikwa kama moja lao.
30
Basi Mungu akiyavika hivyo majani ya porini yanayokaa leo tu, kesho yatupwe katika mabiwi, yateketee, Je? Hatazidi kuwavika ninyi? Mbona mna mtegemea kidogo tu?
31
Basi msisumbuke mkisema: Tutakula nini? au: Tutakunywa nini? au: Tutavaa nini?
32
Kwani wamizimu ndio wanaoyatafuta hayo yote; lakini Baba yenu wa mbinguni amewajua, ya kuwa mnapaswa nayo hayo yote.
33
Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na wongofu wake! Ndivyo, mtakavyopewa hayo yote.
34
Basi, msisumbukie ya kesho! Kwani siku ya kesho itayasumbukia yaliyo yake. Inatosha, kila siku iwe na uovu wake.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28