bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 27
Matthew 27
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 28 →
1
Ilipokuwa asubuhi, watambikaji wakuu wote na wazee wa kwao wakamlia Yesu njama, kwamba wamwue.
2
Wakamfunga, wakaenda naye, wakamtia mikononi mwa Pilato aliyekuwa mtawala nchi.
3
Hapo Yuda aliyemchongea akamwona, ya kuwa amekwisha kuhukumiwa, akajuta, akazirudisha zile fedha 30 kwa watambikaji wakuu na kwa wazee
4
akisema: Nimekosa nilipotoa mtu asiyepaswa na kumwagwa damu yake. Wale wakasema: Jambo hilo hatumo, litazame mwenyewe!
5
Ndipo, alipozitupa zile fedha Jumbani mwa Mungu, akaondoka, akaenda zake, akajinyonga.
6
Kisha watambikaji wakuu wakaziokota zile fedha, wakasema: Ni mwiko kuzitia katiaka sanduku ya vipaji, kwa kuwa ni fedha za damu.
7
Wakazipigia shauri, wakazinunua shamba la mfinyanzi, liwe la kuzikia wageni.
8
Kwa hiyo shamba lile linaitwa hata leo Shamba la Damu.
9
Ndipo, yalipotimia, mfumbuaji Yeremia aliyoyasema: Wamezichukua fedha 30, ni upato wa mtu aliyeuzwa, waliomnunua kwa wana wa Isiraeli;
10
wakazitoa kununua shamba la mfinyanzi, kama Bwana alivyoniambia.
11
Yesu alipopelekwa mbele ya mtawala nchi, mtawala nchi akamwuliza akisema: Wewe ndiwe mfalme wa Wayuda? Yesu akamwambia: Wewe unavyosema, ndivyo.
12
Tena aliposutwa nao watambikaji wakuu na wazee hakujibu neno.
13
Pilato alipomwambia: Husikii yote, wanayokusimangia?
14
hakumjibu hata neno moja. Ikawa, mtawala nchi akastaajabu sana.
15
*Kwa desturi ya sikukuu mtawala nchi alikuwa amezoea kuwafungulia mfungwa mmoja, watu wengi waliyemtaka.
16
Siku zile palikuwa na mfungwa aliyejulikana kwa ubaya, jina lake Baraba.
17
Walipokusanyika, Pilato akawauliza: Mwamtaka yupi, niwafungulie? Baraba au Yesu anayeitwa Kristo?
18
Kwani aliwajua, ya kuwa wamemtoa kwa wivu.
19
Naye alipoketi katika kiti cha uamuzi, mkewe akatuma kwake kumwambia: Usijitie katika jambo la yule mwongofu! Kwani nimeteseka mengi kwa ajili yake katika ndoto za usiku wa leo.
20
Lakini watambikaji wakuu na wazee wakawashurutisha makundi ya watu, wamtake Baraba, wamwangamize Yesu.
21
Mtawala nchi akajibu akiwaambia: Katika hawawawili mwamtaka yupi, niwafungulie? Wakasema: Baraba!
22
Pilato akamwambia: Basi, Yesu anayeitwa Kristo nimfanyie nini? Wakasema wote: Na awambwe msalabani!
23
Aliposema: Ni kiovu gani, alichokifanya? wakakaza kupiga makelele wakisema: Na awambwe msalabani!
24
Pilato alipoona, ya kama hakuna linalofaa, ila matata yatakuwako mengi, akatwaa maji, akanawa mikono yake machoni pa watu, akasema: Mimi simo katika damu ya mtu huyu mwongofu, tazameni, ni shauri lenu!
25
Ndipo, watu wote walipojibu wakisema: Damu yake itujie sisi na watoto wetu!
26
Kisha akawafungulia Baraba, lakini Yesu akamtoa, apigwe viboko, kisha awambwe msalabani.
27
Ndipo, askari wa mtawala nchi walipompeleka Yesu bomani, wakakita kikosi chote cha askari, waje hapo, alipokuwa.
28
Wakamvua nguo zake, wakamvika kanzu nyekundu ya kifalme.
29
Wakasuka kilemba cha miiba, wakamvika kichwani, wakampa mwanzi mkononi mwake mwa kuume, wakampigia magoti, wakamfyoza na kusema: Pongezi, mfalme wa Wayuda!
30
Kisha wakamtemea mate, wakaushika ule mwanzi, wakampiga kichwani.
31
Walipokwisha kumfyoza wakamvua kanzu ya kifalme, wakamvika tena nguo zake, wakampeleka, wamwambe msalabani.*
32
Walipotoka wakaona mtu wa Kirene, jina lake Simoni; huyu wakamshurutisha, amchukulie msalaba wake.
33
Walipofika mahali panapoitwa Golgota, maana yake: Fuvu la Kichwa,
34
wakampa mvinyo iliyochanganyika na maji ya nyongo, anywe. Naye alipoyaonja hakutaka kunywa.
35
Walipokwisha kumwamba msalabani wakazigawanya nguo zake na kuzipigia kura, kusudi yatimie yaliyosemwa na mfumbuaji kwamba: Wakajigawanyia nguo zangu, nalo vazi langu wakalipigia kura.
36
Wakakaa wakimlinda palepale.
37
Juu ya kichwa chake wakabandika andiko la mashtaka yake ya kwamba: HUYU NI YESU, MFALME WA WAYUDA.
38
Pamoja naye wakawambwa misalabani wanyang, anyi wawili, mmoja kuumeni, mmoja kushotoni.
39
Waliopita wakamtukana, wakavitingisha vichwa vyao
40
wakisema: Wewe unayelivunja Jumba la Mungu na kulijenga tena kwa siku tatu, jiokoe mwenyewe! Ukiwa Mwana wa Mungu shuka msalabani!
41
Vilevile nao watambikaji wakuu pamoja na waandishi na wazee wakamfyoza wakisema:
42
Wengine aliwaokoa, lakini mwenyewe hawezi kujiokoa. Kama ndiye mfalme wa Waisiraeli, ashuke sasa hivi msalabani! Ndivyo, tutakavyomtegemea nasi.
43
Alimtegemea Mungu, na amwokoe sasa, kama anamtaka! kwani alisema: Mimi ni Mwana wa Mungu.
44
Vivyo hivyo wakamtukana hata wale wanyang'anyi waliowambwa misalabani pamoja naye.
45
Tangu saa sita pakawa na giza katika nchi yote mpaka saa tisa.
46
Ilipokuwa kama saa tisa, Yesu akapaza sauti sana akisema: Eli, Eli, lama sabaktani? Ni kwamba: Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
47
Wengine wao waliosimama hapo walipoyasikia wakasema: Huyu anamwita Elia.
48
Papo hapo mmoja wao akapiga mbio, akachukua mwani, akauchovya sikini na kuutia katika utete, akamnywesha.
49
Wengine wakasema: Acha, tuone, kama Elia anakuja kumwokoa!
50
Kisha Yesu akapaza tena sauti sana, akakata roho.
51
Papo hapo ndipo, pazia la Jumbani mwa Mungu lilipopasuka toka juu mpaka chini, likawa vipande viwili. Nchi ikatetemeka, miamba ikapasuka,
52
makaburi yakafunuka, ikafufuka miili mingi ya watu watakatifu waliolala,
53
wakatoka makaburini mwao, yeye alipokwisha kufufuka, wakauingia mji mtakatifu, wakatokea wengi, wawaone.
54
Lakini bwana askari nao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu walipoliona lile tetemeko na yale mambo yaliyokuwapo, wakaogopa sana, wakasema: Kweli, huyu alikuwa Mwana wa Mungu!
55
Pale palikuwa na wanawake wengi, walisimama mbali wakitazama; ndio waliomfuata Yesu toka Galilea wakimtumikia.
56
Kati yao walikuwapo Maria Magadalene na Maria, mama yao Yakobo na Yosefu, tena mama yao wana wa Zebedeo.
57
Ilipokuwa jioni, akaja mtu mwenye mali nyingi wa Arimatia, jina lake Yosefu; naye mwenyewe alikuwa mwanafunzi wa Yesu.
58
Huyo akaenda kwa Pilato, akataka kupewa mwili wa Yesu; ndipo, Pilato alipoagiza, apewe.
59
Yosefu akauchukua ule mwili, akaufunga kwa sanda nyeupe,
60
akauweka katika kaburi lake jipya, alilokuwa amelichonga mwambani. Akafingirisha jiwe kubwa mlangoni pa kaburi, akaenda zake.
61
Nao akina Maria Magadalene na Maria yule mwingine, walikuwa wamekaa hapa wakilielekea kaburi.
62
Kulipokucha, ni siku inayofuata maandalio ya kondoo ya Pasaka, watambikaji wakuu na Mafariseo wakamkusanyikia Pilato,
63
wakamwambia: Bwana, tumekumbuka, ya kuwa yule mdanganyifu alisema alipokuwa anaishi bado: Baada ya siku tatu nitafufuka.
64
Kwa hiyo agiza, kaburi lilindwe mpaka siku ya tatu, wanafunzi wake wasije, wamwibe, wakawaambia watu: Amefufuka katika wafu! madanganyo hayo ya mwisho yakawa mabaya kuliko yale ya kwanza.
65
Pilato akawaambia: Chukueni askari wa kulinda! Nendeni, mkalilinde kaburi, kama mnavyojua!
66
Nao wakaenda, wakaitia muhuri yao juu ya lile jiwe, wakawaweka askari hapo, walilinde kaburi.
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 28 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28