bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 10
Matthew 10
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 11 →
1
Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa nguvu za kufukuza pepo wachafu na za kuponya wagonjwa wo wote na wanyonge wo wote.
2
Majina yao wale mitume kumi na wawili ndiyo haya: Wa kwanza Simoni anayeitwa Petero na Anderea nduguye, Yakobo wa Zebedeo na Yohana nduguye,
3
Filipo na Bartolomeo, Toma na Mateo, mtoza kodi, Yakobo wa Alfeo na Tadeo,
4
Simoni wa Kana na Yuda Iskariota aliye mchongea halafu.
5
Hao kumi na wawili Yesu aliwatuma na kuwaagiza akisema: Msiende katika njia za wamizimu, wala mji wowote wa Wasamaria msiuingie!
6
Lakini mwende kwa kondoo waliopotea wa mlango wa Isiraeli!
7
Tena mnapokwenda pigeni mbiu mkisema: Ufalme wa mbingu umekaribia!
8
Walio wagonjwa waponyeni, waliokufa wafufueni, wenye ukoma watakaseni, nazo pepo zifukuzeni! Bure mmeyapata, tena yatoeni bure!
9
Msichukue mishipini mwenu dhahabu wala shilingi wala senti!
10
Msichukue mkoba wa njiani wala nguo mbili wala viatu wala fimbo! Kwani mtenda kazi hupaswa na kupewa chakula chake.
11
Lakini mji au kijiji mtakamoingia ulizeni, kama yumo mtu anayepaswa na kuwapokea! Kaeni mwake, mpaka mtakapotoka tena!
12
Tena mkiingia nyumbani wapeni salamu!
13
Ikiwa wamepaswa nao, utengemano wenu utakaa humo. Lakini ikiwa hawakupaswa nao, utengemano wenu utawarudia ninyi.
14
Tena mtu asipowapokea wala asipoyasikia maneno yenu, basi, kama ni nyumba au mji, mtokeni na kuyakung'uta mavumbi ya miguuni penu!
15
Kweli nawaambiani: Siku ya hukumu nchi ya Sodomu na Gomora itapata mepesi kuliko mji ule.
16
Tazameni, mimi nawatuma, mwe kama kondoo walio katikati ya mbwa wa mwitu. Kwa hiyo mwe wenye mizungu kama nyoka, tena mwe wakweli, kama njiwa walivyo! Jilindeni kwa ajili ya watu!
17
Kwani watawapeleka barazani kwao wakuu na kuwapiga katika nyumba zao za kuombea.
18
Kwa ajili yangu watawavuta kwa mabwana wakubwa na kwa wafalme, mje mnishuhudie kwao na kwa wamizimu.
19
Lakini hapo watakapowatoa, msihangaikie wala mizungu wala maneno ya kuwajibu! Kwani saa ileile mtapewa maneno, mtakayoyasema.
20
Kwani si ninyi mnaosema, ila ni Roho wa Baba yenu; ndiye anayesema vinywani mwenu.
21
Ndugu na ndugu watatoana, wauawe, hata baba watawatoa watoto wao, hata watoto watawainukia wazazi wao, wawaue.
22
Nanyi mtakuwa mmechukiwa na watu wote kwa ajili ya Jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokoka.
23
Lakini watakapowafukuza mjini humu kimbilieni mwingine! Kwani nawaambiani iliyo kweli: Hamtaimaliza miji ya Isiraeli, mpaka Mwana wa mtu atakapokuja.
24
*Mwanafunzi hampiti Mfunzi wake, wala mtumwa hampiti bwana wake.
25
Inamtosha mwanafunzi kuwa, kama mfunzi wake alivyo, vilevile mtumwa inamtosha kuwa, kama bwana wake alivyo. Kama Mwenye nyumba walimwita Belzebuli (Mkuu wa pepo), hawatazidi kuwaita hivyo waliomo nyumbani mwake?
26
Msiwaogope! Kwani hakuna lililofunikwa lisilofunuliwa halafu, wala hakuna lililofichwa lisilotambulikana halafu.
27
Ninalowaambia gizani lisemeni mwangani! Tena ninalowanong'oneza masikioni, litangazeni barazani!
28
Tena msiwaogope wanaoweza kuiua miili tu, wasiweze kuziua nazo roho! Lakini mfulize kumwogopa anayeweza kuziangamiza roho pamoja na miili shimoni mwa moto!
29
Je? Videge viwili haviuzwi kwa senti moja? Lakini hata mmoja wao haanguki chini, Baba yenu asipojua.
30
Lakini kwenu ninyi hata nywele za vichwani zimehesabiwa zote.
31
Kwa hiyo msiogope ninyi mnapita videge vingi!
32
Kila atakayeungama mbele ya watu, kwamba ni mtu wangu, nami nitaungama mbele ya Baba yangu wa mbinguni, kwamba ni mtu wangu.
33
Lakini atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele ya Baba yangu wa mbinguni.*
34
Msidhani, ya kuwa nimejia kuiletea nchi utengemano! Sikujia kuleta utengemano, ila upanga.
35
Kwani nimejia kutenga watu, wagombane mtu na baba yake, mwana wa kike na mama yake, vilevile mkwe na mkwewe,
36
nao watakaomchukia mtu ndio waliomo mwake.
37
Anayempenda baba yake au mama yake kuliko mimi hanipasi; anayempenda mwanawe wa kiume au wa kike kuliko mimi hanipasi.
38
Tena asiyejitwisha msalaba wake na kunifuata nyuma yangu hanipasi.
39
Mwenye kuiponya roho yake ataiangamiza; mwenye kuiangamiza roho yake kwa ajili yangu ataiponya.
40
Anayewapokea ninyi hunipokea mimi; naye anayenipokea mimi humpokea aliyenituma.
41
Anayepokea mfumbuaji, kwa kuwa ni mfumbuaji, atapata mshahara kama wa mfumbuaji; naye anayepokea mwongofu, kwa kuwa ni mwongofu, atapata mshahara kama wa mwongofu.
42
Tena mtu akinywesha mmoja wao walio wadogo kinyweo cha maji mazizima tu, kwa kuwa ni mwanafunzi, kweli nawaambiani: Mshahara wake hautampotea kamwe.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28