bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 17
Matthew 17
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 18 →
1
Baada ya siku sita Yesu akamchukua Petero na Yakobo na Yohana nduguye, akapanda pamoja nao peke yao juu ya mlima mrefu.
2
Huko akageuzwa sura yake machoni pao. Uso wake ukamulika kama jua, nazo nguo zake zikamerimeta kama mwanga.
3
Walipotazama, wametokewa na Mose na Elia, wanaongea na Yesu.
4
Petero akasema akimwambia Yesu: Bwana, hapa ni pazuri kuwapo sisi. Ukitaka, nitajenga hapa vibanda vitatu; kimoja chako, na kimoja cha Mose, na kimoja cha Elia.
5
Angali akisema, mara wingu jeupe likawatia kivuli, sauti ikatoka winguni, ikisema: Huyu ndiye mwanangu mpendwa, ambaye nimependezwa naye. Msikilizeni yeye!
6
Wanafunzi walipoyasikia wakaanguka kifudifudi, wakaingiwa na woga sana.
7
Yesu akawaendea, akasema akiwagusa: Inukeni, msiogope!
8
Walipoyainua macho yao, hakuna waliyemwona, asipokuwa Yesu peke yake.
9
Walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu akawaagiza akisema: Msimwambie mtu ye yote mliyoyaona, mpaka Mwana wa mtu atakapofufuliwa katika wafu!*
10
Nao wanafunzi wakamwuliza wakisema: Basi, waandishi husemaje: Sharti kwanza Elia aje?
11
Naye akajibu akisema: Kweli Elia anakuja, vyote avigeuze kuwa vipya.
12
Lakini nawaambiani: Elia amekwisha kuja, nao hawakumtambua, wakamtendea yote, waliyoyataka. Hivyo hata Mwana wa mtu atateswa nao.
13
Hapo ndipo wanafunzi walipojua, ya kuwa amewaambia mambo ya Yohana Mbatizaji.
14
Walipofika penye kundi la watu, mtu akamjia, akampigia magoti, akasema:
15
Bwana, umhurumie mwanangu! Kwani ni mwenye kifafa, aumia vibaya. Kwani mara nyingi huanguka motoni, tena mara nyingi huanguka majini.
16
Nikampeleka kwa wanafunzi wako, lakini hawakuweza kumponya.
17
Yesu akajibu akisema: Enyi wa kizazi kisichomtegemea Mungu kwa kupotoka! Nitakuwapo nanyi mpaka lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni hapa, nilipo!
18
Yesu alipomkaripia, pepo akamtoka; naye mtoto akapona tangu saa ileile.
19
Kisha wanafunzi wakamjia Yesu, alipokuwa peke yake, wakasema: Mbona sisi hatukuweza kumfukuza huyo?
20
Naye akawaambia: Ni kwa ajili hammtegemei Mungu vema. Maana nawaambia la kweli: Cheo chenu cha kumtegemea Mungu kikiwa kidogo kama kipunje cha mbegu, mtauambia mlima huu: Ondoka hapa, ulipo, uende pale! nao utaondoka. Hivyo halitakuwako neno lisilowezekana nanyi.
21
Lakini kabila hili la pepo halitoki isipokuwa kwa nguvu ya kuomba na ya kufunga.
22
Walipokuwa wakizunguka huko Galilea, Yesu akawaambia: Mwana wa mtu atatiwa mikononi mwa watu,
23
nao watamwua, kisha siku ya tatu atafufuliwa. Wakasikitika sana.
24
Walipofika Kapernaumu, watoza kodi wakamjia Petero, wakasema: Mfunzi wenu halipo kodi?
25
Akasema: Hulipa. Naye alipokuja nyumbani, Yesu akaanza kumwuliza akisema: Waonaje, Simoni, wafalme wa nchi huwatoza watu gani chango au kodi? Wana wao wenyewe au wageni?
26
Alipojibu: Huwatoza wageni, Yesu akamwambia: Basi, wana wenyewe hawatozwi.
27
Lakini tusiwakwaze! Nenda pwani, uloe kwa ndoana! Kisha samaki wa kwanza atakayezuka umshike, ufumbue kinywa chake! Mle utaona fedha, itwae, ukawape kwa ajili yetu, mimi na wewe!
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 18 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28