bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 18
Matthew 18
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 19 →
1
Saa ile wanafunzi wakamjia Yesu, wakamwuliza wakisema: Aliye mkuu katika ufalme wa mbingu ni nani?
2
Akaita kitoto, akamsimamisha katikati yao,
3
akasema: Kweli nawaambiani: Msipogeuka, mkawa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbingu.
4
Mtu atakayejinyenyekeza mwenyewe, awe kama kitoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbingu.
5
Naye atakayepokea kitoto mmoja kama huyu kwa jina langu hunipokea mimi.
6
Lakini mtu atakayekwaza mmoja tu aliye mwenzao hawa wadogo wanaonitegemea inamfaa kutungikwa shingoni pake jiwe kubwa la kusagia, kisha atoswe kilindini mwa bahari.
7
Yako yatakayoupata ulimwengu kwa ajili ya makwazo. Kweli makwazo sharti yaje, lakini mtu yule anayelileta kwazo atapatwa na mambo.
8
Nawe, mkono wako ukikukwaza, au mguu wako ukikukwaza, uukate uutupe mbali! Kuingia penye uzima mwenye kilema au kiwete kutakufaa kuliko hapo, ukiwa mwenye mikono miwili au miguu miwili, ukatupwa katika moto usiozimika kale na kale.
9
Nalo jicho lako likikukwaza, basi ling'oe ulitupe mbali! Kuingia penye uzima mwenye chongo kutakufaa kuliko hapo, ukiwa mwenye macho mawili, ukatupwa shimoni mwa moto.
10
Tazameni, msiwabeze wadogo hawa hata mwenzao mmoja! Kwani nawaambiani: Malaika zao mbinguni huutazama siku zote uso wa Baba yangu alioko mbinguni.
11
Kwani Mwana wa mtu amekuja kukiokoa kilichoangamia.
12
Mwaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, tena mmoja wao akipotea, hatawaacha wale tisini na tisa milimani, aende kumtafuta yule aliyepotea?
13
Naye akipata kumwona, kweli nawaambiani: Atamfurahia kuliko wale tisini na tisa wasiopotea.
14
Vivyo hivyo Baba yenu alioko mbinguni hataki, hawa walio wadogo hata mmoja wao apotee.
15
Ndugu yako akikukosea, nenda kamwonye, wewe na yeye mko peke yenu! Akikusikia, umempata tena ndugu yako.
16
Lakini asipokusikia, chukua pamoja na wewe tena mmoja au wawili! Maana kila shauri limalizike kwa kusemewa na mashahidi wawili au watatu.
17
Naye akikataa kuwasikia hao, waambie wateule wenziwe shauri hilo! Lakini atakapokataa kuwasikia nao wateule, awe kwako kama mtu wa kimizimu au mtoza kodi!
18
Kweli nawaambiani: Lo lote, mtakalolifunga nchini, litakuwa limefungwa hata mbinguni; nalo lo lote, mtakalolifungua nchini, litakuwa limefungwa hata mbinguni; nalo lo lote, mtakalolifungua nchini, litakuwa limefunguliwa hata mbinguni.
19
Tena nawaambiani: Kila jambo, wenzenu wawili nchini watakalopatana kuliomba, watapewa na Baba yangu alioko mbinguni.
20
Kwani watu wawili au watatu wanapolikusanyikia Jina langu, nami nipo hapo katikati yao.
21
*Ndipo, Petero alipomjia, akamwambia: Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi, nikimwondolea? Yatosha mara saba?
22
Yesu akamwambia: Sikuambii: Mwondolee mara saba, ila mwondolee mara sabini mara saba!
23
Kwa sababu hiyo ufalme wa mbingu umefanana na mfalme aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake.
24
Alipoanza kuhesabu akaletewa mmoja mwenye madeni ya mizigo 10000 ya fedha.
25
Naye alipokosa vya kumlipa, bwana akaagiza, wauzwe yeye na mkewe na watoto wake navyo vyote, alivyokuwa navyo, deni lipate kulipika.
26
Mtumwa akamwangukia, akamlalamikia akisema: Nivumilie, nitakulipa yote!
27
Bwana akamwonea uchungu yule mtumwa, akamfungua, akamwachilia hata deni lake.
28
Lakini yule mtumwa alipotoka akamwona mtumwa mwenziwe mmoja aliyekuwa mdeni wake wa shilingi 100. Akamkamata, akamshika koo, akasema: Lipa deni lako!
29
Mtumwa mwenziwe akaanguka miguuni pake, akambembeleza akisema: Nivumilie, nitakulipa!
30
Lakini yule hakutaka, akaenda, akamtia kifungoni, mpaka atakapolilipa lile deni.
31
Basi, watumwa wenziwe walipoyaona yaliyokuwa wakasikitika sana. Wakaja, wakamweleza bwana wao hayo yote yaliyokuwa.
32
Ndipo, bwana wake alipomwita, akamwambia: Wee mtumwa mbaya, lile deni lote nalikuachilia, uliponibembeleza.
33
Wewe nawe haikukupasa kumhurumia mtumwa mwenzio, kama nilivyokuhurumia mimi?
34
Bwana wake akakasirika, akamtoa, afungwe, mpaka atakapolilipa deni lake lote.
35
Ndivyo, naye Baba yangu wa mbinguni atakavyowatendea ninyi, msipoondoleana mioyoni mwenu kila mtu na ndugu yake.*
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 19 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28