bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Matthew 23
Matthew 23
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 24 →
1
Kisha Yesu akasema na watu waliokutanika na wanafunzi wake,
2
kwamba: Kitini pa Mose wamekaa waandishi na Mafariseo.
3
Yo yote, watakayowaambia, yafanyeni na kuyashika! Lakini kama wafanyavyo, msiyafuate! Kwani kusema wanasema, lakini hawayafanyi.
4
Huwafungia watu mizigo mizito isiyochukulika wakiwawekea mabegani, lakini wenyewe hawataki kuigusa hata kwa kidole chao kimoja tu.
5
Matendo yao yote huyafanyia kutazamwa na watu. Hukuza makaratasi ya kuombea, huviongeza navyo vishada vya nguo zao, viwe vinene.
6
Wakialikwa chakulani hupenda kukaa penye wakuu, namo nyumbani mwa kuombea hupenda viti vya mbele.
7
Hupenda kuamkiwa na watu sokoni na kuitwa mfunzi mkuu.
8
Lakini ninyi msitake kuitwa mfunzi mkuu! Kwani mfunzi wenu ni mmoja, ndiye Kristo, nanyi nyote ni ndugu.
9
Tena nchini msimwite mtu baba yenu! Kwani baba yenu ni mmoja, ni wa mbinguni.
10
Wala msitake kuitwa kiongozi! Kwani kiongozi wenu ni mmoja, ni Kristo.
11
Lakini kwenu aliye mkubwa na awatumikie ninyi!
12
Kwani atakayejikweza mwenyewe atanyenyekezwa; naye atakayejinyenyekeza mwenyewe atakwezwa.
13
Yatawapata ninyi waandishi na Mafariseo mlio wajanja, kwani mnawafungia watu mlango wa ufalme wa mbingu. Ninyi hamwingii, nao wanaotaka kuingia hamwaachi, waingie.
14
Yatawapata ninyi waandishi na Mafariseo mlio wajanja, kwani mnazila nyumba za wajane mkijitendekeza, kama mnakaza kuwaombea. Kwa hiyo mapatilizo yenu yatakuwa kuliko ya wengine.
15
Yatawapata ninyi waandishi na Mafariseo mlio wajanja, kwani mnazunguka baharini na katika nchi kavu, mpate mfuasi mmoja tu; kisha hapo akipatikana, mnamgeuza kuwa wa kutumbukizwa motoni kuwapita ninyi kabisa.
16
Yatawapata ninyi viongozi vipofu mnaosema: Mtu atakapoapa na kulitaja Jumba la Mungu, si kitu; lakini mtu atakapoapa na kuitaja dhahabu ya Jumba la Mungu amejifunga!
17
Wajinga na vipofu ninyi! Iliyo kubwa ni nini? Dhahabu au Jumba la Mungu linaloitakasa dhahabu?
18
Tena mnasema: Mtu atakapoapa na kuitaja meza ya Bwana, si kitu; lakini atakapoapa na kukitaja kipaji kilichoko juu yake amejifunga!
19
Vipofu ninyi! Iliyo kubwa ni nini? Kipaji au meza ya Bwana inayokitakasa kipaji?
20
Mtu anayeapa na kuitaja meza ya Bwana huapa na kuitaja hiyo meza pamoja navyo vyote vilivyopo pake.
21
Tena mtu anayeapa na kulitaja Jumba la Mungu huapa na kulitaja hilo Jumba pamoja naye yule anayekaa humo.
22
Tena mtu anayeapa na kuitaja mbingu huapa na kukitaja kiti cha kifalme cha Mungu pamoja na yeye anayekikalia.
23
Yatawapata ninyi waandishi na Mafariseo mlio wajanja, kwani fungu la kumi mnalitolea hata mchicha na nyanya na pilipili, lakini yaliyo magumu katika Maonyo mmeyaacha, yale ya hukumu na ya huruma na ya mategemeo. Haya yawapasa kuyashika pasipo kuyaacha yale.
24
Viongozi vipofu ninyi, mbu mnawatema, lakini ngamia mnawameza!
25
Yatawapata ninyi waandishi na Mafariseo mlio wajanja, kwani vinyweo na vyano mnaviosha nje, lakini ndani vimejaa mapokonyo na mapujufu.
26
Fariseo kipofu, kwanza osha ndani yake kinyweo na chano, vipate kuwa safi hata nje!
27
Yatawapata ninyi waandishi na Mafariseo mlio wajanja, kwani mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo huonekana nje kuwa mazuri, lakini ndani hujaa mifupa ya wafu na uchafu wote.
28
Vivyo hivyo nanyi nje mnaonekana kwa watu kuwa waongofu, lakini ndani yenu imejaa ujanja na upotovu.
29
Yatawapata ninyi waandishi na Mafariseo mlio wajanja, kwani mnayajenga makaburi ya wafumbuaji, tena mnayapamba makumbusho ya waongofu
30
na kusema: Sisi kama tungalikuwapo siku za baba zetu, basi, hatungalifanya nao bia ya kuwaua wafumbuaji.
31
Hivyo mnajishuhudia wenyewe, ya kuwa m-wana wao waliowaua wafumbuaji.
32
Nanyi kijazeni kipimo cha baba zenu!
33
M nyoka, m wana wa chatu! Mtaikimbiaje hukumu ya kutumbukizwa shimoni mwa moto?
34
*Kwa sababu hii tazameni, mimi natuma kwenu wafumbuaji na werevu wa kweli na waandishi; wengine wao mtawaua na kuwawamba misalabani, wengine wao mtawapiga katika nyumba zenu za kuombea, kisha mtawafukuza mji kwa mji;
35
hivyo zitawajia damu zote za waongofu zilizomwagwa nchini, kuanzia damu ya Abeli aliyekuwa mwongofu mpaka kuifikia damu ya Zakaria, mwana wa Berekia, mliyemwua katikati ya Jumba la Mungu na meza ya Bwana.
36
Kweli nawaambiani: hayo yote yatawajia wao wa kizazi hiki.
37
Yerusalemu, Yerusalemu, unawaua wafumbuaji, ukawapiga mawe walitumwa kwako! Mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako, kama kuku anavyovikusanya vifaranga vyake mabawani! Lakini hamkutaka!
38
Mtaona, Nyumba yenu ikiachwa, iwe peke yake!
39
Kwani nawaambiani: Tangu sasa hamtaniona tena, mpaka mtakaposema: Na atukuzwe ajaye kwa Jina la Bwana!*
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 24 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28