bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 1
2 Chronicles 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 2 →
1
Salomo, mwana wa Dawidi, akajipatia nguvu katika ufalme, naye Bwana Mungu wake akawa naye, akampa ukuu uliozidi.
2
Ndipo, Salomo alipowaita Waisiraeli wote, wakuu wa maelfu na wa mamia na waamuzi na watukufu wa Waisiraeli wote waliokuwa vichwa vya milango,
3
wakaenda, yeye Salomo pamoja na huo mkutano wote, kilimani kwa Gibeoni, kwani ndiko, lilikokuwa Hema la Mkutano la Mungu, Mose, mtumishi wa Bwana, alilolitengeneza nyikani.
4
Lakini Sanduku la Mungu Dawidi alikuwa amelitoa Kiriati-Yearimu, akaliweka hapo, alipolitengenezea yeye Dawidi, kwani alilipigilia hema Yerusalemu.
5
Lakini meza ya shaba ya kutambikia, aliyoitengeneza Besaleli, mwana wa Uri, mwana wa Huri, ilikuwa huko mbele ya Kao lake Bwana; ndiyo, Salomo na mkutano waliyoiendea.
6
Salomo akamtambikia Bwana huko juu ya ile meza ya shaba iliyokuwa penye Hema la Mkutano, akatoa ng'ombe elfu za tambiko za kuteketezwa nzima juu yake hiyo meza.
7
*Usiku huo Mungu akamtokea Salomo, akamwambia: Omba kwangu, uyatakayo, nikupe!
8
Salomo akamwambia Mungu: wewe ulimfanyizia baba yangu Dawidi mambo ya upole mwingi, ukanipa kuwa mfalme mahali pake.
9
Sasa Bwana Mungu, neno lako, ulilomwambia baba yangu Dawidi, na litiwe nguvu, litimie! Kwani wewe umenipa kuwa mfalme wa watu walio wengi kama mavumbi ya nchi.
10
Sasa nipe werevu wa kweli, nipate kujua penye kutoka mbele ya watu hawa na penye kuingia! Kwani mimi ni mtu gani wa kujua kuwaamua hawa watu wengi walio ukoo wako?
11
Ndipo, Mungu alipomwambia salomo: Kwa kuwa jambo kama hili limo moyoni mwako, ukaacha kuniomba mali na mapato mengi na utukufu na kufa kwa wachukivu wako, wala hukuniomba siku nyingi za kuwapo, ila umejiombea werevu wa kweli, upate kujua, jinsi utakavyowaamua walio ukoo wangu, niliokupa, uwe mfalme wao,
12
kwa hiyo umekwisha kupewa werevu wa kweli na ujuzi, tena nitakupa mali na mapato mengi na utukufu, wasioupata wafalme wote waliokuwako mbele yako, nao watakaokuwako nyuma yako hawatayapata.*
13
Kisha Salomo akaondoka kilimani kwa Gibeoni, akaja Yerusalemu akitoka kwenye Hema la Mkutano, akawa mfalme wa Waisiraeli.
14
Salomo akakusanya magari na wapanda farasi, hata akawa na magari 1400 na wapanda farasi 12000, akawakalisha katika miji ya magari namo mwake mfalme mle Yerusalemu.
15
Mfalme akajipatia fedha na dhahabu kuwa nyingi mle Yerusalemu kama mawe, nayo miti ya miangati akajipatia kuwa mingi kama mitamba katika nchi ya tambarare.
16
Nao farasi, Salomo aliokuwa nao, walitoka Misri, wachuuzi wengi wa mfalme waliwaleta wengi wakiwanunua na kuzilipa bei zao.
17
Magari, waliyoyatoa Misri na kuyapeleka kwao, moja lilikuwa fedha 600, na farasi mmoja fedha 150.
18
Vivyo hivyo waliwapelekea nao wafalme wote wa Wahiti na wafalme wa Ushami kwa mikono yao.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36