bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 35
2 Chronicles 35
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 34
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 36 →
1
Kisha Yosia akamfanyia Bwana huko Yerusalemu sikukuu ya Pasaka, wakachinja wana kondoo wa Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.
2
Akawaagiza watambikaji kuja kuzifanya kazi zao ziwapasazo, akawashikiza mioyo, watumikie Nyumbani mwa Bwana.
3
Akawaambia Walawi waliowafundisha Waisiraeli wote, waliokuwa watakatifu wa Bwana: Liwekeni Sanduku takatifu katika hiyo Nyumba, aliyoijenga Salomo, mwana wa Dawidi, mfalme wa Waisiraeli! Msilichukue tena mabegani! Sasa mtumikieni Bwana Mungu wenu, mwatumikie nao walio ukoo wake,
4
mkijiweka tayari kwa milango ya baba zenu na kwa zamu zenu, kama Dawidi, mfalme wa Isiraeli, alivyoviandika, na kama mwanawe Salomo alivyoviandika naye.
5
Simameni Patakatifu kwa vyama vya milango ya baba vya ndugu zenu walio watuwatu tu, kila fungu la mlango mmoja lipate Walawi.
6
Kisha wachinjeni wana kondoo wa Pasaka na kujitakasa, kuwatengenezeeni ndugu zenu na kufanya, kama Bwana alivyoagiza kinywani mwa Mose!
7
Kisha mfalme akawatolea watu kondoo na wana mbuzi, wote kuwa wa Pasaka wa watu wote waliooneka, wote wakawa 30000 na ng'ombe 3000, wote walitoka katika makundi ya mfalme.
8
Nao wakuu wake waliwatolea watu na watambikaji na Walawi vipaji kwa kupenda wenyewe: Hilkia na Zakaria na Yehieli waliokuwa wenye amri Nyumbani mwa Mungu waliwapa watambikaji wana kondoo wa Pasaka 2600 na ng'ombe 300.
9
Nao wakuu wa Walawi Konania na ndugu zake Semaya na Netaneli, tena Hasabia na Yieli na Yozabadi waliwatolea Walawi kondoo wa Pasaka 5000 na ng'ombe 500.
10
Utumishi ulipokwisha kutengenezwa, watambikaji wakaja kusimama mahali pao, nao Walawi kwa zamu zao, kama mfalme alivyoagiza.
11
Walipowachinja wana kondoo wa Pasaka, watambikaji wakazipokea damu mikononi mwao wakazinyunyiza, nao Walawi wakawa wakichuna.
12
Wakaziondoa nyama za kuchoma na kuvipa vyama vya milango yao walio watuwatu tu, wenyewe wamtolee Bwana, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Mose. Nao ng'ombe wakawafanya vivyo hivyo.
13
Kisha nyama za Pasaka wakazioka motoni, kama walivyoagizwa; lakini zile za vipaji vitakatifu wakazipika katika vyungu na katika masufuria na katika makaango, wakazipelekea upesi wale walio watuwatu tu.
14
Kisha wakajiandalia wenyewe na watambikaji, kwani watambikaji, wana wa Haroni, walifanya kazi za kuziteketeza ng'ombe za tambiko pamoja na mafuta mpaka usiku. Kwa hiyo Walawi wakajiandalia wenyewe na watambikaji, wana wa Haroni.
15
Nao waimbaji, wana wa Asafu, walisimama mahali pao, kama Dawidi na Asafu na Hemani na Yedutuni, mchunguzaji wa mfalme, walivyoviagiza; nao walinda malango walisimama kila penye lango lake, hawakuwa na shuruti kuondoka katika utumishi wao, kwani ndugu zao Walawi waliwaandalia.
16
Ndivyo, kazi zote za utumishi wa Bwana zilivyotengenezwa siku ile ya kufanya Pasaka pamoja na kuteketeza ng'ombe za tambiko mezani pa kumtambikia Bwana, kama mfalme Yosia alivyoagiza.
17
Nao wana wa Isiraeli waliokuwako wakafanya Pasaka siku hiyo, nayo hiyo sikukuu ya Mikate isiyochachwa wakaila siku saba.
18
Pasaka kama hii haikufanywa kwa Waisiraeli tangu siku za mfumbuaji Samweli; wafalme wote wa Waisiraeli hawakufanya Pasaka, kama Yosia alivyoifanya pamoja na watambikaji na Walawi na Wayuda na Waisiraeli wote waliokuwako na wenyeji wa Yerusalemu.
19
Pasaka hii ikafanywa katika mwaka wa kumi na nane wa ufalme wa Yosia.
20
Hayo yote, aliyoyafanya ya kuitengeneza Nyumba hiyo, yalipokwisha kufanyika, akapanda Neko, mfalme wa Misri, kwenda kupigana Karkemisi penye jito la Furati, naye Yosia akatoka kumpinga.
21
Yule akatuma wajumbe kwake kumwambia: Tuko na neno gani mimi na wewe, mfalme wa Yuda? Leo sikukujia wewe, ila ule mlango ninaotaka kupigana nao. Naye Mungu ameniagiza kwenda upesi; jiepushe kwake Mungu aliye upande wangu, asije kukuangamiza!
22
Lakini Yosia hakuugeuza uso wake na kumwacha, ila alijipa moyo mwingine kwenda kupigana naye, asiyasikie maneno ya Neko yaliyotoka kinywani mwa Mungu, akaenda kupigana naye bondeni kwa Megido.
23
Wenye kupiga mishale wakampiga mfalme Yosia; ndipo, mfalme alipowaambia watumishi wake: Nipitisheni huku! Kwani nimeumia sana.
24
Ndipo, watumishi wake walipomtoa katika gari na kumweka katika gari la pili, alilokuwa nalo, wakampeleka Yerusalemu; ndiko, alikokufa. Wakamzika makaburini kwa baba zake. Nao Wayuda na Wayerusalemu wote wakamlilia Yosia,
25
naye Yeremia akamwombolezea Yosia. Nao waimbaji wote waume na wake humtaja Yosia katika maombolezo yao hata siku hii ya leo; hivi vikawa desturi kwao Waisiraeli, nayo yamekwisha kuandikwa katika maombolezo.
26
Mambo mengine ya Yosia na matendo ya upole wake yaliyopatana nayo yaliyoandikwa katika Maonyo ya Bwana,
27
nayo mambo yake ya kwanza na ya mwisho tunayaona, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Waisiraeli na wa Wayuda.
← Chapter 34
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 36 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36