bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 13
2 Chronicles 13
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 14 →
1
Katika mwaka wa 18 wa mfalme Yeroboamu Abia akapata kuwa mfalme wa Wayuda.
2
Akawa mfalme mle Yerusalemu miaka 3; jina la mama yake ni Mikaya, binti urieli wa Gibeoni. Naye akapiga vita na Yeroboamu.
3
Abia akajifunga kwenda vitani mwenye vikosi vya mafundi wa vita, watu 400000 waliochaguliwa. Naye Yeroboamu akajipanga vitani mwenye watu 800000 waliochaguliwa kwa kuwa mafundi wa vita wenye nguvu.
4
Abia akaondoka kuja kusimama juu ya mlima wa Semaraimu ulioko milimani kwa Efuraimu, akasema: Nisikilizeni, Yeroboamu nanyi Waisiraeli wote!
5
Je? Hamjui, ya kuwa Bwana Mungu wa Isiraeli alimpa Dawidi kuwa mfalme wa Waisiraeli kale na kale, yeye na wanawe, alipofanya naye agano la chumvi?
6
Lakini Yeroboamu, mwana wa Nebati, aliyekuwa mtumishi wa Salomo, mwana wa Dawidi, akaondoka kwa kumkataa bwana wake na kuacha kumtii.
7
Wakakusanyika kwake watu walio wa ovyoovyo tu wasiofaa kitu, wakajipatia nguvu za kumshinda Rehabeamu, mwana wa Salomo; kwani Rehabeamu alikuwa akingali kijana, nao moyo wake mchanga, hakuweza kujishupaza mbele yao.
8
Sasa ninyi mnajiwazia, ya kuwa mtaweza kujishupaza mbele ya ufalme wa Bwana uliomo mikononi mwa wana wa Dawidi, kwa kuwa kwenu ni uvumi wa watu wengi, nazo ndama za dhahabu mnazo, Yeroboamu alizowatengenezea kuwa miungu yenu.
9
Hamkuwafukuza watambikaji wa Bwana, wana wa Haroni, pamoja na Walawi, mkajifanyizia watambikaji, kama makabila ya nchi hizi? Kila ajaye na kuleta mtoto mume wa ng'ombe na madume saba ya kondoo, apate kulijaza gao lake, basi, hupata kuwa mtambikaji wao isiyo miungu.
10
Lakini sisi Bwana Mungu wetu hakutuacha, nao wana wa Haroni wanamtumikia Bwana kuwa watambikaji, nao Walawi wanafanya kazi zao;
11
kila kunapokucha na kila kunapokuchwa humvukizia Bwana wakimteketezea ng'ombe za tambiko na kumvikizia mavukizo yanukayo vizuri, tena humwekea mikate katika meza iliyo ya dhahabu tupu, tena hukiwasha kinara cha dhahabu na taa zake kila kunapokuchwa, kwani sisi tunaushika ulinzi wa Bwana Mungu wetu, lakini ninyi mmemwacha.
12
Na mwone, ya kuwa Mungu yuko kwetu, ndiye anayetutangulia, nao watambikaji wake watapiga matarumbeta ya kuvumisha sana, wawazomee ninyi! Wana wa Isiraeli, msije kupigana na Mungu wa baba zenu! Kwani hamtafanikiwa.
13
Lakini Yeroboamu alikuwa ametuma wengine, wawazunguke, wapate kuwavizia huko nyuma kuwajia migongoni kwao; kwa hiyo wengine wao walikuwa mbele ya Wayuda, nao waliowavizia walikuwa nyuma yao.
14
Wayuda walipogeuka wakaona, ya kuwa hawana budi kupigana mbele na nyuma; ndipo, walipomlilia Bwana, watambikaji wakayapiga matarumbeta yao.
15
Kisha watu wa Yuda wakapiga yowe; ikawa, watu wa Yuda walipopiga yowe, Mungu akampiga Yeroboamu na Waisiraeli wote mbele ya Abia na ya Wayuda.
16
Ndipo, wana wa Isiraeli walipowakimbia Wayuda, naye Mungu akawatia mikononi mwao.
17
Abia na watu wake wakawapiga, pigo likawa kubwa mno; kwao Waisiraeli wakaanguka kwa kuuawa watu 500000, nao ni watu wliochaguliwa.
18
Ndivyo, wana wa Isiraeli walivyonyenyekezwa siku zile, lakini wana wa Yuda wakapata nguvu, kwa kuwa walimwegemea Bwana Mungu wa baba zao.
19
Abia akakimbia, amfuate Yeroboamu na kumfukuza, akateka kwake miji, ndio Beteli na mitaa yake na Yesana na mitaa yake na Efuraimu na mitaa yake.
20
Yeroboamu hakupata nguvu tena katika hizo siku za Abia, kisha Bwana akampiga, akafa.
21
Abia akajipatia nguvu, akajichukulia wanawake 18, akazaa wana wa kiume 22 na wa kike 16.
22
Mambo mengine ya Abia na njia zake na maneno yake yameandikwa katika kitabu cha maelezo ya mfumbuaji Ido.
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36