bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 5
2 Chronicles 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 6 →
1
Kazi zote, ambazo Salomo aliifanyia nyumba ya Bwana zilipomalizika, Salomo akavipeleka vipaji vitakatifu vyote vya baba yake Dawidi pamoja na fedha na dhahabu na vyombo vyote, akaviweka penye vilimbiko vya nyumba ya Mungu.
2
Kisha Salomo akawakusanya wazee wa Waisiraeli nao wote waliokuwa vichwa vya mashina nao wakuu wa milango ya wana wa Isiraeli mle Yerusalemu kwenda kulitoa Sanduku la Agano la Bwana katika mji wa Dawidi ulioitwa Sioni.
3
Ndipo, watu wote wa Isiraeli walipkusanyika kwa mfalme kufanya sikukuu, ikawa mwezi wa saba.
4
Wazee wote wa Isiraeli walipokwisha fika, Walawi wakalichukua hilo Sanduku.
5
Wakalipeleka Sanduku pamoja na Hema la Mkutano na vyombo vitakatifu vyote vilivyokuwa Hemani, hivyo watambikaji walio Walawi wakavipandisha.
6
Naye mfalme Salomo pamoja na mkutano wote wa Waisiraeli waliokusanyika kwake mbele ya hilo Sanduku wakatoa mbuzi na kondoo na ng'ombe kuwa ng'ombe za tambiko, nao hawakuhesabika, wala hawakuwangika kwa kuwa wengi mno.
7
Watambikaji wakaliingiza Sanduku la Agano la Bwana mahali pake katika chumba cha ndani kiitwacho Patakatifu Penyewe, wakaliweka chini ya mabawa ya Makerubi.
8
Yale Makerubi yalikuwa yameyakunjua mabawa juu ya mahali pale, Sanduku lilipowekwa; ndivyo, Makerubi yalivyolifunika juu hilo Sanduku nayo mipiko yake.
9
Kwa urefu wa mipiko pembe zao hii mipiko zikaoneka kutoka penye Sanduku kuelekea mle chumbani mwa ndani, lakini nje hazikuoneka; nayo imo humo mpaka siku hii ya leo.
10
Mle Sandukuni hamkuwamo na kitu, ni zile mbao mbili tu, Mose alizozitia huko Horebu, Bwana alipofanya Agano na wana wa Isiraeli, walipotoka Misri.
11
Kisha watambikaji wakatoka Patakatifu; nao hawa watambikaji waliooneka hapo walikuwa wamejitakasa wote pasipo kuziangalia zamu zao,
12
nao waimbaji wote pia walio Walawi, wale wa Asafu na wa Hemani na wa Yedutuni pamoja na wana wao na ndugu zao, wote walikuwa wamevaa nguo za bafta, wakashika patu na mapango na mazeze, wakawa wamesimama upande wa maawioni kwa jua penye meza ya kutambikia, tena walikuwako pamoja na watambikaji 120 wenye kupiga matarumbeta.
13
Palipotukia pa kupigia matarumbeta na kuimba nyimbo, ikawapasa wote kuzisikiza sauti zao kwa mara moja kuwa kama mtu mmoja tu, wamshangilie Bwana na kumshukuru wakipaza sauti na kupiga matarumbeta na patu na vyombo vyote vya kuimbia, wamshangilie Bwana, ya kuwa ni mwema, ya kuwa upole wake ni wa kale na kale. Ndipo, Nyumbani mlipojaa wingu, humo Nyumbani mwa Bwana.
14
Nao watambikaji hawakuweza kusimama humo na kuzifanya kazi za utumishi wao kwa ajili ya hilo wingu, kwani utukufu wa Bwana uliijaza Nyumba ya Mungu.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36