bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 21
2 Chronicles 21
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 22 →
1
Yosafati akaja kulala na baba zake, akazikwa kwa baba zake mjini mwa Dawidi. Naye mwanawe Yoramu akawa mfalme mahali pake.
2
Yoramu alikuwa na ndugu, nao walikuwa wana wa Yosafati, ndio Azaria na Yehieli na Zakaria na Azaria na Mikaeli na Sefatia; hawa wote walikuwa wana wa Yosafati, mfalme wa Waisiraeli.
3
Hawa baba yao aliwapa vipaji vingi vya fedha na vya dhahabu na vya vitu vyenye kima, pamoja na miji yenye maboma katika nchi ya Yuda, lakini ufalme alimpa Yoramu, kwani huyu alikuwa mwanawe kwa kwanza.
4
Yoramu alipokwisha kujisimikia ufalme wa baba yake na kujipatia nguvu, akawaua ndugu zake wote kwa upanga, hata wakuu wengine wa Waisiraeli
5
Yoramu alikuwa mwenye miaka 32 alipoupata ufalme, akawa mfalme mle Yerusalemu miaka 8.
6
Akaendelea katika njia za wafalme wa Waisiraeli, kama wale wa mlango wa Ahabu walivyofanya, kwani binti Ahabu alikuwa mkewe; basi, naye akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana.
7
Lakini Bwana hakutaka kuuangamiza mlango wa Dawidi kwa ajili ya agano, alilolifanya na Dawidi, kwa kuwa alisema, ya kama atampa yeye na wanawe kuwa taa iwakayo siku zote.
8
Katika hizo siku zake Waedomu wakalivunja agano wakijitoa mikononi mwa Wayuda, wakajiwekea mfalme wa kuwatawala.
9
Ndipo, Yoramu alipoondoka kuwaendea pamoja na wakuu wake, akiyachukua magari yote. Ikawa, alipoondoka usiku, akawapiga Waedomu waliomzunguka yeye na wakuu wa magari.
10
Lakini Waedomu wakalivunja agano tena, wakajitoa mikononi mwa Wayuda mpaka siku hii ya leo. Siku zile ndipo, nao wa Libuna walipolivunja agano na kujitoa mkononi mwake, kwani alimwacha Bwana Mungu wa baba zake.
11
Yeye naye akafanya matambiko ya vilimani katika milima ya Yuda; ndivyo, alivyowazinisha wenyeji wa Yerusalemu, nao Wayuda akawaponza.
12
Ikafika kwake barua ya mfumbuaji Elia ya kwamba: Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa baba yako Dawidi anavyosema: kwa kuwa hukuendelea katika njia za baba yako Yosafati, wala katika njia za Asa, mfalme wa Wayuda,
13
ukaendelea katika njia za wafalme wa Waisiraeli, ukawazinisha Wayuda na wenyeji wa Yerusalemu, kama mlango wa Ahabu ulivyozini, ukawaua nao ndugu zako wa mlango wa baba yako waliokuwa wema kuliko wewe,
14
na umwone Bwana, akiwapiga pigo kubwa watu wako, hata wanao na wake zako na mali zako zote.
15
Lakini wewe utapatwa na magonjwa mengi kwa kuugua tumboni mwako, mpaka matumbo yako yatokee kwa kuugua hivyo siku nyingi na nyingi.
16
Kisha Bwana akaziamsha roho za Wafilisti na za Waarabu waliopakana na Wanubi, wamjie Yoramu.
17
Wakapanda katika nchi ya Yuda na kujipenyeza huko, wakaziteka mali zote zilizoonekana nyumbani mwa mfalme, hata watoto wake na wakeze, hakusalia mtoto kwake ila Yoahazi tu aliyekuwa mdogo katika wanawe wote.
18
Baada ya hayo Bwana akampiga tumboni mwake, apate ugonjwa usio na mganga wa kuuponya.
19
Ukawa wa siku nyingi na nyingi; matumbo yake yakatokea kwa huo ugonjwa, siku zilipokwisha kupita kama miaka miwili, akafa na kuumia vibaya. Kisha watu wake hawakumteketezea manukato, kama walivyowateketezea baba zake.
20
Alikuwa mwenye miaka 32 alipoupata ufalme, akawa mfalme mle Yerusalemu miaka 8, akajiendea pasipo kuombolezewa, wakamzika mjini mwa Dawidi, lakini hawakumzika makaburini kwa wafalme.
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 22 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36