bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 12
2 Chronicles 12
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 13 →
1
Ikawa, Rehabeamu alipokwisha kuushikiza ufalme wake na kuutia nguvu, akayaacha Maonyo ya Bwana, yeye na Waisiraeli wote pamoja naye.
2
Katika mwaka wa tano wa mfalme Rehabeamu akapanda Sisaki, mfalme wa Misri, kuujia Yerusalemu, kwani waliyavunja maagano ya Bwana.
3
Akaleta magari 1200 na wapanda farasi 60000 nao watu waliokuja naye toka Misri hawakuhesabika, Walibia na Wasuki na Wanubi.
4
Akaiteka miji yenye maboma iliyokuwako Uyuda, akafika hata Yerusalemu.
5
Ndipo, mfumbuaji Semaya alipokuja kwake mfalme Rehabeamu na kwa wakuu wa Wayuda waliokusanyika kwake Yerusalemu kwa ajili ya Sisaki, akawaambia: Hivi ndivyo, anavyosema Bwana: Ninyi mmeniacha, basi, mimi nami nimewaacha na kuwatia mkononi mwa Sisaki.
6
Ndipo, wakuu wa Isiraeli na mfalme walipojinyenyekeza, wakasema: Mwongofu ni Bwana!
7
Bwana alipoona, ya kuwa wamejinyenyekeza, neno la Bwana likamjia Semaya kwamba: Kwa kuwa wamejinyenyekeza, sitawaangamiza, ila punde kidogo nitawapatia uponya, makali yangu yasimwagiwe Yerusalemu na huyo Sisaki.
8
Lakini watakuwa watumishi wake, wapate kujua, utumishi wangu ulivyo, nao utumishi wa wafalme wa nchi nyingine ulivyo.
9
Sisaki, mfalme wa Misri, akapanda, akaujia Yerusalemu, akavichukua vilimbiko vya Nyumbani mwa Bwana navyo vilimbiko vya nyumbani mwa mfalme, vyote pia akavichukua, nazo ngao za dhahabu, Salomo alizozitengeneza, akazichukua.
10
Mahali pao mfalme Rehabeamu akatengeneza ngao za shaba, akazitia mikononi mwa wakuu wa wapiga mbio waliongoja pa kuingia nyumbani mwa mfalme, waziangalie.
11
Kila mara mfalme alipoingia Nyumbani mwa Bwana, hao walinzi wakaja, wakazichukua, kisha wakazirudisha chumbani mwao wapiga mbio.
12
Kwa kuwa amejinyenyekeza, makali ya Bwana yakageuka na kumwacha, asimwangamize na kummaliza kabisa, maana katika nchi ya Yuda yalikuwamo bado mambo mema.
13
Kisha mfalme Rehabeamu akapata nguvu tena mle Yerusalemu na kuushika ufalme. Alipoupata ufalme alikuwa mwenye miaka 41, akawa mfalme miaka 17 katika mji wa Yerusalemu, Bwana aliouchagua katika mashina yote ya Isiraeli, alikalishe Jina lake humo. Jina la mama yake ni Nama aliyekuwa Mwaamoni.
14
Akayafanya yaliyokuwa mabaya, kwani hakuuelekeza moyo wake, umtafute Bwana.
15
Mambo ya Rehabeamu, ya kwanza na ya mwisho, hayakuandikwa kwenye mambo ya mfumbuaji Semaya na ya mchunguzaji Ido, kama mambo ya wakale yalivyoandikwa? Lakini Rehabeamu na Yeroboamu walikuwa wakipigana vita siku zile zote.
16
Kisha Rehabeamu akaja kulala na baba zake, akazikwa mjini mwa Dawidi, naye mwanawe Abia akawa mfalme mahali pake.
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 13 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36