bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 28
2 Chronicles 28
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 27
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 29 →
1
Ahazi alikuwa mwenye miaka 20 alipoupata ufalme, akawa mfalme miaka 16 mle Yerusalemu; hakuyafanya yanyokayo machoni pake Bwana kama baba yake Dawidi,
2
ila akaendelea kuzishika njia za wafalme wa Waisiraeli, akatengeneza navyo vinyago vya Mabaali vilivyoyeyushwa.
3
Naye yeye akavukiza bondone kwa Bin-Hinomu, hata wanawe akawatumia kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa motoni akiyafuata hayo matapisho ya wamizimu, Bwana aliowafukuza mbele ya wana wa Isiraeli.
4
Akatambika na kuvukiza vilimani pa kutambikia napo pengine palipoinukia juu, hata chini ya kila mti uliokuwa wenye majani mengi.
5
Kwa hiyo Bwana akamtia mkononi mwa mfalme wa Ushami, wakampiga, wakateka kwake mateka mengi, wakawapeleka Damasko. Akatiwa hata mkononi mwa mfalme wa Waisiraeli aliyempiga pigo kubwa.
6
Kwani Peka, mwana wa Remalia, akaua katika nchi ya Yuda siku moja watu 120000, wote walikuwa wenye nguvu, kwa kuwa walimwacha Bwana Mungu wa baba zao.
7
Hata Zikiri, fundi wa vita wa Waefuraimu, akamwua Masea, mwana wa mfalme, na Azirikamu, mkuu wa nyumba ya mfalme, na Elkana aliyemfuata mfalme kwa ukuu.
8
Nao wana wa Isiraeli wakateka kwa ndugu zao 200000, wanawake na watoto wa kiume na wa kike na mali nyingi, walizozinyang'anya kwao; haya mateka wakayapeleka Samaria.
9
Huko kulikuwa na mfumbuaji wa Bwana, jina lake Odedi. Huyu akavitokea vile vikosi, vilipoingia Samaria, akawaambia: Tazameni! Kwa kuwa Bwana Mungu wa baba zenu amewakasirikia sana Wayuda, akawatia mikononi mwenu, lakini ninyi kwa machafuko mkamwaga kwao damu nyingi zilizofika hata mbinguni.
10
Sasa ninyi mwataka kuwanyenyekeza kwa nguvu hawa wana wa Yuda na wa Yerusalemu, wawe watumwa na vijakazi wenu. Lakini nanyi mliyojipatia kwake Bwana Mungu wenu sizo manza tu, mlizozikora?
11
Kwa hiyo nisikieni sasa, mrudishe kwao mateka, mliyoyateka kwa ndugu zenu! Kwani nanyi makali ya Bwana yawakayo moto yanawakalia.
12
Ndipo, walipoinuka waume waliokuwa wakuu wa wana wa Efuraimu, ndio Azaria, mwana wa Yohana, Berekia, mwana wa Mesilemoti, na Hizikia, mwana wa Salumu, na Amasa, mwana wa Hadilai; hawa wakawainukia waliotoka vitani,
13
wakawaambia: Msiyalete mateka yenu hapa! Kwani hivyo tutakora manza kwa Bwana, nanyi mnataka kweli kuyaongeza makosa yetu na manza zetu, kwani manza zetu ni nyingi, nayo makali yawakayo moto yanatukalia sisi Waisiraeli.
14
Ndipo, wapiga vita walipoyaacha mateka yao machoni pao wakuu napo pao mkutano wote pamoja na zile mali, walizozinyang'anya;
15
nao wale waume waliotajwa hapa juu majina yao wakainuka kuyachukua hayo mateka, kisha wote waliokuwa uchi wakawavika wakiwapa nguo na viatu na kuvitoa mlemle katika mapokonyo, kisha wakawapa vyakula na vya kunywa na mafuta ya kukipaka, nao wote waliojikwaakwaa wakawapandisha punda, wakawapeleka kwa ndugu zao Yeriko, ule mji wenye mitende, kisha wakarudi Samaria.
16
Siku zile mfalme Ahazi akatuma kwao wafalme wa Asuri, waje kumsaidia,
17
kwa maana Waedomu walikuja tena, wakawapiga, wakachukua mateka.
18
Nao Wafilisti wakaiingia miji ya nchi ya tambarare na miji ya kusini katika nchi ya Yuda na kunyang'anya mali, wakateka Beti-Semesi na Ayaloni na Gederoti na Soko na mitaa yake na Timuna na mitaa yake na Gimuzo na mitaa yake, wakakaa humo.
19
Kwani Bwana aliwanyenyekeza Wayuda kwa ajili ya Ahazi, mfalme wa Waisiraeli, kwani aliwalegeza Wayuda alipomvunjia Bwana maagano.
20
Ndipo, Tilgati-Pilneseri, mfalme wa Asuri, alipomjia, lakini akamsonga, hakumpatia nguvu.
21
Kwani Ahazi alichukua kwa nguvu yaliyokuwamo Nyumbani mwa Bwana namo nyumbani mwa mfalme nazo mali za wakuu, akampa mfalme wa Asuri, lakini hakusaidiwa naye.
22
Papo hapo, aliposongeka, yeye mfalme Ahazi akazidi kumvunjia Bwana maagano,
23
akaitumikia miungu ya Damasko iliyompiga, akasema: kwa kuwa miungu ya wafalme wa Ushami ndiyo iliyowasaidia, basi, nitaitambikia hiyohiyo, wanisadie; nayo ndiyo iliyomkwaza mwenyewe na Waisiraeli wote.
24
Kisha Ahazi akavikusanya vyombo vya Nyumba ya Mungu, akavivunjavunja hivyo vyombo vya Nyumba ya Mungu, akaifunga milango ya Nyumba ya Bwana, akajitengenezea pa kutambikia pembeni po pote mle Yerusalemu.
25
Hata kila mji mmoja wa Yuda akautengenezea vilima vya kuvukizia miungu mingine juu yao; ndivyo, alivyomkasirisha Bwana Mungu wa baba zake.
26
Mambo yake mengine na njia zake zote, za kwanza na za mwisho, tunaziona, zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Wayuda na wa Waisiraeli.
27
Kisha Ahazi akaja kulala na baba zake, wakamzika katika mji wa Yerusalemu, kwani hawakumpeleka penye makaburi ya wafalme wa Waisraeli. Naye mwanawe Hizikia akawa mfalme mahali pake.
← Chapter 27
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 29 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36