bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 8
2 Chronicles 8
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 9 →
1
Ile miaka ishirini, ambayo Salomo aliijenga Nyumba ya Bwana na nyumba yake, ilipokwisha,
2
ndipo, Salomo alipoijenga ile miji, Huramu aliyompa Salomo, akakalisha humo wana wa Isiraeli.
3
Kisha Salomo akaenda Hamati-Soba, akauchukua.
4
Akajenga Tadimori ulioko nyikani, hata miji yote yenye vilimbiko, aliyoijenga kule Hamati.
5
Kisha akajenga Beti-Horoni wa juu na Beti-Horoni wa chini kuwa miji yenye maboma iliyokuwa na kuta na malango na makomeo.
6
Ndivyo, alivyojenga hata Balati na miji yote yenye vilimbiko, Salomo aliyokuwa nayo, hata miji yote ya magari na miji ya farasi na majengo yote yaliyompendeza Salomo, aliyotaka kuyajenga kwa mapenzi yake mle Yerusalemu nako huko Libanoni na katika nchi yo yote ya ufalme wake.
7
Watu aliowatumia, ndio wote waliosalia na Wahiti na wa Waamori na wa Waperizi na wa Wahiwi na wa Wayebusi wasiokuwa wa Waisiraeli;
8
wana wao wale waliosalia na kuachwa na wenzao katika nchi hii, kwa kuwa wana wa Isiraeli hawakuwamaliza, basi, hao wote Salomo akawafanyisha kazi za utumwa hata siku hii ya leo.
9
Lakini wana wa Isiraeli Salomo hakuwataka kuwa watumwa wa kumfanyizia kazi, kwani hawa walikuwa wapiga vita na wakuu wa thelathini na wakuu wa magari yake na wapanda farasi wake.
10
Nao wakuu wa mfalme Salomo waliowekwa kusimamia kazi walikuwa 250, ndio waliowatawala watu wa kazi,
11
Binti Farao Salomo akamtoa mjini mwa Dawidi, akampeleka kukaa katika nyumba, aliyomjengea, kwani alisema: Mwanamke asikae kwangu nyumbani mwa Dawidi, mfalme wa Waisiraeli, kwa kuwa ni takatifu, kwani Sanduku la Bwana liliingia mumo humo.
12
Tangu hapo ndipo, Salomo alipomtolea Bwana ng'ombe za tambiko za kuteketezwa hapo mezani pa kumtambikia Bwana, alipopajenga mbele ya ukumbi;
13
akatoa ng'ombe za tambiko zipasazo kila siku moja, kama Mose alivyoagiza: za mapumziko, za miandamo ya mwezi, za sikukuu zilizo tatu za kila mwaka: sikukuu ya Mikate isiyochachwa, sikukuu ya Majuma na sikukuu ya Vibanda.
14
Kama baba yake Dawidi alivyoviagiza, akayaweka mafungu ya watambikaji ya kuzifanya kazi zao nayo ya Walawi kwa zamu zao: wa kuimba mashangilio nao wa kuwatumikia watambikaji, kama ilivyopasa kila siku moja; akawaweka nao walinda malango kwa mafungu yao, walingoje kila lango moja, kama Dawidi aliyekuwa mtu wa Mungu alivyoviagiza.
15
Hawakutangua agizo la mfalme, alilowaagiza la watambikaji na la Walawi kwa ajili ya mambo yote, hata kwa ajili ya vilimbiko.
16
Kwa hiyo kazi zote za Salomo zikaendelea vema tangu siku ile, misingi ya Nyumba ya Bwana ilipowekwa, hata siku hiyo, Nyumba yote nzima ya Bwana ilipomalizika.
17
Kisha Salomo akaenda Esioni-Geberi na Eloti huko pwani kwenye bahari iliyoko katika nchi ya Edomu.
18
Huramu akatuma kwake vyombo vilivyopelekwa na watumishi wake pamoja na watumishi walioyajua mambo ya baharini; wakaenda Ofiri pamoja na watumishi wake Salomo, wakachukua huko vipande vya dhahabu 450, ndio frasila 1350, wakampelekea mfalme salomo.
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36