bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 25
2 Chronicles 25
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 24
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 26 →
1
Amasia alikuwa mwenye miaka 25 alipoupata ufalme, akawa mfalme miaka 29 mle Yerusalemu. Jina la mama yake ni Yoadani wa Yerusalemu.
2
Akayafanya yanyokayo machoni pake Bwana, lakini hakuyafanya kwa moyo wote mzima.
3
Ikawa, alipoushupaza ufalme wake, akawaua watumishi wake waliomwua baba yake mfalme.
4
Lakini wana wao hakuwaua, kwa kuwa katika Maonyo katika kitabu cha Mose imeandikwa, ya kuwa Bwana ameagiza kwamba: Baba wasife kwa ajili ya wana, wala wana wasife kwa ajili ya baba, ila kila mtu sharti afe kwa kosa lake yeye.
5
Kisha Amasia akawakusanya Wayuda, akawapanga kwa milango na kwa wakuu wa maelfu na kwa wakuu wa mamia wote pia waliokuwa Wayuda na Wabenyamini. Alipowakagua walio wenye miaka ishirini na zaidi akapata watu 300000 waliochaguliwa kwenda vitani waliojua kushika mikuki na ngao.
6
Akajipatia nako kwa Waisiraeli watu wa mshahara 100000 waliokuwa mafundi wa vita wenye nguvu, akawalipa vipande mia vya fedha, ndio shilingi milioni na 200000.
7
Ndipo, mtu wa Mungu alipomjia, akamwambia: Mfalme, vikosi vya Waisiraeli visiende na wewe! Kwani Bwana hawi nao Waisiraeli, maana wote ni wana wa Efuraimu.
8
Kama ni kwenda, vifanye wewe, ukijishupaza, upate kupigana! Kama sivyo, Mungu atakukwaza mbele ya adui, kwani Mungu anazo nguvu za kusaidia na za kukwaza.
9
Amasia akamwuliza huyu mtu wa Mungu: Tena nivifanyeje vile vipande mia vya fedha, nilivyowapa wao wa kikosi cha Waisiraeli? Ndipo, huyu mtu wa Mungu alipomwambia: Bwana anaweza kukupa zaidi ya hivyo.
10
Kisha Amasia akakitenga kile kikosi kilichokuja kwake toka nchi ya Efuraimu, waende kwao; nao wakawakasirikia sana Wayuda, wakarudi kwao wenye makali yaliyowaka moto.
11
Kisha Amasia akajishupaza, akawaongoza watu wake kwenda katika Bonde la Chumvi, akawapiga wana wa Seiri 10000,
12
wengine 10000 wana wa Yuda wakawateka, wa hai, wakawapeleka mwambani juu, wakawakumba toka hapo juu mwambani; ndipo, wote pia walipopondeka.
13
Lakini watu wa kile kikosi, Amasia alichokirudisha, wasiende naye kupigana, waliingia miji ya Yuda toka Samaria hata Beti-Horoni, na kunyang'anya mali, wakapiga humo watu 3000, wakachukua mali nyingi, walizozinyang'anya.
14
Amasia aliporudi akiisha kuwashinda Waedomu akaileta miungu ya wana wa Seiri, akaiweka kuwa miungu yake, akaiangukia na kuivukizia.
15
Kwa hiyo Bwana akamkasirikia Amasia sana, akatuma mfumbuaji kwake, akamwambia: Mbona unaifuatafuata miungu ya watu hao, isiyowaponya watu wao mikononi mwako?
16
Alipomwambia hayo, akamwuliza: Tumekuweka kula njama na mfalme? Yaache! Unatakiaje, wakupige? Ndipo, mfumbuaji alipoacha akisema: Ninajua sasa, ya kuwa Mungu anataka kukuangamiza, kwa sababu umefanya hivyo, usilisikie shauri langu.
17
Kisha Amasia, mfalme wa Yuda, akapiga shauri, akatuma kwa Yoasi, mwana wa Yoahazi, mwana wa Yehu, mfalme wa Waisiraeli, kumwambia: Njoo, tuonane uso kwa uso!
18
Naye Yoasi, mfalme wa Waisiraeli, akatuma kwa Amasia, mfalme wa Wayuda, kumwambia: Kingugi kilichoko Libanoni kilituma kwa mwangati ulioko Libanoni kwamba: Mpe mwanangu mtoto wako wa kike, awe mkewe! Ndipo, nyama wa porini wa huko Libanoni alipopita, akakikanyaga kile kingugi na kukiponda.
19
Unasema, umewapiga Waedomu; kwa hiyo moyo wako unakukuza, ujitutumue. Sasa kaa nyumbani mwako! Mbona unataka kujitia katika vita vibaya, uanguke wewe na Wayuda pamoja na wewe?
20
Lakini Amasia hakusikia, kwani jambo hilo limetoka kwa Mungu, awatie mikononi mwa wengine, kwa kuwa waliifuatafuata miungu ya Waedomu.
21
Basi, Yoasi, mfalme wa Waisiraeli, akapanda, wakaonana uso kwa uso, yeye na Amasia, mfalme wa Wayuda, huko Beti-Semesi katika nchi ya Wayuda.
22
Wayuda wakashindwa na Waisiraeli, wakakimbia kila mtu hemani kwake.
23
Naye Yoasi, mfalme wa Waisiraeli, akamkamata Amasia, mfalme wa Yuda, aliyekuwa mwana wa Yoasi, mwana wa Yoahazi, kule Beti-Semesi, akampeleka Yerusalemu, akalivunja boma la Yerusalemu toka lango la Efuraimu hata lango la pembeni, ndio mikono 400.
24
Akachukua dhahabu na fedha zote, navyo vyombo vyote vilivyopatikana Nyumbani mwa Mungu kwa Obedi-Edomu navyo vilimbiko vya nyumbani mwa mfalme nao watu, aliowataka kuwa kole, kisha akarudi Samaria.
25
Ikawa, Yoasi, mwana wa Yoahazi, mfalme wa Isiraeli, alipokwisha kufa, Amasia, mwana wa Yoasi, mfalme wa Wayuda, akawapo tena miaka 15.
26
Mambo mengine ya Amasia, ya mwanzo na ya mwisho, hatuyaoni, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Wayuda na wa Waisiraeli?
27
Tangu hapo, Amasia alipoacha kumfuata Bwana, walikuwako watu huko Yerusalemu waliomlia njama ya kumwua; kwa hiyo akakimbilia Lakisi, lakini wale wakatuma watu kumfuata lakisi, nao wakamwua huko.
28
Wakamchukua kwa farasi, wakamzika kwa baba zake mjini mwa Yuda.
← Chapter 24
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 26 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36