bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 32
2 Chronicles 32
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 31
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 33 →
1
Hayo yalipokwisha kufanyika kwa welekevu, akaja Saniheribu, mfalme wa Asuri; akaingia katika nchi ya Yuda, akapiga makambi kwenye miji yenye maboma, akataka kujipenyeza humo, iwe yake.
2
Hizikia alipoona, ya kuwa Saniheribu amekuja na kuuelekeza uso wake kuja kupiga vita Yerusalemu,
3
akafanya shauri na wakuu wake na mafundi wake wa vita kuyaziba maji ya chemchemi zilizoko nje ya mji, nao wakamsaidia.
4
Wakakusanyika watu wengi, wakaziziba chemchemi zote, hata kijito kilichopita katikati ya nchi hiyo wakisema: Mbona tuache, wafalme wa Asuri wakifika waone maji mengi?
5
Akakaza kuutengeneza ukuta wote wa boma na kuujenga tena hapo, ulipobomoka, hata minara akaipandisha kwenda juu zaidi, nao ukuta wa pili wa nje akaujenga tena, hata ngome ya mji wa Dawidi akaitia nguvu, akatengeneza mata na ngao nyingi.
6
Nao watu akawawekea wakuu wa vita, akawakusanya kwake uwanjani penye lango la mji, akawashikiza mioyo akiwaambia:
7
Jipeni mioyo, mpate nguvu! Msiogope, wala msiingiwe na vituko mkimwona mfalme wa Asuri nao wale watu wengi mno, alio nao wote! Kwani walio upande wetu ndio wengi kuliko wao walio upande wake.
8
Yeye anayo mikono yenye nyama, lakini sisi tunaye Bwana Mungu wetu kuwa msaada wetu kwa kutupigania mapigano yetu. Nao watu wakashikizwa na haya maneno ya Hizikia, mfalme wa Yuda.
9
Baada ya hayo Saniheribu, mfalme wa Asuri, alipokuwa Lakisi pamoja na utukufu wake wote akatuma watumishi wake kwenda Yerusalemu kwa Hizikia, mfalme wa Wayuda, na kwa Wayuda wote waliokuwamo Yerusalemu kuwaambia:
10
Hivi ndivyo, anavyosema Saniheribu, mfalme wa Asuri: Ninyi mnaegemea nini mkikaa ngomeni Yerusalemu na kusongwa?
11
Je? Siye Hizikia anayewaponza na kuwatoa, mfe kwa njaa na kwa kiu akiwaambia: Bwana Mungu wetu atatuponya mkononi mwa mfalme wa Asuri?
12
Huyu Hizikia siye aliyewakataza watu kumtambikia pake pa kutambikia vilimani napo penye meza zake za kutambikia akiwaambia Wayuda na Wayerusalemu kwamba: Sharti mmwangukie mbele ya meza moja tu ya kumtambikia na kumvukizia hapo tu?
13
Hamyajui, mimi na baba zangu tuliyoyafanyia makabila yote ya nchi hizo? Je? Miungu yao mataifa ya nchi hizi iliweza kweli kuziponya nchi zao mikononi mwangu?
14
Katika miungu yote ya haya mataifa, baba zangu waliyoyatia mwiko wa kuwapo, ulikuwa upi ulioweza kuwaponya watu wake mkononi mwangu? Naye Mungu wenu atawezaje kuwaponya mkononi mwangu?
15
Sasa Hizikia asiwadanganye na kuwaponza ninyi kwa maneno kama hayo! Msimtegemee! Kwani hakuna mungu wo wote wa taifa au ufalme wo wote ulioweza kuwaponya watu wake mkononi mwangu wala mikononi mwa baba zangu. Sembuse Mungu wenu atawezaje kuwaponya mkononi mwangu?
16
Yako na mengine, watumishi wake waliyoyasema ya kumkataa Bwana Mungu na mtumishi wake Hizikia.
17
Akaandika nazo barua za kumfyoza Bwana Mungu wa Isiraeli, akisema humo kwamba: Kama miungu ya mataifa ya nchi hizi isivyoweza kuwaponya watu wao mkononi mwangu, vivyo hivyo naye Mungu wa Hizikia hataweza kuwaponya watu wake mkononi mwangu.
18
Nao wa Yerusalemu waliokuwa ukutani juu wakawaambia haya Kiyuda na kuzipaza sana sauti zao, wawaogopeshe na kuwastusha, wapate kuuteka mji huu.
19
Mambo ya Mungu wa Yerusalemu wakayawazia kuwa kama mambo ya miungu ya makabila mengine ya nchi hii iliyokuwa kazi za mikono ya watu tu.
20
Ndipo, mfalme Hizikia na mfumbuaji Yesaya, mwana wa Amosi, walipoomba kwa ajili ya hayo na kumlilia Alioko mbinguni.
21
Bwana akatuma malaika wake, akaangamiza katika makambi ya mfalme wa Asuri mafundi wa vita wote waliokuwa wenye nguvu na wenye amri na wakuu, naye yeye hakuwa na budi kurudi kwao na kuuinamisha uso chini kwa soni. Alipoingia nyumbani mwa mungu wake, ndipo, wanawe wengine waliozaliwa naye mwenyewe walipomwua kwa upanga.
22
Ndivyo, Bwana alivyomwokoa Hizikia na wenyeji wa Yerusalemu mkononi mwa Saniheribu, mfalme wa Wasuri, namo mikononi mwao wote wengine akiwalinda pande zote.
23
Watu wengi wakamtolea Bwana vipaji na kuvipeleka Yerusalemu, naye Hizikia, mfalme wa Wayuda, wakampa matunzo, naye tangu hapo akatukuka sana machoni pao wamizimu wote.
24
Siku hizo Hizikia akaugua, kufa kukamjia karibu sana; alipomlalamikia Bwana, huyu akasema naye na kumtolea kielekezo.
25
Lakini Hizikia hakuyarudisha hayo mema aliyofanyiziwa, kwa kuwa moyo wake ulijikuza. Kwa hiyo makali ya Bwana yakaja kumkalia yeye, hata Wayuda na Wayerusalemu.
26
Lakini Hizikia kwa hivyo, moyo wake ulivyojikuza, akajinyenyekeza tena yeye pamoja na wenyeji wa Yerusalemu; kwa sababu hii makali ya Bwana hayakuwatokea siku za Hizikia.
27
Hizikia akawa mwenye mali na macheo mengi, akajipatia vilimbiko vya fedha na vya dhahabu na vya vito vyenye kima na vya manukato na vya ngao na vya vyombo vyo vyote, alivyovitamani,
28
hata mawekeo ya mazao ya ngano na ya mvinyo mbichi na ya mafuta, hata mabanda ya nyama wote wa kufuga na makundi mazizini.
29
Akajenga hata miji, kwani alikuwa na mbuzi na kondoo na ng'ombe wengi, kwani Mungu alimpa kupata mali nyingi sana.
30
Naye Hizikia ndiye aliyeliziba tokeo la juu la maji ya kijito cha Gihoni na kuyapeleka moja kwa moja, yaushukie mji wa Dawidi upande wa machweoni kwa jua. Ndivyo, Hizikia alivyofanikiwa katika kazi zote.
31
Hapo tu, wakuu wa Babeli walipotuma wasemaji kwake wa kuuliza maana ya kielekezo kilichofanyika katika nchi hii, Mungu alimwacha, amjaribu, ayajue yote yaliyokuwa moyoni mwake.
32
Mambo mengine ya Hizikia nayo matendo ya upole wake tunayaona, yameandikwa katika maono ya mfumbuaji Yesaya, mwana wa Amosi, na katika kitabu cha wafalme wa Wayuda na wa Waisiraeli.
33
Hizikia alipokwenda kulala na baba zake, wakamzika pa kupandia penye makaburi ya wana wa Dawidi; Wayuda wote na wenyeji wa Yerusalemu wakamheshimu sana, alipokufa. Naye mwanawe Manase akawa mfalme mahali pake.
← Chapter 31
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 33 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36