bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 14
2 Chronicles 14
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 15 →
1
Abia akaja kulala na baba zake, wakamzika mjini mwa Dawidi, naye mwanawe Asa akawa mfalme mahali pake. Siku zake nchi ikapata kutulia miaka kumi.
2
Asa akayafanya mema yanyokayo machoni pake Bwana Mungu wake.
3
Akapaondoa pa kutambikia miungu migeni na matambiko ya vilimani, akazivunja nazo nguzo za mawe za kutambikia, nayo miti ya Ashera akaikatakata.
4
Akawaambia Wayuda, wamtafute Bwana Mungu wa baba zao, wayafanye Maonyo na maagizo yake.
5
Katika miji yote ya Wayuda akayaondoa matambiko ya vilimani na mifano ya jua; kwa hivyo, alivyoushika ufalme, nchi ikatulia.
6
Akajenga miji yenye maboma katika nchi ya Yuda, kwani nchi ilikuwa imetulia, hakuwa na vita vyo vyote katika miaka hiyo, kwani Bwana alimpatia utulivu.
7
Kwa hiyo aliwaambia Wayuda: Na tuijenge miji hii na kuizungushia maboma na minara na kutia humo malango yenye makomeo; nchi hii ingaliko wazi mbele yetu, kwani tumemtafuta Bwana Mungu wetu; naye kwa hivyo, tulivyomtafuta, ametupatia kutulia pande zote. Basi, wakaijenga, wakafanikiwa.
8
Asa akawa na vikosi vya watu walioshika ngao na mikuki, Wayuda 300000 na Wabenyamini walioshika ngao ndogo, waliojua hata kupinda pindi 280000; hawa wote walikuwa mafundi wa vita wenye nguvu.
9
Ndipo, alipotokea kwao Mnubi Zera mwenye vikosi vya watu milioni na magari 340, akaja mpaka Maresa.
10
Asa akamtokea, wakajipanga kupigana katika bonde la Sefata karibu ya Maresa.
11
Asa akamlalamikia Bwana Mungu wake akisema: Bwana, hakuna mwingine, usipokuwa wewe, anayeweza kumsaidia mwenye watu wengi naye asiye na nguvu; tusaidie, Bwana Mungu wetu! Kwani tumekuegemea wewe, tukaja kwa Jina lako kupigana na uvumi huu wa watu; Bwana, Mungu wetu ndiwe wewe! Hapa pasiwe na mtu atakayekushinda nguvu!
12
Ndipo, Bwana alipowapiga Wanubi mbele ya Asa na mbele ya Wayuda, Wanubi wakakimbia.
13
Asa akawakimbiza pamoja na hao watu, aliokuwa nao, mpaka Gerari; kwa Wanubi watu wakauawa kabisa, hakusalia kwao waliopona, kwani walivunjwa mbele ya Bwana na mbele ya vikosi vyake. Kisha Wayuda wakachukua mateka mengi sana.
14
Wakaipiga miji yote pia iliyokuwa pande zote za Gerari, kwani tisho la Bwana lilikuwa limewaguia, wakazipokonya mali zote zilizokuwa katika miji hiyo yote, nazo mali za kupokonya zikawamo nyingi sana.
15
Nayo mahema ya makundi wakayavunja, wakateka mbuzi na kondoo wengi, hata ngamia, kisha wakarudi Yerusalemu.
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36