bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 30
2 Chronicles 30
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 31 →
1
Hizikia akatuma kwa Waisiraeli na kwa Wayuda wote, nao Waefuraimu na Wamanase akawaandikia barua, waje Yerusalemu Nyumbani mwa Bwana Mungu wa Isiraeli kula sikukuu ya Pasaka ya Bwana Mungu wa Isiraeli.
2
Mfalme na wakuu wake nao mkutano wote wa watu wakafanya shauri huko Yerusalemu kula sikukuu ya Pasaka katika mwezi wa pili.
3
Kwani hawakuweza kuila siku zile, kwa kuwa watambikaji wa kutosha hawajajieua, nao watu hawakukusanyika Yerusalemu.
4
Shauri hili likanyoka machoni pake mfalme napo pao mkutano wote.
5
Wakaagiza kupiga mbiu kwa Waisiraeli wote toka Beri-Seba hata Dani, watu waje kula sikukuu ya Pasaka ya Bwana Mungu wa Isiraeli mle Yerusalemu, kwani tangu siku nyingi hawakuila, kama ilivyoandikwa.
6
Wajumbe wapigao mbio wakaenda na barua, walizopewa na mfalme na wakuu wake, katika nchi zote za Waisiraeli na za Wayuda, wakasema, kama walivyoagizwa na mfalme: Wana wa Isiraeli rudini kwake Bwana, Mungu wa Aburahamu na wa Isaka na wa Isiraeli! Ndipo, atakaporudi kwao waliosalia kwenu kwa kupona mikononi mwa wafalme wa Asuri.
7
Msiwe kama baba zenu na ndugu zenu walioyavunja maagano ya Bwana Mungu wa baba zao, akawatoa, waangamizwe, kama mnavyoona nanyi.
8
Sasa msizishupaze kosi zenu kama baba zenu! Ila mpeni Bwana mikono mkija Patakatifu pake, alipopatakasa kuwa pake kale na kale! Kamtumikieni Bwana Mungu wenu! Ndipo, makali yake yawakayo moto yatakapoondoka kwenu.
9
Kwani mkirudi kwake Bwana, ndugu zenu na wana wenu watahurumiwa nao waliowateka na kuwahamisha, wapate kurudi katika nchi hii, kwani Bwana Mungu wenu ni mwenye utu na huruma, hatauondoa uso kwenu, mkirudi kwake.
10
Basi, hao wajumbe wapigao mbio wakaenda kuingia mji kwa mji katika nchi ya Efuraimu na ya Manase hata Zebuluni, lakini watu wakawacheka na kuwafyoza.
11
Watu wa Aseri tu na wa Manase na wa Zebuluni wakajinyenyekeza, wakaja Yerusalemu.
12
Hata katika nchi ya Yuda mkono wa Mungu ukawako, ukawapa kuwa wenye moyo mmoja wa kulifanya agizo la mfalme na la wakuu, Bwana alilowaambia.
13
Katika mwezi wa pili wakakusanyika Yerusalemu watu wengi kuila sikukuu ya Mikate isiyochachwa, ukawa mkutano mkubwa sana.
14
Wakainuka, wakapaondoa pote pa kutambikia palipokuwamo Yerusalemu, navyo vivukizo vyote wakaviondoa, wakavitupa katika mto wa Kidoroni.
15
Kisha wakachinja wana kondoo wa Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili, kwani watambikaji na Walawi walijieua kwa kuona soni, wakapeleka ng'ombe za tambiko Nyumbani mwa Bwana.
16
Wakasimama mahali pao palipowapasa, kama Maonyo ya Mose aliyekuwa mtu wa Mungu yalivyoagiza. Hao watambikaji wakazinyunyiza damu, walizozipokea mikononi mwa Walawi.
17
Kwani katika huo mkutano walikuwako wengi wasiojieua; kwa sababu hii Walawi wakawachinjia wote wasiotakata wana kondoo wa Pasaka, wawatakase kuwa wa Bwana.
18
Kwani watu wengi sana wa Efuraimu na wa Manase na wa Isakari na wa Zebuluni hawakujitakasa, kwani hawakuila kondoo ya Pasaka, kama ilivyoandikwa. Lakini Hizikia aliwaombea kwamba: Bwana aliye mwema na amwondolee makosa
19
kila mtu aliyeuelekeza moyo wake kumtafuta Mungu Bwana aliye Mungu wa baba zake, ingawa hakuupata utakaso upapasao Patakatifu.
20
Bwana akamsikia Hizikia, akawaponya hao watu.
21
Ndivyo, wana wa Isiraeli waliokuwamo Yerusalemu walivyoila sikukuu ya Mikate isiyochachwa siku saba kwa furaha kubwa, nao Walawi na watambikaji wakamshangilia Bwana siku kwa siku na kumpigia Bwana vyombo vyenye sauti za nguvu.
22
Naye Hizikia akawaambia Walawi wote waliokuwa wenye akili njema katika kazi ya Bwana maneno yaliyoingia mioyoni mwao, wakaila sikukuu hii ya ushahidi siku saba, wakitoa vipaji vya tambiko vya shukrani, wamshukuru Bwana Mungu wa baba zao.
23
Kisha mkutano wote ukafanya shauri kuendelea siku saba tena, wakala sikukuu tena siku saba kwa furaha.
24
Kwani Hizikia, mfalme wa Wayuda, aliutolea huo mkutano madume ya ng'ombe 1000 na mbuzi na kondoo 7000, nao wakuu waliutolea mkutano madume ya ng'ombe 1000 na mbuzi na kondoo 7000; nao watambikaji walijieua wengi.
25
Wakafurahi watu wote wa huo mkutano wa Wayuda pamoja na watambikaji na Walawi na mkutano wao wote waliotoka kwa Waisiraeli nao wageni waliotoka katika nchi ya Waisiraeli nao waliokaa katika nchi ya Wayuda.
26
Ikawa furaha kubwa mle Yerusalemu, kwani tangu siku za Salomo, mwana wa Dawidi, mfalme wa Waisiraeli, haya kuwamo mle Yerusalemu mambo kama hayo.
27
Mwisho watambikaji na Walawi wakainuka, wakawabariki watu; sauti zao zikasikiwa, nayo maombo yao yakafika mbinguni kwenye Kao lake takatifu.
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 31 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36