bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 23
2 Chronicles 23
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 24 →
1
Katika mwaka wa saba Yoyada akajishupaza, akawachukua wakuu wa mamia, Azaria, mwana wa Yerohamu, na Isimaeli, mwana wa Yohana, na Azaria, mwana wa Obedi, na Masea, mwana wa Adaya, na Elisafati, mwana wa Zikiri, akafanya maagano nao.
2
Wakazunguka katika nchi ya Yuda, wakawakusanya Walawi na kuwatoa katika miji yote ya Yuda pamoja na wakuu wa milango ya Isiraeli, wakaja Yerusalemu.
3
Huu mkutano wote ukafanya agano na mfalme Nyumbani mwa Mungu, Yoyada akawaambia: Mtazameni huyu mwana wa mfalme! Atakuwa mfalme, kama Bwana alivyosema kwa ajili ya wana wa Dawidi.
4
Hili ndilo neno, mtakalolifanya: fungu lenu la tatu, ninyi watambikaji na Walawi, watakaoingia kazi siku ya mapumziko, sharti walinde malangoni;
5
fungu jingine la tatu sharti walinde nyumbani mwa mfalme, fungu jingine la tatu walinde langoni penye msingi. Kisha watu wote waje nyuani penye Nyumba ya Bwana.
6
Lakini Nyumbani mwa Bwana mtu asiingie, wasipokuwa watambikaji nao Walawi wanaotumikia. Hao wataingia, kwani ndio watakatifu. Nao watu wote sharti walinde ulinzi wa Bwana,
7
nao Walawi sharti wamzunguke mfalme pande zote, kila mtu akiyashika mata yake, kisha kila atakayeingia Nyumbani mwa Bwana na auawe! Hivyo sharti mwe na mfalme, akiingia, hata akitoka.
8
Walawi na Wayuda wote wakayafanya yote, kama mtambikaji Yoyada alivyowaagiza, kila mtu akawachukua wate wake walioingia kazi siku ya mapumziko nao waliotoka kazi siku ya mapumziko, kwani mtambikaji Yoyada hakuwapa ruhusa waliozimaliza zamu.
9
Kisha mtambikaji Yoyada akawapa wakuu wa mamia mikuki na ngao ndogo na kubwa za mfalme Dawidi zilizokuwa Nyumbani mwa Mungu.
10
Akawapanga watu wote, kila mtu na mkuki wake mkononi mwake kuanzia upande wa kuume wa Nyumba kuufikia upande wa kushoto wa Nyumba, kuifikia meza ya kutambikia na tena kuifikia Nyumba yenyewe, wamzunguke mfalme pande zote.
11
Kisha wakamtoa mwana wa mfalme, wakamvika kilemba cha kifalme, wakampa nacho kizingo cha Ushahidi, wakamfanya kuwa mfalme, Yoyada na wanawe wakimpaka mafuta na kusema: pongezi, mfalme!
12
Atalia alipozisikia sauti za watu waliomkimbilia mfalme na kumshangilia, akaja naye hapo, watu walipo, penye Nyumba ya Bwana.
13
Alipotazama, akamwona mfalme, akisimama katika ulingo wake pa kuingilia, nao wakuu na wapiga matarumbeta wakisimama kwake mfalme, nao watu wote wa nchi yao wakawa wenye furaha na kupiga matarumbeta, nao waimbaji wakavipiga vyombo vya kuimbia, wakawaongoza watu kushangilia. Ndipo, Atalia alipoyararua mavazi yake na kupiga kelele kwamba: Mmedanganyika! Mmedanganyika!
14
Ndipo, mtambikaji Yoyada alipowatoa wakuu wa mamia waliovisimamia vikosi, akawaambia: Mtoeni hapa penye mipango ya watu! Naye atakayemfuata na auawe kwa upanga! Kwani mtambikaji alisema: Msimwue Nyumbani mwa Bwana!
15
Wakamkamata kwa mikono, naye alipofika pa kuliingilia lango la farasi penye nyumba ya mfalme, wakamwua huko.
16
Kisha Yoyada akafanya agano, yeye na watu wote na mfalme, wawe ukoo wake Bwana.
17
Ndipo, watu wote walipoiingia nyumba ya Baali, wakaibomoa; nazo meza za kumtambikia na vinyago vyake wakavivunjavunja kabisa, naye Matani, mtambikaji wa Baali, wakamwua mbele ya meza za kutambikia.
18
Kisha Yoyada akaweka watambikaji na Walawi kuwa wakaguzi wa Nyumba ya Bwana, kwani Dawidi aliwapatia hao kazi ya kuiangalia Nyumba ya Bwana, wamteketezee Bwana ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, kama ilivyoandikwa katika Maonyo ya Mose, pamoja na kuimba nyimbo za furaha, kama Dawidi alivyowaongoza.
19
Akaweka nao walinda malango ya Nyumba ya Bwana, mtu asiingie akiwa mwenye uchafu kwa jambo lo lote.
20
Kisha akawachukua wakuu wa mamia na watukufu na watawalaji wa watu nao watu wote wa nchi hii, akamtoa mfalme Nyumbani mwa Bwana, wakaingia nyumbani mwa mfalme na kupita katikati katika lango la juu, wakamketisha mfalme katika kiti cha kifalme.
21
Wakafurahi watu wote wa nchi hii, nao mji ukatulia. Lakini Atalia walikuwa wamemwua kwa upanga.
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 24 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36