bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 22
2 Chronicles 22
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 23 →
1
Wenyeji wa Yerusalemu wakampa mwanawe mdogo Ahazia ufalme mahali pake, kwani wakubwa wake wote waliuawa na kikosi kilichokuja na Waarabu kambini. Ndivyo, Ahazia, mwana wa Yoramu, alivyopata kuwa mfalme wa Wayuda.
2
Alikuwa mwenye miaka 22, alipoupata ufalme, akawa mfalme mle Yerusalemu mwaka mmoja. Jina la mama yake ni Atalia, binti Omuri.
3
Yeye naye akaendelea katika njia za mlango wa Ahabu, kwani mama yake ndiye aliyemwongoza kuyafanya yaliyo maovu.
4
Akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana kama mlango wa Ahabu, kwani hao ndio waliomwongoza, baba yake alipokwisha kufa, wampatie mwangamizo.
5
Kwa kuongozwa nao akaja kwenda na Yoramu, mwana wa Ahabu, mfalme wa Waisiraeli, kumpelekea Hazaeli, mfalme wa Ushami, vita huko Ramoti wa Gileadi. Washami walipomwumiza Yoramu,
6
akarudi Izireeli, apate watakao mponya vidonda, walivyompiga kule Rama, alipopigana na Hazaeli, mfalme wa Ushami. Ndipo, Azaria, mwana wa Yoramu, mfalme wa Wayuda, aliposhuka kumtazama Yoramu, mwana wa Ahabu, huko Izireeli, kwani ndiko, alikougulia.
7
Hili lilitoka kwake Mungu kuwa mwangamizo wake Ahazia, alipofika kwa Yoramu: kwani alipokwisha kufika akatoka pamoja na Yoramu kwenda kupigana na Yehu, mwana wa Nimusi, Bwana aliyempaka mafuta, aung'oe mlango wa Ahabu.
8
Ikawa, Yehu alipoupatiliza mlango wa Ahabu, akawaona nao wakuu wa Wayuda na wana wa ndugu zake Ahazia waliomtumikia Ahazia, akawaua.
9
Alipoagiza kumtafuta Ahazia, wakamkamatia Samaria, alikojificha, wakampeleka kwa Yehu, wakamwua, wakamzika, kwani walisema: Yeye ni mwana wa Yosafati aliyemtafuta Bwana kwa moyo wake wote. Lakini katika mlango wa Ahazia hakuwako mwenye nguvu aliyeweza kuwa mfalme.
10
Atalia, mamake Ahazia, alipoona, ya kuwa mwanawe amekufa, akaondoka, akawaua wazao wote wa kifalme wa mlango wa Yuda.
11
Lakini Yosabati, binti mfalme, akamchukua Yoasi, mwana wa Ahazia, akamwiba katikati ya wana wa mfalme waliokwenda kuuawa, akamweka pamoja na mnyonyeshaji wake katika chumba cha kulalia. Ndivyo, Yosabati, binti mfalme Yoramu, mkewe mtambikaji Yoyada, aliyekuwa umbu lake Ahazia, alivyomficha Yoasi, Atalia asimwone, asipate kumwua.
12
Akakaa kwao Nyumbani mwa Mungu na kufichwa miaka sita, Atalia alipokuwa mfalme wa kike wa nchi hiyo.
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 23 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36