bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 36
2 Chronicles 36
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 35
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
1
Watu wa nchi hii wakamchukua Yoahazi, mwana wa Yosia, wakamfanya kuwa mfalme mahali pa baba yake Yosia mle Yerusalemu.
2
Yoahazi alikuwa mwenye miaka 23 alipoupata ufalme, akawa mfalme miezi 3 mle Yerusalemu;
3
ndipo, mfalme wa Misri alipomwondoa Yerusalemu, akailipisha nchi hii vipande 100 vya fedha, ndio shilingi milioni na 200000, na kipande kimoja cha dhahabu, ndio shilingi 220000.
4
Mfalme wa Misri akamfanya ndugu yake Eliakimu kuwa mfalme wa Wayuda na wa Wayerusalemu, akaligeuza jina lake, akamwita Yoyakimu; lakini ndugu yake Yoahazi Neko akamchukua, akampeleka Misri.
5
Yoyakimu alikuwa mwenye miaka 25 alipoupata ufalme, akawa mfalme miaka 11 mle Yerusalemu, akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana Mungu wake.
6
Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, akamjia, akamfunga kwa minyororo kumpeleka Babeli.
7
Navyo vyombo vingine vya Nyumba ya Bwana Nebukadinesari akavipeleka Babeli, akvitia jumbani mwake huko Babeli.
8
Mambo mengine ya Yoyakimu na matapisho yake, aliyoyafanya, na mengine yaliyooneka kwake tunayaona, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Waisiraeli na wa Wayuda. Naye mwanawe Yoyakini akawa mfalme mahali pake.
9
Yoyakini alikuwa mwenye miaka 8 alipoupata ufalme, akawa mfalme miezi mitatu na siku kumi mle Yerusalemu, akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana.
10
Mwaka mwingine ulipoanza, mfalme Nebukadinesari akatuma, akampeleka Babeli pamoja na vyombo vya Nyumba ya Bwana, alivyovitamani, akamfanya ndugu yake Sedekia kuwa mfalme wao Wayuda na Wayerusalemu.
11
Sedekia alikuwa mwenye miaka 21 alipoupata ufalme, akawa mfalme miaka 11 mle Yerusalemu.
12
Akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana Mungu wake; hakujinyenyekeza mbele ya mfumbuaji Yeremia aliyekuwa kinywa cha Bwana.
13
Hata mfalme Nebukadinesari akamkataa akiacha kumtii, naye alikuwa amemwapisha na kumtaja Mungu, akaushupaza ukosi wake, nao moyo wake akaufanya kuwa mgumu, asirudi kwake Bwana Mungu wa Isiraeli.
14
Nao wakuu wote wa watambikaji na wa watu wakazidi kuyavunja maagano na kufanya mengi kama hayo matapisho yote ya wamizimu, hata Nyumba ya Bwana wakaichafua, aliyoitakasa mle Yerusalemu.
15
Yeye Bwana Mungu wa baba zao akatuma kwao wajumbe pasipo kuchoka kuwatumia, kwani aliwaonea walio ukoo wake huruma, hata Kao lake.
16
Lakini wao wakawasimanga wajumbe wa Mungu, nayo maneno yake wakayabeza na kuwafyoza wafumbuaji wake, mpaka makali ya Bwana yawakayo moto wa kuwakasirikia walio ukoo wake yakamkwea, asipatikane aliyeweza kuwaponya.
17
Ndipo, alipomhimiza mfalme wa Wakasidi kupanda kwenda kwao, akawaua vijana wao kwa panga katika Nyumba iliyokuwa Patakatifu pao, hakuwahurumia, wala mvulana wala mwanamwali, wala wazee wala wakongwe, wote pia Mungu aliwatia mkononi mwake.
18
Navyo vyombo vyote vya Nyumbani mwa Mungu, vikubwa kwa vidogo, navyo vilimbiko vya Nyumbani mwa Bwana, navyo vilimbiko vya mfalme na vya wakuu wake, vyote pia akavipeleka Babeli.
19
Kisha wakaiteketeza Nyumba ya Mungu wakazibomoa kuta za boma la Yerusalemu, nayo majumba mazuri yote wakayateketeza kwa moto, navyo vyombo vyote vyenye kima wakaviangamiza.
20
Nao wote waliosalia, wasiouawa na panga, akawahamisha kwenda Babeli, wakawa watumwa wake yeye na wa wanawe, mpaka Wapersia walipopata ufalme.
21
Ndivyo, lilivyotimia neno la Bwana, alilolisema kinywani mwa Yeremia, nchi hii ipate kuimaliza miaka yake ya mapumziko; kwani siku zote za kukaa peke yake tu ilipumzika, hata ikatimia miaka 70.
22
Katika mwaka wa kwanza wa Kiro, mfalme wa Wapersia, ndipo, lilipotimia neno la Bwana, alilolisema kinywani mwa Yeremia, maana Bwana akaiamsha roho yake Kiro, mfalme wa Wapersia, akatangaza mbiu katika ufalme wake wote kwa vinywa vya watu na kwa barua kwamba:
23
Hivi ndivyo, anavyosema Kiro, mfalme wa Wapersia: Ufalme wote wa nchi hii amenipa Bwana Mungu wa mbinguni, naye mwenyewe akaniagiza kumjengea Nyumba kule Yerusalemu katika nchi ya Yuda; ye yote wa kwenu aliye wa ukoo wake na apande kurudi kwao, naye Bwana Mungu wake awe naye!
← Chapter 35
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36