bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 11
2 Chronicles 11
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 12 →
1
Rehabeamu alipofika Yerusalemu, akaikusanya milango ya Yuda na ya Benyamini, watu 180000 waliochaguliwa kupiga vita, wapigane na Waisiraeli, wamrudishie Rehabeamu ufalme huo.
2
Lakini neno la Bwana likamjia Semaya aliyekuwa mtu wa Mungu, kwamba:
3
Mwambie Rehabeamu, mwana wa Salomo, mfalme wa Wayuda, nao Waisiraeli wote walioko katika nchi ya Yuda na ya Benyamini kwamba:
4
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Msipande kwenda kupigana na ndugu zenu! Rudini kila mtu nyumbani kwake! Kwani jambo hili limefanywa na mimi. Walipoyasikia maneno haya ya Bwana wakarudi wakiacha kumwendea Yeroboamu.
5
Rehabeamu alipokaa Yerusalemu akajenga miji yenye maboma katika nchi ya Yuda.
6
Akajenga maboma Beti-Lehemu na Itamu na Tekoa,
7
na Beti-Suri na Soko na Adulamu,
8
na Gati na Maresa na Zifu,
9
na Adoraimu na Lakisi na Azeka,
10
na Sora na Ayaloni na Heburoni; hii ndiyo miji yenye maboma katika nchi ya Yuda na ya Benyamini.
11
Haya maboma akayajenga kuwa yenye nguvu, akaweka humo wenye amri na vilimbiko vya vilaji na vya mafuta na vya mvinyo.
12
Humo katika kila mji mmoja akaweka ngao na mikuki, akaijenga kuwa yenye nguvu nyingi mno. Nchi ya Yuda na ya Benyamini ikawa yake.
13
Watambikaji na Walawi katika nchi zote za Isiraeli wakarudi upande wake na kutoka katika mipaka yao yote.
14
Kwani Walawi wakayaacha malisho na mapato yao, wakaenda Uyuda na Yerusalemu, kwa kuwa Yeroboamu na wanawe waliwatupa, waiswe watambikaji wa Bwana.
15
Akajiwekea mwenyewe watambikaji wa kutambika vilimani, nao wa kutambikia mashetani na ndama, alizozitengeneza.
16
Katika mashina yote ya Isiraeli watu waliojipa mioyo ya kumtafuta Bwana Mungu wa Isiraeli wakawafuata wale, wakaja Yerusalemu kumtolea Bwana Mungu wa baba zao ng'ombe za tambiko.
17
Hawa ndio walioutia ufalme wa Yuda nguvu, wakamwongezea Rehabeamu, mwana wa Salomo, uwezo miaka mitatu, kwani waliendelea katika njia za Dawidi na za Salomo miaka mitatu.
18
Rehabeamu akamwoa Mahalati wa Yerimoti, mwana wa Dawidi na wa Abihaili, binti Eliabu, mwana wa Isai.
19
Huyu akamzalia wana hawa: Yeusi na Semaria na Zahamu.
20
Kisha akamwoa Maka, binti Abisalomu; huyu alimzalia Abia na Atai na Ziza na Selomiti.
21
Rehabeamu akampenda maka, binti Abisalomu, kuliko wakeze na masuria zake wote, kwani alichukua wake 18 na masuria 60, akazaa wana wa kiume 28 na wa kike 60.
22
Rehabeamu akamweka Abia, mwana wa Maka, kuwa mkuu na mwenye amri kwa ndugu zake, kwani alitaka kumpa ufalme.
23
Kwa kuwa mwenye utambuzi akawatawanya wanawe wote katika nchi zote za Yuda na za Benyamini akiwaweka katika miji yote yenye maboma, akawapa vyakula vingi, akawaposea hata wanawake wengi.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36