bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 9
2 Chronicles 9
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 10 →
1
Mfalme wa kike wa Saba alipousikia uvumi wa Salomo, akaenda Yerusalemu kumjaribu Salomo kwa maulizo ya kufumbafumba, akaja na vikosi vikubwa mno na ngamia waliochukua uvumba na dhahabu nyingi na vito. Alipofika kwa Salomo akasema naye na kumwuliza yote, aliyokuwa nayo moyoni mwake.
2
Salomo akamwelezea yote, aliyomwuliza, halikuwako neno lililofichika maana kwake Salomo, asiloweza kumwelezea.
3
Ndipo, mfalme wa kike wa Saba alipouona werevu wa Salomo kuwa wa kweli, kisha akaitazama nyumba, aliyoijenga,
4
na vilaji vilivyopo mezani na vikao vya watumwa wake na kazi za watumishi wake na mavazi yao, hata watunza vinywaji wake na mavazi yao na dari, aliyoiweka juu ya Nyumba ya Bwana; ndipo, roho yake ilipozimia,
5
akamwambia mfalme: Kumbe ni ya kweli, niliyoyasikia katika nchi yangu ya mambo yako na ya werevu wako ulio wa kweli!
6
Lakini sikuyaitikia hayo maneno yao kuwa ya kweli, mpaka nikija, nikayaona kwa macho yangu. Tena naona, ya kuwa sikuambiwa nusu tu ya werevu wako mwingi mno ulio wa kweli, maana ni mkuu kuliko ule uvumi, niliousikia.
7
Wenye shangwe ni watu wako, nao hawa watumwa wako ni wenye shangwe kwa kusimama mbele yako siku zote na kuyasikia maneno ya werevu wako ulio wa kweli.
8
Bwana Mungu wako na atukuzwe, kwa kuwa alipendezwa na wewe, akakukalisha katika kiti chake cha kifalme, uwe mfalme wa Bwana Mungu wako! Kwa kuwa Mungu wako anawapenda Waisiraeli, awapatie kuwapo kale na kale, alikupa kuwa mfalme wao, uwaamue kwa wongofu.
9
Kisha akampa mfalme vipande vya dhahabu 120, ndio frasila 360, na uvumba mwingi sana na vito; uvumba mwingi kama huo, mfalme wa kike wa Saba aliompa Salomo, ulikuwa haujapatikana bado.
10
Kweli nao watumishi wa Huramu na watumishi wa Salomo waliotoa dhahabu kule Ofiri wakaleta nayo miti ya uvumba na vito,
11
naye mfalme akaitumia hiyo miti ya uvumba ya kutengeneza vipago vya Nyumba ya Bwana na vya nyumba ya mfalme na mazeze na mapango ya waimbaji. Lakini mali kama hizo hazijaonekana siku za mbele katika nchi ya Yuda.
12
Kisha mfalme Salomo akampa mfalme wa kike wa Saba yote, aliyopendezwa nayo, aliyomwomba, kuliko yale, aliyomletea mfalme; kisha akarudi kwenda kwao katika nchi yake, yeye na watumishi wake.
13
Uzito wa dhahabu, Salomo alizoletewa katika mwaka mmoja ulikuwa vipande vya dhahabu 666, ndio frasila 2000,
14
pasipo zile, watembeaji na wachuuzi walizomletea; nao wafalme wote wa nchi ya Waarabu na watawala nchi wakamletea Salomo dhahabu na fedha.
15
Mfalme Salomo akatengeneza ngao 200 za dhahabu zilizofuliwa, kila ngao moja ikatumiwa sekeli 600, ndio nusu kubwa ya frasila ya dhahabu zilizofuliwa.
16
Kisha akatengeneza ngao ndogo 300 za dhahabu zilizofuliwa, hizi ngao ndogo kila moja ikatumiwa sekeli 300, ndio ratli tisa za dhahabu; mfalme akaziweka katika nyumba ya mwituni kwa Libanoni.
17
Kisha mfalme akatengeneza kiti kikubwa cha kifalme cha pembe za tembo, akakifunikiza dhahabu tupu.
18
Hicho kiti cha kifalme kilikuwa na vipago sita vya kukipandia, tena hapo chini yake palikuwa pamefanyizwa pa kuwekea miguu, napo palikuwa pa dhahabu. Tena hapo pa kukalia palikuwa na maegemeo huku na huko, nayo mifano miwili ya simba ilikuwa imesimama hapo penye maegemeo.
19
Tena mifano kumi na miwili ya simba ilikuwa imesimama juu ya vile vipago sita huku na huko. Kitu kilichotengenezwa vizuri hivyo hakikuwako katika ufalme wote.
20
Navyo vyombo vyote vya kunywea vya mfalme Salomo vilikuwa vya dhahabu, navyo vyombo vyote vya ile nyumba ya mwituni kwa Libanoni vilikuwa vya dhahabu zilizong'azwa; kwani fedha ziliwaziwa kuwa si kitu katika siku za Salomo.
21
Kwani merikebu za mfalme zilikwenda Tarsisi zikipelekwa na watumishi wa Huramu; kila miaka mitatu hizo merikebu zilizokwenda Tarsisi zikaja mara moja, zikaleta dhahabu na fedha na pembe za tembo na tumbili na madege wenye manyoya mazuri mno wanaoitwa tausi.
22
Hivyo ndivyo, mfalme Salomo alivyokuwa mkuu kuwapita wafalme wote wa huku nchini kwa utukufu na kwa werevu wa kweli.
23
Wafalme wote wa huku nchini wakataka kuuona uso wake Salomo, wayasikie maneno ya werevu wake wa kweli, Mungu alioutia moyoni mwake.
24
Nao wakaleta kila mtu matunzo yake: vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu na mavazi na mata na uvumba na farasi na nyumbu; vikawa hivyo mwaka kwa mwaka.
25
Salomo akawa na majozi ya farasi 4000 na magari, tena wapanda farasi 12000, akawakalisha katika miji ya magari namo mwake mfalme mle Yerusalemu.
26
Akawa akiwatawala wafalme wote toka lile jito mpaka nchi ya Wafilisti kuifikilia nayo nchi ya Misri.
27
Mfalme akajipatia fedha kuwa nyingi mle Yerusalemu kama mawe, nayo miti ya miangati akajipatia kuwa mingi kama mitamba katika nchi ya tambarare.
28
Wakamletea Salomo farasi, waliowatoa Misri na katika nchi zote.
29
Mambo mengine ya Salomo ya kwanza na ya mwisho hayakuandikwa kwenye mambo ya mfumbuaji Natani na kwenye ufumbuaji wa Ahia wa Silo na kwenye maono ya mchunguzaji Yedi, aliyomchunguzia Yeroboamu, mwana wa Nebati?
30
Salomo akawa mfalme mle Yerusalemu na kuwatawala Waisiraeli wote miaka 40.
31
Kisha Salomo akaja kulala na baba zake, wakamzika mjini mwa baba yake Dawidi, naye mwanawe Rehabeamu akawa mfalme mahali pake.
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 10 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36