bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 24
2 Chronicles 24
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 25 →
1
Yoasi alikuwa mwenye miaka 7 alipoupata ufalme, akawa mfalme mle Yerusalemu miaka 40. Jina la mama yake ni Sibia wa Beri-Seba.
2
Yoasi akayafanya yanyokayo machoni pake Bwana siku zote, mtambikaji Yoyada alizokuwapo.
3
Yoyada akamwoza wake wawili, akazaa wana wa kiume na wa kike.
4
Ikawa baada ya hayo, Yoasi akajipa moyo wa kuirudishia Nyumba ya Bwana upya.
5
Akawakusanya watambikaji na Walawi, akawaambia: Tokeni, mwende katika miji yote ya Yuda, mkusanye kwa Waisiraeli wote fedha za kuitengeneza Nyumba ya Mungu wenu mwaka kwa mwaka! Neno hili na mlifanye kwa upesi! Lakini Walawi hawakulifanya kwa upesi.
6
Ndipo, mfalme alipomwita Yoyada aliyekuwa mkuu wao, akamwambia: Mbona hukuwafuatafuata Walawi, watoze Wayuda na Wayerusalemu machango, aliyoyaagiza Mose, mtumishi wa Bwana, mkutano wa Waisiraeli wayachangie Hema la Ushahidi, kisha wayalete huku?
7
Kwani wana wa Atalia, yule mwanamke aliyefanya maovu tu, wameichakaza Nyumba ya Mungu, navyo vyombo vitakatifu vyote vya Nyumba ya Bwana wakavifanya kuwa vya Mabaali,
8
Kwa kuwa mfalme aliviagiza, wakatengeneza kasha moja, wakaliweka nje langoni penye Nyumba ya Bwana,
9
wakapiga mbiu katika nchi ya Yuda namo Yerusalemu, watu wamletee Bwana machango, Mose, mtumishi wa Mungu, aliyoyaagiza kule nyikani, Waisiraeli wayatoe.
10
Wakuu wote na watu wote wakafurahi, wakayaleta, wakayatia mle kashani, hata wakalijaza.
11
Ikawa, palipotimia pa kulipeleka hilo kasha kwa wasimamizi wa mfalme, likachukuliwa na Walawi; ilikuwa hapo, walipoona, ya kuwa zimo fedha nyingi, Kisha akaja mwandishi wa mfalme na msimamizi wa mtambikaji mkuu, wakatoa fedha zote zilizokuwamo kashani, kisha wakalichukua, wakalirudisha mahali pake siku kwa siku. Ndivyo, walivyokusanya fedha nyingi.
12
Mfalme na Yoyada wakawapa mafundi wa kazi za kuitengeneza Nyumba ya Bwana; nao wakajitafutia waashi na maseremala wa kuirudishia Nyumba ya Bwana upya, hata wafua vyuma na shaba wa kuitengenezatengeneza Nyumba ya Bwana.
13
Hao mafundi wakazifanya kazi zao, kwa kazi za mikono yao matengenezo yakaendelea, wakaisimamisha Nyumba ya Bwana kuwa, kama ilivyokuwa, wakaishupaza.
14
Walipokwisha wakazipeleka fedha zilizobaki kwa mfalme na kwa Yoyada, wakazitumia kutengeneza vyombo vya Nyumba ya Bwana, ni vyombo vya kutumia, walipotoa ng'ombe za tambiko, na vyano na vyombo vingine vya dhahabu na vya fedha, kisha wakamtolea Bwana katika Nyumba ya Bwana ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima pasipo kukoma siku zote za Yoyada.
15
Yoyada alipokuwa mzee wa kushiba siku, akafa; akawa mwenye miaka 130 alipokufa.
16
Wakamzika mjini mwa Dawidi penye wafalme, kwani aliwafanyizia Waisiraeli mema kwa kuyatengeneza mambo ya Mungu na ya Nyumba yake.
17
Yoyada alipokwisha kufa, wakuu wa Wayuda wakaja, wakamwangukia mfalme; ndipo, mfalme alipowasikia.
18
Wakaiacha Nyumba ya Bwana Mungu wa baba zao, wakaitumikia miti ya Ashera na nguzo za kutambikia; ndipo, Mungu alipoikasirikia nchi ya Yuda na Yerusalemu kwa kuzikora hizo manza,
19
akatuma kwao wafumbuaji, wawarudishe kwake Bwana, lakini hawakuwasikiliza.
20
Ndipo, roho ya Mungu ilipomwingia Zakaria, mwana wa mtambikaji Yoyada, akaja kusimama mbele ya watu mahali palipokuwa juu kidogo, akawaambia: Hivi ndivyo, Mungu anavyosema: Mbona mnayaacha maagizo ya Bwana, msiendelee kufanikiwa? Kwa kuwa mmemwacha Bwana, naye amewaacha.
21
Ndipo, walipomlia njama, wakamwua kwa kumpiga mawe uani penye Nyumba ya Bwana kwa kuagizwa na mfalme.
22
Ndipo, mfalme Yoasi alipoacha kuyakumbuka matendo yote ya upole, baba yake Yoyada aliyomfanyizia, naye akamwua mwanawe; huyu alipokufa akasema: Bwana na ayaone na kuyalipisha!
23
Ikawa, mwaka ulipokwisha, vikapanda vikosi vya Washami, kupigana naye, wakaja kuiingia nchi ya Yuda, hata Yerusalemu, wakawaangamiza wakuu wote wa watu wote pia, nayo mateka yao wakayatuma kwa mfalme wa Damasko.
24
Kweli hivyo vikosi vya Ushami vilikuja vyenye watu wachache tu, lakini Bwana akatia mikononi mwao vikosi vilivyokuwa vyenye watu wengi sana, kwa kuwa walimwacha Bwana Mungu wa baba zao; ndivyo, walivyompatiliza Yoasi.
25
Walipokwenda zao, wakamwacha mwenye magonjwa mengi; ndipo, watumishi wake walipomlia njama, kwa kuwa alizimwaga damu za wana wa mtambikaji Yoyada, wakamwua kitandani pake, akafa; kisha wakamzika mjini mwa Dawidi, lakini hawakumzika penye makaburi ya wafalme.
26
Waliomlia njama ndio hawa: Zabadi, mwana wa Simati aliyekuwa mwanamke wa Kiamoni, na Yozabadi, mwana wa Simuriti aliyekuwa mwanamke wa Kimoabu.
27
Mambo ya wanawe na yale ya machango mengi, aliyoyachangisha, na majengo ya kuijenga tena Nyumba ya Mungu, tunayaona, yameandikwa katika maelezo ya kitabu cha matendo ya wafalme. Naye mwanawe Amasia akawa mfalme mahali pake.
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 25 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36