bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 26
2 Chronicles 26
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 25
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 27 →
1
Watu wote wa Yuda wakamchukua Uzia aliyekuwa mwenye miaka 16, wakamfanya kuwa mfalme mahali pa baba yake Amasia.
2
Yeye akaujenga Eloti, akaurudisha kwao Wayuda, mfalme alipokuwa amelala na baba zake.
3
Uzia alikuwa mwenye miaka 16 alipoupata ufalme, akawa mfalme miaka 52 mle Yerusalemu. Jina la mama yake ni Yekolia wa Yerusalemu.
4
Akayafanya yanyokayo machoni pake Bwana, kama yote, baba yake Amasia aliyoyafanya.
5
Akawa akimtafuta Mungu siku, alizokuwapo Zakaria aliyemfundisha maana ya kumtazamia Mungu; nazo siku zile, alipomtafuta Bwana, Mungu akayaendesha mambo yake.
6
Akatoka, akapigana na Wafilisti, akalivunja boma la Gati na boma la Yabune na boma la Asdodi, akajenga miji kwao Waasdodi nako kwao Wafilisti.
7
Mungu akamsaidia kuwashinda Wafilisti na Waarabu waliokaa Guri-Baali na Wameuni.
8
Ndipo, Waamoni walipompa Uzia mahongo, jina lake likafika hata Misri, kwani alijipatia nguvu zaidi.
9
Kisha Uzia akajenga minara huko Yerusalemu penye lango la pembeni napo penye lango la bondeni napo, boma lilipojipinda, akaitia nguvu.
10
Hata nyikani akajenga minara, akachimba visima vingi, kwani alikuwa na makundi mengi katika nchi ya tambarare, nako kwenye mbuga; akawa na wakulima na watunza mizabibu milimani na mashambani kwenye wiva, kwani alipenda kazi za ulimaji.
11
Tena Uzia alikuwa na vikosi vya wapiga vita waliotoka kupigana, kila kimoja chenye hesabu ya watu waliokaguliwa na mwandishi Yieli na mwenye amri Masea kwa msaada wa Hanania aliyekuwa mkuu wa mfalme;
12
hesabu yote ya wakuu wa milango ya mafundi wa vita ilikuwa 2600.
13
Mikononi mwao vilikuwa vikosi vya askari, watu 307500 waliopiga vita kwa nguvu nyingi, wamsaidie mfalme kushinda adui.
14
Hivyo vikosi vyote Uzia akavipatia ngao na mikuki na kofia ngumu na shati za vyuma na pindi na mawe ya makombeo.
15
Akatengeneza mle Yerusalemu makombeo makubwa, akitumia mafundi wenye mawazo ya kutunga matengenezo kama hayo, akayaweka juu ya minara, hata pembenipembeni ya kutupia mishale na mawe makubwa; kwa hiyo jina lake likafika hata katika nchi za mbali, kwani vikastaajabisha, alivyosaidiwa, akaendelea kupata nguvu.
16
Alipopata nguvu, moyo wake ukajikuza, afanye yasiyofanywa, akamvunjia Bwana Mungu wake maagano akiingia Jumbani mwa Bwana kumvukizia mezani pa kuvukizia.
17
Mtambikaji Azaria akamfuata pamoja na watambikaji wa Bwana 80 waliokuwa wenye nguvu.
18
Wakajipanga, wamkinge mfalme Uzia wakimwambia: Siyo kazi yako, Uzia, kumvukizia Bwana, ila ni yao watambikaji walio wana wa Haroni, wametakaswa, wavukize. Toka Patakatifu, kwani umeyavunja maagano, kwani hutajipatia macheo kwa Bwana Mungu.
19
Ndipo, Uzia alipochafuka, nacho kivukizio cha kuvukizia kilikuwa mkononi mwake; alipowatolea watambikaji machafuko yake, ukoma ukamtoka pajini pake usoni pa watambikaji mle Nyumbani mwa Bwana kando ya meza ya kuvukizia.
20
Mtambikaji mkuu Azaria na watambikaji wote walipomgeukia, mara wakamwona kuwa na ukoma pajini; ndipo, walipomfukuza huko upesiupesi, naye akajihimiza kutoka, kwa kuwa Bwana amempiga.
21
Mfalme Uzia akawa mwenye ukoma hata siku ya kufa kwake, akakaa akiwa mwenye ukoma katika nyumba ya wagonjwa waliotengwa, kwani alikatazwa kuiingia Nyumba ya Bwana, mwanawe Yotamu akawa mkuu nyumbani mwa mfalme, akawaamua watu wa nchi hii.
22
Mambo mengine ya Uzia, ya mwanzo na ya mwisho, aliyaandika mfumbuaji Yesaya, mwana wa Amosi.
23
Uzia akaja kulala na baba zake, wakamzika kwa baba zake porini kwenye makaburi ya wafalme, kwani walisema: Huyu ni mkoma. Kisha mwanawe Yotamu akawa mfalme mahali pake.
← Chapter 25
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 27 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36