bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 10
2 Chronicles 10
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 11 →
1
Rehabeamu akaenda Sikemu, kwani Waisiraeli wote walifikia Sikemu kumpa ufalme.
2
Naye Yeroboamu, mwana wa Nebati, alikuwa huko Misri, alikokimbilia alipomkimbia mfalme Salomo; lakini alipopashwa hizo habari akarudi toka Misri.
3
Wakamwita, naye akaja na Waisiraeli wote, wakamwambia Rehabeamu kwamba:
4
Baba yako alitutwisha mzigo mzito, sasa wewe utupunguzie ule utumwa mgumu wa baba yako nao mzigo wake mzito, aliotutwisha! Kisha tutakutumikia.
5
Akawaambia: Kwanza nendeni siku tatu, kisha rudini kwangu! Watu walipokwenda zao,
6
mfalme Rehabeamu akafanya shauri na wazee waliomtumikia baba yake Salomo, alipokuwa mzima bado, akawauliza: Ninyi shauri lenu ni nini? Watu hawa tuwape majibu gani?
7
Wakamwambia hivi: Ukijulikana kwao watu hawa kuwa mwema, ukiwapendeza na kuwaambia maneno mema, ndipo, watakapokuwa watumishi wako siku zote.
8
Lakini akaliacha shauri la wazee, walilompa, akafanya shauri na vijana waliokua naye na kumtumikia,
9
akawauliza: Ninyi shauri lenu ni nini? Tuwape majibu gani watu hawa walioniambia: Tupunguzie mzigo, aliotutwisha baba yako?
10
Vijana hawa waliokuwa naye wakasemezana naye kwamba: Haya ndiyo, uwaambie watu waliokuambia kwamba: Baba yako aliukuza mzigo wetu kuwa mzito, wewe utupunguzie huu mzigo wetu, basi, uwaambie hivyo: Kidole changu kidogo na kinenepe kuliko viuno vya baba yangu;
11
sasa vitakuwa hivi: kama baba yangu aliwatwisha mzigo mzito, mimi nitauzidisha mzigo wenu; kama baba yangu aliwapiga fimbo, mimi nitawapiga viboko vyenye miiba.
12
Yeroboamu na watu wote wakaja kwake Rehabeamu siku ya tatu, kama mfalme alivyosema kwamba: Rudini siku ya tatu!
13
Ndipo, mfalme alipowapa majibu magumu, yeye Rehabeamu akiliacha shauri la wazee,
14
akasema nao na kulifuata shauri la vijana, akawaambia: kama baba yangu aliwatwisha mzigo mzito, mimi nitauzidisha; kama baba yangu aliwapiga fimbo, mimi nitawapiga viboko vyenye miiba.
15
Mfalme hakuwasikia wale watu, kwani Mungu aliyageuza kuwa hivyo, yeye Bwana apate kulitimiza neno lake, alilomwambia Yeroboamu, mwana wa Nebati, kinywani mwa Ahia wa Silo.
16
Waisiraeli wote walipoona, ya kuwa mfalme hakuwasikia, ndipo, watu walipomjibu mfalme kwamba: Sisi tuna bia gani na Dawidi? Hatuna fungu lo lote kwake mwana wa Isai. Waisiraeli, haya! Rudini sasa mahemani kwenu, kila mtu kwake! Nawe Dawidi, na uuangalie mwenyewe mlango wako! Ndipo, Waisiraeli wote walipokwenda mahemani kwao.
17
Ni wana wa Isiraeli waliokaa katika miji ya Yuda tu, Rehabeamu aliowapata, awe mfalme wao.
18
Mfalme Rehabeamu alipomtuma Hadoramu aliyekuwa msimamizi wa kazi za nguvu, wana wa Isiraeli wakampiga mawe, hata akafa. Kisha mfalme Rehabeamu akajihimiza kupanda garini na kukimbilia Yerusalemu.
19
Ndivyo, Waisiraeli walivyojitenga na mlango wa Dawidi mpaka siku ya leo.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36