bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 3
2 Chronicles 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 4 →
1
Salomo akaanza kuijenga nyumba ya Bwana Yerusalemu katika mlima wa Moriya, Bwana alikomtokea baba yake Dawidi, mahali pale, Dawidi alipopaagiza penye kupuria ngano pa Myebusi Ornani.
2
Akaanza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili wa mwaka wa nne wa ufalme wake.
3
Nayo misingi, Salomo aliyoiweka ya kuijenga nyumba ya Mungu, ni hii: urefu wa kwenda mbele kwa kipimo cha kale ulikuwa mikono 60, nao upana wake ulikuwa mikono 20.
4
Ukumbi uliokuwa mbele ya nyumba ulikuwa mikono 20 kwa kuupatanisha na upana wa nyumba, nao urefu wa kwenda juu ulikuwa mikono 120, ndani akazifunika kuta zake kwa mabati ya dhahabu tupu.
5
Nyumba kubwa akaipigilia kutani mbao za mivinje, nazo akazivika mabati ya dhahabu nzuri, humo namo akachora mitende na mikufu.
6
Akaipamba hiyo nyumba kwa vito vyenye kima, ipate utukufu; zile dhahabu zilikuwa dhahabu za Parawaimu.
7
Boriti na vizingiti na kuta zake na milango yake ya humu nyumbani akaivika mabati ya dhahabu, napo kutani akachora Makerubi.
8
Kisha akapatengeneza Patakatifu Penyewe, urefu wake ulikuwa mikono 20 kwa kuupatanisha na upana wa nyumba, upana wake nao ulikuwa mikono 20, akapavika mabati ya dhahabu nzuri za vipande vya dhahabu 600, ndio frasila 1800.
9
Misumari ilipopimiwa uzito wa dhahabu yao, ukawa sekeli za dhahabu 50, ndio ratli mbili. Navyo vyumba vya juu akavivika dhahabu.
10
Kisha mle Patakatifu Penyewe akatengeneza Makerubi mawili yaliyochongwa na mafundi, nayo akayafunikiza dhahabu.
11
Mabawa ya haya Makerubi urefu wao ulikuwa mikono 20: bawa la moja lenye mikono mitano liligusa ukuta wa nyumba, nalo la pili lenye mikono mitano liligusa bawa la Kerubi la pili;
12
vilevile bawa la Kerubi la pili lenye mikono mitano liligusa ukuta wa nyumba, nalo bawa la pili lenye mikono mitano lilishikamana na bawa lake lile Kerubi jingine.
13
Hivyo, haya mabawa ya Makerubi yalivyokuwa yamekunjuka, yalikuwa yenye mikono 20, nayo yalisimama kwa miguu yao, nazo nyuso zao zilielekea nyumbani.
14
Akatungika pazia la nguo za kifalme nyeusi na nyekundu na za rangi na za bafta, namo akashonea mifano ya Makerubi.
15
Mbele ya nyumba akaweka nguzo mbili zenye urefu wa mikono 35, nacho kichwa kilichokuwa juu ya kila moja kilikuwa chenye urefu wa mikono mitano.
16
Akatengeneza hata mikufu kuwa ukingo wa chini wa hivyo vichwa, akaitia juu ya hizo nguzo; kisha akatengeneza komamanga 100, akaziangika pale penye mikufu.
17
Akazisimamisha hizo nguzo mbele ya jumba hili, moja kuumeni, moja kushotoni; ya kuumeni akaiita Yakini (Hushikiza), ya kushotoni Boazi (Nguvu imo).
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36