bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 16
2 Chronicles 16
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 17 →
1
Katika mwaka wa 36 wa ufalme wa Asa ndipo, Basa, mfalme wa Waisiraeli, alipopanda kuijia nchi ya Yuda, akajenga Rama, asipatikane mtu anayeweza kutoka wala kuingia kwa Asa, mfalme wa Wayuda.
2
Ndipo, Asa alipochukua fedha na dhahabu katika vilimbiko vya Nyumba ya Bwana na vya nyumba ya mfalme, akazituma kwake Benihadadi, mfalme wa Ushami, aliyekaa Damasko, kumwambia:
3
Liko agano, tuliloliagana mimi na wewe, naye baba yangu na baba yako; kwa hiyo ninatuma kwako fedha na dhahabu. Nenda, ulivunje agano, uliloliagana na Basa, mfalme wa Waisiraeli, aondoke kwangu!
4
Benihadadi akamwitikia mfalme Asa, akawatuma wakuu wa vikosi vyake, alivyokuwa navyo, kwenda kupigana na miji ya Waisiraeli, wakaiingia miji ya Iyoni na Dani na Abeli-Maimu na miji yote ya Nafutali iliyokuwa yenye vilimbiko.
5
Basa alipoyasikia haya akaacha kuujenga Rama na kuzikomesha kazi zake.
6
Kisha mfalme Asa akawatwaa Wayuda wote, wakayachukua mawe ya huko Rama nayo miti yake, Basa aliyoitumia ya kujenga Rama, naye akaitumia ya kujenga Geba na Misipa.
7
Siku hizo mtazamaji Hanani akaja kwa Asa, mfalme wa Wayuda, akamwambia: Kwa kuwa umemwegemea mfalme wa Ushami, usimwegemee Bwana Mungu wako, kwa hiyo vikosi vya mfalme wa Ushami vimeponyoka mkononi mwako.
8
Wale Wanubi na Walibia hawakuwa vikosi vingi vyenye magari na wapanda farasi wengi mno? Lakini kwa kuwa ulimwegemea Bwana, akawatia mkononi mwako.
9
Kwani macho ya Bwana huzunguka katika nchi zote, ajitokeze kuwa mwenye nguvu kwao waliomwelekezea mioyo yao yote mizima. Katika jambo hili umefanya upumbavu, kwa hiyo tangu sasa huna budi kupiga vita.
10
Asa akamkasirikia mtazamaji, akamfunga nyumbani mwenye mikatale, kwani alimchafukia kwa ajili ya hayo. Nao watu wengine Asa akawakorofisha siku zile.
11
Mambo ya Asa, ya kwanza na ya mwisho, tukitaka kuyatazama, tunayaona, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Wayuda na wa Waisiraeli.
12
Katika mwaka wa 39 wa ufalme wake Asa akaugua miguu, huu ugonjwa wake ukazidi sana; namo katika huu ugonjwa wake hakumtafuta Bwana, ila waganga.
13
Kisha Asa akaja kulala na baba zake, akafa katika mwaka wa 41 wa ufalme wake.
14
Wakamzika penye makaburi yake, aliyojichimbia mjini mwa Dawidi; wakamlaza katika kilalo walichokijaza uvumba wa namna nyingi na manukato yaliyotengenezwa na mafundi, wakamvukizia mavukizo makubwa sana.
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 17 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36