bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 20
2 Chronicles 20
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 21 →
1
Ikawa baada ya hayo, wakaja wana wa Moabu na wana wa Amoni pamoja na Waamoni wengine kumpelekea Yosafati vita.
2
Watu wakaja kumpasha Yosafati habari kwamba: Uvumi wa watu wengi unakujia, unatoka ng'ambo ya huko ya bahari upande wa Ushami, nao wamekwisha kufika Hasesoni-Tamari, ndio Engedi.
3
Yosafati akaogopa, akamwelekezea Bwana uso wake na kulitafuta shauri lake, akatangaza katika nchi yote ya Yuda, watu wafunge.
4
Wayuda wakakusanyika kutafuta msaada kwa Bwana; walipokwisha kufika na kutoka katika miji yote ya Yuda, wamtafute Bwana,
5
Yosafati akaja kusimama katika huo mkutano wa Wayuda na Wayerusalemu Nyumbani mwa Bwana mbele ya ua mpya,
6
akasema: Bwana Mungu wa baba zetu, wewe siwe Mungu akaaye mbinguni na kuzitawala nchi zote za wamizimu zenye wafalme? Mkononi mwako zimo nguvu na uwezo mwingi, hakuna awezaye kujisimamisha kwako.
7
Wewe hukuwafukuza wenyeji wa nchi hii mbele yao walio ukoo wako wa Waisiraeli, ukaitoa na kuwapa wao wa uzao wa mpenzi wako Aburahamu, iwe yao kale na kale?
8
Wakakaa huku, wakakujengea huku Patakatifu pa Jina lako kwa kwamba:
9
Mabaya yatakapotujia, kama panga za kutupatiliza au magonjwa ya kuambukiza au njaa, tuje kusimama mbele ya Nyumba hii na kukulalamikia usoni pako kwa kusongeka kwetu, kwani Jina lako linakaa humu Nyumbani; ndipo, utakapotusikia, utuokoe.
10
Sasa watazame hawa wana wa Amoni na wa Moabu na wa milima ya Seiri! Hapo, Waisiraeli walipotoka katika nchi ya Misri, hukuwapa ruhusa kuingia kwao hawa; kwa hiyo waliondoka kwao pasipo kuwaangamiza.
11
Sasa unawaona, wanavyotufanyizia wakija kutufukuza katika nchi hii, uliyotupatia, utupe sisi, iwe fungu letu.
12
Mungu wetu, hutaki kuwapatiliza? Kwani kwetu sisi hakuna nguvu za kuushinda huu uvumi ya watu wengi mno waliotujia. Sisi hatujui la kufanya, kwa hiyo macho yetu yanakuelekea.
13
Nao Wayuda wote walikuwa wamesimama mbele ya Bwana pamoja na watoto wao wachanga na wanawake na wana wao.
14
Ndipo, Yahazieli, mwana wa Zakaria, mwana wa Benaya, mwana wa Yieli, mwana wa Matania, aliyekuwa Mlawi wa mlango wa Asafu, alipoingiwa na Roho ya Bwana pale katikati ya mkutano,
15
akasema: Ninyi Wayuda wote nanyi wenyeji wa Yerusalemu na wewe mfalme Yosafati, sikilizeni: Haya ndiyo, Bwana anayowaambia: Msiogope, wala msiingiwe na vituko mkiuona uvumi huu wa watu wengi! Kwani vita hivi si vyenu, ila vya Mungu.
16
Kesho shukeni kwenda kwao! Ndipo, mtakapowaona, wakipanda pa kupandia kwenda Sisi, nanyi mtawakuta kwenye mwisho wa bonde lililoko mbele ya nyika ya Yerueli.
17
Lakini ninyi hamtapigana huko, jipangeni tu na kusimama, mwone, Bwana atakavyowapatia wokovu, ninyi Wayuda na Wayerusalemu! Msiogope, wala msiingiwe na vituko! Kesho watokeeni tu! Naye Bwana atakuwa nanyi.
18
Ndipo, Yosafati alipouinamisha uso wake hata chini, hata Wayuda wote pamoja na wenyeji wa Yerusalemu wakamwangukia Bwana na kumwomba.
19
Kisha wakainuka Walawi waliokuwa wa mlango wa Kehati na wa Kora kumshangilia Bwana Mungu wa Isiraeli, wakizipaza kabisa sauti zao ziwe kuu.
20
Kesho yake wakaondoka na mapema kwenda nyikani kwa Tekoa; hapo, walipotoka, Yosafati akasimama hapo akisema: Nisikilizeni, ninyi Wayuda na wenyeji wa Yerusalemu! Mtegemeeni Bwana Mungu wenu, ndipo, mtakaposhupazwa! Wategemeeni nao wafumbuaji wake, ndipo, mtakapofanikiwa!
21
Alipokwisha kuwapa watu shauri hili akaweka watakaomwimbia Bwana nao watakaoutukuza urembo wa Patakatifu, watoke na kuwatangulia wenye mata na kusema: Mshukuruni Bwana, ya kuwa upole wake ni wa kale na kale!
22
Papo hapo, walipoanza kupiga yowe na shangwe, ndipo, Bwana alipoleta watu wa kuwavizia wana wa Amoni na wa Moabu nao wa milima ya Seiri walioingia katika nchi ya Yuda.
23
Maana wana wa Amoni na wa Moabu wakawainukia wenyeji wa milimani kwa Seiri na kuwaua na kuwaangamiza, walipokwisha kuwamaliza wenyeji wa Seiri, wakasaidiana kila mtu na mwenzake kuuana.
24
Wayuda walipofika hapo pa kuchungulia nyikani, wakiugeukia ule uvumi wa watu, wakaona mizoga tu iliyolala chini, hakuwako aliyepona.
25
Ndipo, Yosafati na watu wake walipokuja kujichukulia nyara, wakaona kwao mali nyingi penye hiyo mizoga na vyombo vyenye kima, wakawavua vingi mno, wasiweze kuvichikua vyote; wakawako siku tatu wakipokonya nyara, kwani zilikuwa nyingi.
26
Siku ya nne wakakusanyika katika Bonde la Tukuzo, kwani huko ndiko, walikomtukuzia Bwana; kwa sababu hii mahali pale wakapaita Bonde la Tukuzo hata leo.
27
Kisha watu wote wa Yuda na wa Yerusalemu wakarudi, naye Yosafati akawatangulia kurudi Yerusalemu na kufurahi, kwani Bwana aliwapa kuwafurahia adui zao.
28
Wakaingia Yerusalemu na kupiga mapango na mazeze na matarumbeta, wakaingia Nyumbani mwa Bwana.
29
Tisho la Bwana likaziguia hizo nchi zote zenye wafalme, waliposikia, ya kama Bwana amepigana na adui za Waisiraeli.
30
Kwa hiyo ufalme wa Yosafati ukapata kutengemana, Mungu wake akimpatia utulivu pande zote.
31
Yosafati akawa mfalme wa Wayuda, naye alikuwa mwenye miaka 35 alipoupata ufalme, akawa mfalme mle Yerusalemu miaka 25. Jina la mama yake ni Azuba, binti Silihi.
32
Akaendelea kuishika njia ya baba yake Asa, hakuiacha kabisa, akayafanya yanyokayo machoni pake Bwana.
33
Matambiko ya vilimani tu hayakukoma, kwani watu hawajamwelekezea Mungu wa baba zao mioyo yao.
34
Mambo mengine ya Yosafati, ya kwanza na ya mwisho, tunayaona, yameandikwa katika mambo ya Yehu, mwana wa Hanani, yaliyotiwa katika kitabu cha wafalme wa Waisiraeli.
35
Baada ya hayo Yosafati, mfalme wa Wayuda, akajiunga na Ahazia, mfalme wa Waisiraeli; lakini huyu matendo yake, aliyoyafanya, yalikuwa maovu.
36
Akajiunga naye kwa kutengeneza merikebu za kwenda Tarsisi; wakatengeneza merikebu hata huko Esioni-Geberi.
37
Eliezeri, mwana wa Dodawa wa Maresa, akamfumbulia Yosafati kwamba: Kwa kuwa umejiunga na Ahazia, Bwana atazivunja hizi kazi zako. Kwa hiyo vyombo vikavunjika, havikuweza kwenda Tarsisi.
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 21 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36