bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 29
2 Chronicles 29
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 30 →
1
Hizikia akaupata ufalme alipokuwa mwenye miaka 25, akawa mfalme miaka 29 mle Yerusalemu. Jina la mama yake ni Abia, binti Zakaria.
2
Akayafanya yanyokayo machoni pake Bwana kama yote, aliyoyafanya baba yake Dawidi.
3
Katika mwaka wa kwanza wa kutawala kwake katika mwezi wa kwanza akaifungua milango ya Nyumba ya Bwana, akaitengeneza vema.
4
Kisha akaleta watambikaji na Walawi, akawakusanya uwanjani upande wa maawioni kwa jua.
5
Akawaambia: Nisikieni, ninyi Walawi! Sasa jieueni, mpate kuieua nayo Nyumba ya Bwana Mungu wa baba zenu na kuutoa uchafu hapa Patakatifu!
6
Kwani baba zetu wameyavunja maagano, wakayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana Mungu wetu, wakamwacha na kuzigeuza nyuso zao, zisilitazame Kao la Bwana, wakalielekezea migongo.
7
Wakaifunga nayo milango ya ukumbi, wakazizima taa zake, hawakumvukizia Mungu wa Isiraeli mavukizo, wala hawakumtolea ng'ombe za tambiko hapa Patakatifu.
8
Kwa hiyo makali ya Bwana yakaikalia nchi ya Yuda na Yerusalemu, akawatoa, watupwe huko na huko, wastukiwe kabisa na kuzomewa, kama ninyi mnavyoviona wenyewe kwa macho yenu.
9
Tazameni! Baba zetu waliuawa kwa panga, nao wana wetu wa kiume na wa kike pamoja na wanawake wetu wakatekwa kwa sababu hiyo.
10
Sasa mimi nimejipa moyo, nifanye agano na Bwana Mungu wa Isiraeli, makali yake yawakayo moto yatuondokee.
11
Sasa ninyi wanangu, msizurure! Kwani ninyi Bwana aliwachagua, msimame mbele yake na kumtumikia, mwe watumishi wake na wavukizaji wake.
12
Ndipo, walipoinuka Walawi: Mahati, mwana wa Amasai, na Yoeli, mwana wa Azaria, walio wana wa Kehati; nao waliokuwa wana wa Merari: Kisi, mwana wa Abudi, na Azaria, mwana wa Yehaleleli, nao waliokuwa wana wa Gersoni: Yoa, mwana wa Zima, na Edeni, mwana wa Yoa;
13
nao waliokuwa wana wa Elisafani: Simuri na Yieli; nao waliokuwa wana wa Asafu: Zakaria na Matania;
14
nao waliokuwa wana wa Hemani: Yehieli na Simei; nao waliokuwa wana wa Yedutuni: Semaya na Uzieli.
15
Wakawakusanya ndugu zao, wakajieua; kisha wakaja kwa agizo la mfalme kuitakasa Nyumba ya Bwana, kama Bwana alivyosema.
16
Watambikaji wakaingia Nyumbani mwa Bwana ndani kuitakasa na kuyatoa machafu yote, waliyoyaona Jumbani mwa Bwana, wakayapeleka uani penye Nyumba ya Bwana; ndiko, Walawi walikoyachukua, wayapeleke nje mtoni kwa Kidoroni.
17
Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza wakaanza kuitakasa, siku ya nane ya huo mwezi wakafika penye ukumbi wa Bwana, wakaitakasa Nyumba ya Bwana tena siku nane, wakaimaliza siku ya kumi na sita ya mwezi wa kwanza.
18
Kisha wakaingia nyumbani kwa mfalme Hizikia, wakamwamiba: Tumeitakasa Nyumba yote ya Bwana, hata meza ya kuteketezea ng'ombe za tambiko na vyombo vyake vyote,, hata meza ya mikate, aliyowekewa Bwana, na vyombo vyake vyote.
19
Navyo vyombo vyote, mfalme Ahazi alivyovichafua katika ufalme wake, alipoyavunja maagano, tumevitengeneza na kuvitakasa, utaviona, viko mbele ya meza ya kumtambikia Bwana.
20
Ndipo, mfalme Hizikia alipoamka na mapema, akawakusanya wakuu wa mji, akapanda kwenda Nyumbani kwa Bwana.
21
Wakaleta madume saba ya ng'ombe na madume saba ya kondoo na wana kondoo saba na madume saba ya mbuzi kuwa ng'ombe za tambiko za weuo kwa ajili ya ufalme na kwa ajili ya Patakatifu na kwa ajili ya Wayuda. Akawaambia watambikaji, wana wa Haroni, wawatoe kuwa ng'ombe za tambiko hapo pa kumtambikia Bwana.
22
Ndipo, walipowachinja hao ng'ombe, nao watambikaji wakazichukua damu zao, wakazinyunyizia meza ya kutambikia; wakawachinja nao madume ya kondoo, nazo damu zao wakazinyunyizia meza ya kutambikia, wakawachinja nao wana kondoo, nazo damu zao wakazinyunyizia meza ya kutambikia.
23
Kisha wakawapeleka madume ya mbuzi ya weuo mbele ya mfalme na mbele ya huo mkutano, wakawabandikia mikono yao.
24
Kisha watambikaji wakawachinja, nazo damu zao wakazinyunyizia meza ya Bwana kuwa mweuo wa kuwapatia Waisiraeli wote upozi, kwani mfalme aliagiza kwa ajili ya Waisiraeli wote kutoa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na za weuo.
25
Naye alikuwa amewasimamisha Walawi penye Nyumba ya Bwana, wakiyashika matoazi na mapango na mazeze, kama Dawidi na Gadi aliyekuwa mchunguzaji wa mfalme na mfumbuaji Natani walivyoviagiza; kwani agizo hilo lilitoka kwa Bwana, likatokea vinywani mwa wafumbuaji wake.
26
Kwa hiyo Walawi wakasimama na kuvishika vyombo vya Dawidi, nao watambikaji wakashika matarumbeta.
27
Hizikia alipoagiza kuziteketeza ng'ombe za tambiko mezani pa kutambikia, papo hapo tambiko lilipanzia, ndipo, wimbo wa Bwana ulipoanzia pamoja na matarumbeta yaliyoongozwa na vyombo vya Dawidi, mfalme wa Waisiraeli.
28
Mkutano wote pia ukamwangukia Bwana, wimbo ulipoimbwa, nayo matarumbeta yalipolia; yote yakawa hivyo, hata ng'ombe za tambiko zikaisha kuteketezwa.
29
Walipokwisha kuziteketeza hizo ng'ombe za tambiko, wakapiga magoti, yeye mfalme nao wote waliokuwako naye, wakamwangukia Bwana.
30
Kisha mfalme Hizikia na wakuu wakawaambia Walawi, wamtukuze Bwana na kuyaimba maneno ya Dawidi na ya mchunguzaji Asafu. Ndipo, walipomtukuza kwa furaha, kisha wakainama, wakamwangukia.
31
Kisha Hizikia akawaitikia akisema: Sasa mmeyajaza magao yenu kumtumikia Bwana, basi, karibuni, mlete huku kwenye Nyumba ya Bwana ng'ombe za tambiko na vipaji vya shukrani! Ndipo, watu wa huo mkutano walipoleta ng'ombe za tambiko na vipaji vya shukrani, kila mtu akatoa ng'ombe za tambiko, kama moyo ulivyopenda.
32
Hesabu ya ng'ombe za tambiko, watu wa huo mkutano walizozitoa, ikawa ng'ombe 70, madume ya kondoo 100, wana kondoo 200; hawa wote walikuwa wa kumteketezea Bwana.
33
Tena za matambiko mengine wakatolewa ng'ombe 600 na kondoo na mbuzi 3000.
34
Watambikaji tu walikuwa wachache, hawakuweza kuwachuna ng'ombe wote wa kuteketezwa, kwa hiyo ndugu zao Walawi wakawasaidia, mpaka kazi hii ikaisha, tena mpaka watambikaji wakajieua, kwani Walawi walikuwa wenye mioyo iliyojihimiza kujieua kuliko yao watambikaji.
35
Nao ng'ombe wa kuteketezwa nzima walikuwa wengi, vilevile vipande vyenye mafuta ya ng'ombe za tambiko za shukurani na vinywaji vya tambiko vilivyopasa kila ng'ombe ya tambiko. Ndivyo, utumishi wa Nyumbani mwa Bwana ulivyotengenezwa tena.
36
Hizikia na watu wote wakafurahi kwa hayo, Mungu aliyowatengenezea watu, kwani jambo hili lilifanyika kwa upesi sana.
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 30 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36