bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 34
2 Chronicles 34
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 33
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 35 →
1
Yosia alikuwa mwenye miaka 8 alipoupata ufalme, akawa mfalme miaka 31 mle Yerusalemu.
2
Akayafanya yanyokayo machoni pake Bwana, akaendelea na kuzishika njia za baba yake Dawidi, hakuziacha na kujiendea kuumeni wala kushotoni.
3
Katika mwaka wa nane wa ufalme wake, yeye alipokuwa akingali mvulana, alianza kumtafuta Mungu wa baba yake Dawidi; tena katika mwaka wa kumi na mbili alianza kuitakasa nchi ya Yuda na mji wa Yerusalemu na kuyaondoa matambiko ya vilimani na miti ya Ashera na vinyago vingine vya kuchonga navyo vilivyoyeyushwa.
4
Usoni pake wakazivunjavunja meza za kuyatambikia Mabaali, nayo mifano ya jua iliyosimamishwa juu yao wakaikatakata, nayo miti ya Ashera na vinyago vingine vya kuchonga navyo vilivyoyeyushwa akavipondaponda, hata vikawa mavumbi, kisha hayo mavumbi akayamwaga juu ya makaburi yao waliovitambikia.
5
Nayo mifupa ya watambikaji wao akaiteketeza juu ya meza zao za kutambikia. Ndivyo, alivyoitakasa nchi ya Yuda na mji wa Yerusalemu.
6
Namo mijini mwa Manase na mwa Efuraimu, hata mwa Nafutali katika mahame yao yaliyokuwapo po pote
7
ndimo, alimozivunjavunja meza za kutambikia, akaiponda miti ya Ashera navyo vinyago vingine, hata vikawa mavumbi, nayo mifano yote ya jua akaikatakata katika nchi yote ya Isiraeli, kisha akarudi Yerusalemu.
8
Katika mwaka wa kumi na nane wa ufalme wake alipokwisha kuitakasa nchi na Nyumba hiyo, akamtuma Safani, mwana wa Asalia, na Masea, mkuu wa mji, na Yoa, mwana wa Yoahazi, aliyekuwa mwandishi wa mambo yaliyopasa kukumbukwa, kwenda kuitengeneza vizuri Nyumba ya Bwana Mungu wake.
9
Wakaja kwa mtambikaji mkuu Hilkia, wakampa zile fedha zilizopelekwa Nyumbani mwa Mungu, ambazo wangoja vizingiti walizikusanya kwao Wamanase na Waefuraimu na kwa Waisiraeli wote wengine na kwa Wayuda na Wabenyamini wote, hata kwa wenyeji wa Yerusalemu.
10
Wakazitia hizo fedha mikononi mwao wenye hiyo kazi waliowekwa kuzisimamia kazi za Nyumbani mwa Bwana; nao wenye hiyo kazi wakazipa wao waliozifanya kazi Nyumbani mwa Bwana za kuirudishia upya Nyumba ya Bwana kwa kuitengeneza vizuri.
11
Nao wakazipa maseremala na waashi za kununua mawe ya kuchonga na miti ifaayo ya kuungia na ya boriti za vipaa vya nyumba.
12
Watu hao walifanya kazi zao kwa welekevu; waliowekwa kuwasimamia katika kazi ni Walawi Yahati na Obadia waliokuwa wa mlango wa Merari, tena Zakaria na Mesulamu waliokuwa wa mlango wa Kehati. Nao walawi wote waliojua kupiga vyombo vya kuimbia
13
walikuwa kwao wachukuzi, nao wakawasimamia wafanya kazi wote, kila mmoja katika utumishi wake, tena walikuwako Walawi walio waandishi na wenye amri na walinda malango.
14
Walipozitoa zile fedha zilizopelekwa Nyumbani mwa Bwana, ndipo, mtambikaji Hilkia alipokiona kitabu cha Maonyo ya Bwana, aliyopewa Mose.
15
Hilkia akasema na kumwambia mwandishi Safani: Nimeona Kitabu cha Maonyo Nyumbani mwa Bwana! Kisha Hilkia akampa Safani hicho kitabu.
16
Safani akakipeleka hicho kitabu kwa mfalme, tena akampasha mfalme habari kwamba: Yote yaliyowekwa mikononi mwa watumishi wako, wao wanayafanya.
17
Fedha zilizooneka Nyumbani mwa Bwana wamezimimina, wakawapa wasimamizi mikononi mwao namo mikononi mwao wafanya kazi.
18
Kisha mwandishi Safani akamsimulia mfalme kwamba: Mtambikaji Hilkia amenipa kitabu; kisha Safani akasoma humo mbele ya mfalme.
19
Ikawa, mfalme alipoyasikia maneno ya Maonyo, akayararua mavazi yake.
20
Kisha mfalme akamwagiza Hilkia na Ahikamu, mwana wa Safani, na Abudoni, mwana wa Mika, na mwandishi Safani na Asaya aliyekuwa mtumishi wa mfalme kwamba:
21
Nendeni kuniulizia Bwana mimi na masao ya Waisiraeli na ya Wayuda kwa ajili ya maneno ya hiki kitabu kilichooneka, kwani makali ya Bwana yenye moto ni makuu, nayo humwagika kwetu, kwa kuwa baba zetu hawakulishika Neno la Bwana na kuyafanya yote yaliyoandikwa humu kitabuni.
22
Ndipo, Hilkia alipokwenda pamoja nao wa mfalme kwa mfumbuaji wa kike Hulda, mkewe Salumu, mwana wa Tokati, mwana wa Hasira aliyeyaangalia mavazi; naye alikaa Yerusalemu katika mtaa wa pili, wakamwambia maneno yaleyale.
23
Akawaambia: Ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema: Mwambieni yule mtu aliyewatuma kwangu:
24
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Mtaniona, nikileta mabaya mahali hapa, yawapate wenyeji wa hapa, ndio viapo vyote vilivyoandikwa katika kitabu, walichokisoma masikioni pa mfalme wa Wayuda,
25
kwa kuwa wameniacha, wakavukizia miungu mingine, wanikasirishe kwa matendo yote ya mikono yao; kwa hiyo makali yangu yenye moto yatamwagwa hapa, wala hayatazimika.
26
Naye mfalme wa Wayuda aliyewatuma kumwuliza Bwana mwambieni haya: Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema: Kwa kuwa hapo, ulipoyasikia maneno yale,
27
moyo wako umelegea, ukajinyenyekeza mbele ya Mungu papo hapo ulipoyasikia maneno yake, aliyoyasema ya mahali hapa na ya wenyeji wake, ukajinyenyekeza kweli mbele yangu na kuyararua mavazi yako na kunililia mimi, basi, kwa hiyo mimi nami nimekusikia; ndivyo, asemavyo Bwana.
28
Utaniona, nikikuita, uje kukutana na baba zako; ndipo, utakapopelekwa kulala kaburini mwako na kutengemana, macho yako yasiyaone hayo mabaya yote, nitakayopaletea mahali hapa na wenyeji wa hapa. Kisha wakampelekea mfalme majibu haya.
29
Ndipo, mfalme alipotuma wajumbe, akawakusanya wazee wote wa Wayuda na wa Yerusalemu.
30
Kisha mfalme akapanda kwenda Nyumbani mwa Bwana pamoja na Wayuda wote na wenyeji wa Yerusalemu na watambikaji na Walawi na watu wote pia, wakubwa kwa wadogo, akawasomea masikioni pao maneno yote ya kitabu cha Agano kilichooneka Nyumbani mwa Bwana.
31
Kisha mfalme akaja kusimama katika ulingo wake, akafanya mbele ya Bwana agano la kumfuata Bwana na kuyaangalia maagizo yake na mashuhuda yake na maongozi yake kwa moyo wake wote na kwa roho yake yote, ayafanye maneno ya Agano hilo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
32
Nao wote walioonekana mle Yerusalemu namo katika nchi ya Benyamini akawashurutisha kulisimamia hilo agano, nao wenyeji wa Yerusalemu wakafanya, kama Agano la Mungu aliye Mungu wa baba zao lilivyowatakia.
33
Kisha Yosia akaondoa kabisa matambikoi yote yatapishayo katika nchi zote zilizokuwa zao wana wa Isiraeli, nao watu wote walioonekana kwa Waisiraeli akawashurutisha kumtumikia Bwana Mungu wao, nazo siku zake zote za kuwapo hawakuacha kumfuata Bwana Mungu wa baba zao.
← Chapter 33
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 35 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36