bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 15
2 Chronicles 15
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 16 →
1
Roho ya Mungu ikaja kumkalia Azaria, mwana wa Odedi,
2
akamtokea Asa, akamwambia: Nisikilizeni, wewe Asa nanyi nyote Wayuda na Wabenyamini: Bwana yuko pamoja nanyi, mkiwa naye; mkimtafuta, atawaonekea ninyi, lakini mkimwacha, atawaacha nanyi.
3
Siku nyingi Waisiraeli walikuwa pasipo Mungu wa kweli, pasipo mtambikaji aliyewafundisha Maonyo.
4
Waliposongeka wakamrudia Bwana Mungu wa Isiraeli, wakamtafuta, naye akawaonekea.
5
Siku zile hawakupata kutengemana, wala aliyetoka, wala aliyeingia, kwani wenyeji wote wa nchi hizi walikuwa na mahangaiko mengi.
6
Ikasukumana, kabila na kabila nyingine, hata mji na mji mwingine, kwani Mungu aliwatisha na kuwasonga po pote.
7
Lakini ninyi jitieni nguvu, wala msiilegeze mikono yenu! Kwani matendo yenu yatapata mshahara wao.
8
Asa alipoyasikia hayo maneno ya ufumbuaji wa mfumbuaji Odedi akajishupaza, akayatowesha matapisho katika nchi yote ya Yuda na ya Benyamini, hata katika miji, aliyoiteka milimani kwa Efuraimu, nayo meza ya kumtambikia Bwana iliyokuwa mbele ya ukumbi wa Bwana akairudishia upya.
9
Kisha akawakusanya Wayuda na Wabenyamini wote nao waliokaa ugenini kwake, Waefuraimu na Wamanase na Wasimeoni, kwani wengi waliokuwa Waisiraeli walirudi upande wake walipoona, ya kuwa Bwana Mungu wake yuko pamoja naye.
10
Wakakusanyika Yerusalemu katika mwezi wa tatu wa mwaka wa kumi na tano wa Ufalme wa Asa,
11
wakamtolea Bwana siku hiyo ng'ombe za tambiko, walizozitoa katika mateka: ng'ombe 700 na kondoo 7000.
12
Wakaagana, wamtafute Bwana Mungu wa baba zao kwa mioyo yao yote na kwa roho zao zote,
13
kwamba: Kila asiyemtafuta Bwana Mungu wa Isiraeli auawe, mdogo kwa mkubwa, mume kwa mke.
14
Wakamwapia Bwana kuyafanya hayo wakipaza sauti za kumshangilia na kupiga matarumbeta na mabaragumu.
15
Wayuda wote wakakifurahia hicho kiapo, kwani waliapa kwa mioyo yao yote; kwa kuwa walimtafuta Bwana kwa kupendezwa kabisa, akawaonekea, akawapatia kutulia pande zote.
16
Mfalme Asa akamwondoa naye mama yake Maka katika ukuu wake, kwa kuwa alitengeneza kinyago cha Ashera, nacho kinyago chake Asa akakikatakata na kukipondaponda, kisha akakiteketeza penye kijito cha Kidoroni.
17
Lakini matambiko ya vilimani hayakutoweka kwao Waisiraeli, lakini moyo wake Asa ulikuwa mtimilifu siku zake zote.
18
Navyo, baba yake alivyovitakasa, pamoja navyo alivyovitakasa mwenyewe, fedha na dhahabu na vyombo, akavipeleka Nyumbani mwa Mungu.
19
Vita havikuwako hata mwaka wa 35 wa ufalme wa Asa.
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 16 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36