bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Chronicles 31
2 Chronicles 31
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 30
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 32 →
1
Walipokwisha kuyamaliza hayo yote, Waisiraeli wote waliokuwako wakatoka kwenda zao katika miji ya Yuda, wakazivunja nguzo za kutambikia, wakaikatakata nayo miti ya Ashera, wakavibomoa vijumba vya kutambikia vilimani pamoja na meza zao za kutambikia katika nchi zote za Yuda na za Benyamini na za Efuraimu na za Manase, mpaka wakavitowesha kabisa hivyo vyote, kisha wana wote wa Isiraeli wakarudi kila mtu mahali palipokuwamali yake katika miji yao.
2
Kisha Hizikia akaweka kazi za zamu za watambikaji na za Walawi zizipasazo zamu zao, kila mtu akawa na kazi yake ya utumishi wake, watambikaji na Walawi: kuteketeza ng'ombe za tambiko na kutengeneza ng'ombe za tambiko za shukrani na kutumikia malangoni kwa matuo yake Bwana na kumshukuru na kumshangilia.
3
Akayaweka nayo yampasayo mfalme kuyatoa katika mali zake kuwa ng'ombe za tambiko za asubuhi na za jioni na za matambiko ya siku za mapumziko na ya miandamo ya mwezi na ya sikukuu, kama ilivyoandikwa katika Maonyo ya Bwana.
4
Tena akawaagiza watu waliokaa Yerusalemu kuwapa watambikaji na Walawi yawapasayo, wapate kuyashika Maonyo ya Bwana.
5
Agizo hili lilipoenea, wana wa Isiraeli wengi wakaleta malimbuko ya ngano na ya mvinyo na ya mafuta na ya asali na ya mazao yote ya mashamba, wakayaleta nayo mafungu ya kumi ya mali zote, yakawa mengi.
6
Nao wana wa Isiraeli na wa Yuda waliokaa katika miji ya Yuda wakaleta nayo mafungu ya kumi ya ng'ombe na ya mbuzi na ya kondoo nayo mafungu ya kumi ya vipaji vitakatifu vilivyotolewa kuwa mali za Bwana Mungu wao, wakaviweka machungu machungu.
7
Katika mwezi wa tatu walianza kuyaweka hayo machungu, wakayamaliza katika mwezi wa tisa.
8
Ndipo, Hizikia na wakuu walipokuja kuyatazama hayo machungu, wakamtukuza Bwana nao Waisiraeli walio ukoo wake.
9
Hizikia alipoulizana na watambikaji na Walawi maana ya hayo machungu,
10
Azaria aliyekuwa mtambikaji mkuu wa mlango wa Sadoki akamjibu, akamwambia: Tangu hapo, walipoanza kuyaleta haya matoleo Nyumbani mwa Bwana, tumekula na kushiba, nayo haya mengi ndiyo yaliyosalia, kwani Bwana amewabariki walio ukoo wake, kwa hiyo vimesalia hivyo vipaji vingi mno.
11
Ndipo, Hizikia alipoagiza, watengeneze vyumba katika Nyumba ya Bwana: walipokwisha kuvitengeneza,
12
wao kwa kuwa welekevu wakaingiza humo yale matoleo na mafungu ya kumi na vipaji vitakatifu vyote pia, Mlawi Konania akawekwa kuyaangalia, naye ndugu yake Simei akawa wa pili.
13
Nao Yehieli na Azazia na Nahati na Asaheli na Yerimoti na Yozabadi na Elieli na Isimakia na Mahati na Benaya wakawekwa kuwa wasimamizi kumsaidia Konania na ndugu yake Simei kwa agizo lake mfalme Hizikia na Azaria aliyekuwa mwenye amri Nyumbani mwa Mungu.
14
Tena Mlawi Kore, mwana wa Imuna, aliyelilinda lango lililoelekea maawioni kwa jua akawekwa kuviangalia vipaji vya Mungu, watu walivyovitoa kwa kupenda kwao wenyewe, agawe yaliyo matoleo ya Bwana nayo yaliyo matakatifu yenyewe.
15
Waliomsaidia katika miji ya watambikaji ni Edeni na Minyamini na Yesua na Semaya na Amaria na Sekania, wawagawie kwa kweli ndugu zao yawapasayo kwa zamu zao, mkubwa kwa mdogo,
16
kuliko wale wanawaume walioandikwa katika kitabu chao walio wa miaka mitatu na zaidi; nao hawa ndio wote waingiao Nyumbani mwa Bwana kwa mambo ya kila siku moja kufanya kazi za utumishi wao ziwapasazo kuziangalia kwa zamu zao.
17
Katika kile kitabu cha udugu wa watambikaji imeandikwa milango ya baba zao, nacho cha Walawi kimeandikwa walio wenye miaka ishirini na zaidi kwa kazi zao ziwapasazo kuziangalia kwa zamu zao.
18
Humo katika kitabu cha udugu wakaandikwa nao watoto wao wadogo wote na wake zao na wana wao wa kiume na wa kike wa mkutano wote pia, kwani kwa kuwa welekevu walijitakasa kuwa watakatifu kweli.
19
Nao wana wa Haroni waliokuwa watambikaji mashambani kwenye mitaa ya miji yao wakapata watu katika kila mji mmoja walioandikwa majina yao, wawagawie yawapasayo, kila mume mmoja fungu lake miongoni mwa watambikaji, namo mwa Walawi wote walioandikwa katika kitabu cha udugu.
20
Ndivyo, Hizikia alivyofanya katika nchi yote ya Yuda, akayafanya yaliyokuwa mema na manyofu na ya kweli machoni pake Bwana Mungu wake.
21
Nazo kazi zote, alizozianza za kuitumikia Nyumba ya Mungu na za kuyafuata Maonyo na maagizo, kwa hivyo, alivyomtafuta Mungu, akazifanya kwa moyo wake wote, akafanikiwa.
← Chapter 30
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 32 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36